habari ndungu zangu!namhukuru sana Mungu kwa kuujua uzi huu.Zamani wakati nikiwa kijana mdogo niliamini ili uweze kufanikiwa kwenye ufugaji wa kuku nilazima uwe na kalama au mkono wa kuku,mara nyingi ktk familia yetu huko kijijini tulikuwa tunafuga kuku mimi na ndugu zangu hatahivyo mimi nilikuwa nabaki mwisho kwa kuwa na idadi ndogo au kutokuwa na kuku hata mmoja hii ilisababishwa na kufa kwa vifaranga pia kufa kwa kuku wakubwa kwa magonjwa na sababu zingine ila kuna mdogo wangu yeye alikuwa anafanikiwa sana kwenye ufugaji wa kuku kuliko wote hivyo ikaaminika kuwa huyo mdogo wangu anamkono wa kuku na mimi sina mkono wa kuku.binafsi nilikuwa napenda sana kufuga kuku lakini nikikumbuka kuwa sina mkono wa kuku najisikia vibaya ila siku moja mwanzoni mwanzoni mwa uzi huu mwaka 2013 niliamua kutoa dukuduku langu humu nashukuru nilipata ushauri ambao ulinitia moyo hadi kufikiria kuanza ufugajia.Baada ya kuweka mazingira vizuri nikaanza ufugaji wa kuku wakienyeji na chotara na mrejesho niliuleta humu ndani page na.43.Uwezi amini matokeo ya ufugaji huo hususani nwaka jana yalikuwa mazuri sana kwani tangu nianze kufuga kuku sikiwahi kuwa na kuku wengi kama wale tena nilikuwa nawafuga huria niliwauza xmass,mwaka mpya na pasaka na bado nina kuku ambao wao nimewaacha kama wazazi.Ninacho taka kushauri tuachane na mambo ya imani zinazo katisha tamaa na kutia hofu mimi naamini ukiwa na maarifa ya kutosha juu ya jambo fulani inatosha kwa asilimia 95 kufanikiwau
Hakika nlipata sana ujuzi kupitia huyu brother na kama site yeye pengine nsingekuwa jf kabisa ama ngechelewa mda kuifahamu. Cc Kubota thanks in advance my brother.Mungu akujalie maisha marefu bro Kubota. Watu makini wanajua mchango wako hapa JF.
. Mashamba huko wanauzaje kwa heka moja mkuu?Mm nahamia Tanga mwezi wa saba, nmefika maeneo ya Pande. Naplan kufanya hii biashara make nshaifanyaga...
Kwa wale wanaoitaji kuku wakienyeji mim nawauza.. Mashamba huko wanauzaje kwa heka moja mkuu?
Kifaranga wa kuchi wa wiki tatu unauza bei gani?Kwa wale wanaoitaji kuku wakienyeji mim nawauza.
1:Nauza vifaranga kuanzia cha siku Moja mpaka wk
Tatu.
2: Nauza vifaranga vya kuroila kuanzia siku moja mpaka wk tatu:
3: Nauza vifaranga vya kenbro kuanzia siku moja mpaka wk tatu
4: Nauza vifaranga vya Kuchi kuanzia siku moja mpaka wk tatu.
Shamba liko mkoa wa Tanga na Arusha.
Napatikana kwa number 0762355114
Angeweka na bei ingekua vizuri zaidi.Kifaranga wa kuchi wa wiki tatu unauza bei gani?