Ufugaji wa Kuku aina ya Kuchi na masoko yake ndani na nje ya Tanzania

Ufugaji wa Kuku aina ya Kuchi na masoko yake ndani na nje ya Tanzania

Kuchi wa ukweli
 

Attachments

  • 1450806745965.jpg
    1450806745965.jpg
    38.1 KB · Views: 822
Hawa kuku wana kipi cha ziada cha tofauti na kuku wengine? Kwa minajili ya Nyama, mayai nk??
Ukiondoa hizo pia wanapendelewa zaidi katika mashindano ya kupigana ambapo watu wanawatumia kucheza kamari.
 
Tayari nimepata contact za dogo Mafia, tumekubaliana kuwa yy atakuja nao mpaka Nyamisati Bandarini, kila kuchi original bei ni Tsh 50,000/ wanaoanza kuwika au wale ambao bado kuwika, na Chotara iwe buku 30,000/. Kwa hiyo aliye tayari atume pm au hapa hapa jamvini aseme, mimi nimeagiza kuchi original kumi kwa ajili ya mbegu. Chotara nitawapata Ikwiriri na Kuruti kisiwani.

Ni vizuri anayetaka aseme na jinsia ya kuchi,isije jamaa akakusanya madume mengi badala ya majike mengi.
Mkuu malila ulifanikiwa kuwafuga hawa ndege? Sehemu gan huko ikwiriri wanapopatikana?
 
Unapo hitaji kuku kuchi wa ukweli, ni pm nipo Zanzibar.
Watu wengi wanachangia lakini wengi wetu, hatuwafahamu vizuri hao kuchi, au kama wanawafahamu basi wanashindwa kujua soko la hao kuku.
Kiufipi sio kila kuchi atakuwa na bei kubwa, vitu vifuatavyo ndo vina determine bei ya kuchi.
1. Mdomo wake, ukiwa mdomo ni mfupi na nimnene sana. Anakuwa na bei nzuri ukilinganisha na mdomo mfupi, mwembamba au mrefu.
2. Kichwa kinene kwa kuku kuchi kinampandisha thamani kuliko kichwa kidogo.
3. Shingo, shingo ndefu inakuwa na bei kubwa kuliko shingo fupi.
4.Urefu wa kuku, mrefu ana bei kubwa kuliko mfupi.
5. Kusima, kuku anatakiwa asimame yani awe muda wote amenyanyua shingo na kifua asiwe anatembea kama ngombe au mbuzi.
6. Upanga wa kichwani, upanga selaini unampunguzia kuchi thamani na upange wa jiwe unampa thamani zaidi.
7. Asili ya kuku wenyewe, kuku wateja wanaemfahamu baba yake na mama yake huwa anathamani kubwa kuliko kuku kuchi humfahamu ukoo wake.
8. Kuzalisha kuchi kama alivyo yeye, hii inategemea na ukoo wa kuchi husika akiwa full kuchi baba na mama anaposibility kubwa ya kuzalisha vifaranga kama yeye, hivyo huwa na bei kubwa kuliko asiweza kujizaa.
Kuku wengi wamikoani ni risk kuwanunua kwa sababu hawafugwi kwa kuzingatia koo zao, wanawachanganya kuku wa aina tofauti, hivyo ktk mazingira hao mteja hawezi kutoa fedha nyingi kwani ni risk hata kama umemkuta mzuri.
Na sio kweli kuwa majike ya kuchi huwa wadogo,
Angalia picha nilizoziweka kwenye thread zangu
 
Kama wewe ni mkulima na mfugaji kwa vitendo na ungependa kujumuika na wakulima wenzako whatsapp 0717269137 (kama haulimi wala kufuga haikuhusu) WE NEED SERIOUS PEOPLE
 
Alichokiandika mtoa mada kina ukweli hao kuku ninao na niliwanunua wakiwa wadigo kabisa yaani ndiyo wanaanza kuota manyoya nikauziwa kifaranga15000 mpaka 20000 saa hizi ninao na ninawauza nipo Geita #+255712946988
 
Habari zenu wadau..naitwa David napatikana Ubungo Kona...nina majogoo ya KUCHI na Majike..nimewatoa katika jamii za wasukuma wanaopataikana katika wilaya ya ulanga huko morogoro katika kijiji cha Itete...kama unahitaji nicheki kupitia hii namba 0717578551 kwa ajili ya maelewano
Hey kiongozi bado una hao kuku wa KUCHI?? nawaitaji
 
Alichokiandika mtoa mada kina ukweli hao kuku ninao na niliwanunua wakiwa wadigo kabisa yaani ndiyo wanaanza kuota manyoya nikauziwa kifaranga15000 mpaka 20000 saa hizi ninao na ninawauza nipo Geita #+255712946988
sasa unauzaje?
 
Yaani hata kama IQ zetu zimeshuka kiasi gani huo ni uchizi of the highest degree
 
Alichokiandika mtoa mada kina ukweli hao kuku ninao na niliwanunua wakiwa wadigo kabisa yaani ndiyo wanaanza kuota manyoya nikauziwa kifaranga15000 mpaka 20000 saa hizi ninao na ninawauza nipo Geita #+255712946988
Sikiliza. Wewe umeshaninua. Sasa hivi na Wewe unatafuta wa kumuuzia. Kama utampata mwenye mawazo uliyokuwa nayo wakati ule unanunua, unaweza kuuza. Ila ktk hali halisi hiyo siyo biashara endelevu. Ni kubahatisha watu wasiyojielewa. Ninunie kuku shs 200,000/= kwa sababu gani hasa. Nyama nzuri, mapambo au bondia wa maonyesho ya mapambano? Mimi siwaelewi. Naona kama mlipoteza hela zenu kwa maneno ya kuambiwa. Samahani lakini huenda nimetumia lugha kali kuonyesha hisia yangu
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Hvi ukipata bingo voda au airtel ya million 100 kwa mfano unaweza ukaiambia kadamnasi kuwa mtandao Fulani instead million mia? Hamishia wenye kuku hao sasa
 
Back
Top Bottom