Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Lakini ukimuwekea mayai viza akaendelea kuatamia halafu baadae ukaweka mayai mazima ili aanze pamoja na wenzake..huoni kama atatotoa kabla akizngatia muda alioanza kuatamia
Mayai hayawezi kutotolewa kabla hayajaatamiwa siku 21,hivyo ataatamia tu mpaka siku 21 zifikie na kutotoa sawa na wenzake
 
Habari wadau?ninaomba msaada wa dawa ya nzuri ya viroboto.maana kuku wngu wanasumbuliwa saana na voboto.
 
Mkuu kuku anaweza kukaa mpaka miezi(siku 60) miwili akiatamia mayai yake.
Kinachotakiwa umpe tu chakula na maji lakini pia ukumbuke kuku ana "intelligence" ya kumuwezesha kuacha mayai masaa kama 72 hivi toka kifaranga wa kwanza atotolewe, uwezo huu alipewa na Mungu.

Kama hakuna yao hata moja litakalototolewa, ataendelea kulalia tu mpaka siku 60, na hapa ndipo wajasiriamali huwa wanacheza napo
kwa kuongezea ni kwamba katika mayai anayo atamia akitotolewa kifaranga hata mmoja baada ya masaa 72 hata kama kutakuwa na mayai mengine mazima kuku ulazimika kutoka nje na kutokuendelea kuatamia ili akamlishe/akawalishe vifaranga waliototolewa maana wanakuwa wanasikia njaa.
 
WEWE TAPELI TU
MANENO MENGIIII KAZI KUTAPELI WATU HUNA LOLOTE
 
mtoa mada anatuletea vitu nusunusu bhana
teh teh teh
mkuu umeusoma huu uzi lakini, ni moja ya nyuzi bora sana hapa JF.

Uzi umefika mpaka page ya 46 unasema ina vitu nusu?? au umeishia page 1 tu ukakatia tamaa njiani??
 
Daaaaah mimi nahisi nimefaidika sana na huu uzi daaaah yani nimepata knowledge kubwa sana.
Lakini nina swali kwa wataalamu mimi nina kuku wangu chotara je wataweza kutaga na kutotoa vifaranga?
 
teh teh teh
mkuu umeusoma huu uzi lakini, ni moja ya nyuzi bora sana hapa JF.

Uzi umefika mpaka page ya 46 unasema ina vitu nusu?? au umeishia page 1 tu ukakatia tamaa njiani??
Asante asigwa........hata mimi acha nicheke kwi kwi kwiiiii
 
kweli? maana naona mtoa mada ameishia katikati na kuingia mitini!!
Daaaaaaaaa hunitendei haki mkuu, ridhika na kidogo nilichochangia, najua unavutiwa sana na uwasilishaji wangu ambao umeu-miss hadi unapata hasira hahahahaaa, .....ninafarijika ninapouona uzi unaendelea kuwa mrefu zaidi na wachangiaji wapo wengi na wamebobea sana sana mmoja wao ni huyu mkuu sana ASIGWA........asante sana sana Mkuu Asigwa
 
Daaaaah mimi nahisi nimefaidika sana na huu uzi daaaah yani nimepata knowledge kubwa sana.
Lakini nina swali kwa wataalamu mimi nina kuku wangu chotara je wataweza kutaga na kutotoa vifaranga?
Mkuu kuku chotara anakua na tabia nusu za kisasa nusu za kienyeji, mara nyingi (almost 80%) wanataga na kutotoa vifaranga.

Kinachotakiwa ni kuwa na majogoo chotara kama wao au kuwa na majogoo ya kienyeji kabisa, ukiweka majogoo ya kisasa kwa kuku chotara inaleta mushkeli kidogo.

Tatizo kubwa la kuku chotara ni baadhi kutokuwa na tabia ya kulali mayai japo si wote, ila ukiyachukua hayo mayai ukampa kuku mwingine mwenye uwezo wa kuatamia au ukaweka kwenye mashine ya kutotoleshea, yanaanguliwa tu kama ya kienyeji
 
Sawa mkuu ngoja nione kuwa je hawa wangu watakua na tabia gani
 
Back
Top Bottom