Unapo hitaji kuku kuchi wa ukweli, ni pm nipo Zanzibar.
Watu wengi wanachangia lakini wengi wetu, hatuwafahamu vizuri hao kuchi, au kama wanawafahamu basi wanashindwa kujua soko la hao kuku.
Kiufipi sio kila kuchi atakuwa na bei kubwa, vitu vifuatavyo ndo vina determine bei ya kuchi.
1. Mdomo wake, ukiwa mdomo ni mfupi na nimnene sana. Anakuwa na bei nzuri ukilinganisha na mdomo mfupi, mwembamba au mrefu.
2. Kichwa kinene kwa kuku kuchi kinampandisha thamani kuliko kichwa kidogo.
3. Shingo, shingo ndefu inakuwa na bei kubwa kuliko shingo fupi.
4.Urefu wa kuku, mrefu ana bei kubwa kuliko mfupi.
5. Kusima, kuku anatakiwa asimame yani awe muda wote amenyanyua shingo na kifua asiwe anatembea kama ngombe au mbuzi.
6. Upanga wa kichwani, upanga selaini unampunguzia kuchi thamani na upange wa jiwe unampa thamani zaidi.
7. Asili ya kuku wenyewe, kuku wateja wanaemfahamu baba yake na mama yake huwa anathamani kubwa kuliko kuku kuchi humfahamu ukoo wake.
8. Kuzalisha kuchi kama alivyo yeye, hii inategemea na ukoo wa kuchi husika akiwa full kuchi baba na mama anaposibility kubwa ya kuzalisha vifaranga kama yeye, hivyo huwa na bei kubwa kuliko asiweza kujizaa.
Kuku wengi wamikoani ni risk kuwanunua kwa sababu hawafugwi kwa kuzingatia koo zao, wanawachanganya kuku wa aina tofauti, hivyo ktk mazingira hao mteja hawezi kutoa fedha nyingi kwani ni risk hata kama umemkuta mzuri.
Na sio kweli kuwa majike ya kuchi huwa wadogo,
Angalia picha nilizoziweka kwenye thread zangu