Mkuu kuku chotara anakua na tabia nusu za kisasa nusu za kienyeji, mara nyingi (almost 80%) wanataga na kutotoa vifaranga.
Kinachotakiwa ni kuwa na majogoo chotara kama wao au kuwa na majogoo ya kienyeji kabisa, ukiweka majogoo ya kisasa kwa kuku chotara inaleta mushkeli kidogo.
Tatizo kubwa la kuku chotara ni baadhi kutokuwa na tabia ya kulali mayai japo si wote, ila ukiyachukua hayo mayai ukampa kuku mwingine mwenye uwezo wa kuatamia au ukaweka kwenye mashine ya kutotoleshea, yanaanguliwa tu kama ya kienyeji