GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Uko wapi mkuu?Hongera kwa ujasiriamali mkuu, nadhani wenzangu wanatoa malezo ya hoja yako, naomba kujua soko la kuku nikitaka kuuza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko wapi mkuu?Hongera kwa ujasiriamali mkuu, nadhani wenzangu wanatoa malezo ya hoja yako, naomba kujua soko la kuku nikitaka kuuza
Njombe mkuuUko wapi mkuu?
Huku Mtwara huwezi kuuliza soko la kuku, wanauzika sana tena bei inafika mpakaNjombe mkuu
[emoji106]Kwanini usitoe somo Hapa watu wengine wakapata kujua na kuelewa?
Huko pm unataka kufanyanuchoyo SAS mkuu,weka mambo hadharani ufaidishe wengi na uelimishe wengi
Umenikumbusha mbali sana hii picDawa ni hii
Wapake rangi ya Ukili au ile rangi inayopakwa kwenye Mikeka yaani wapake kiwiliwili chote, kuna rangi nyekundu,blue manjano au yeyote ile hii itamfanya kuku aonekane kiumbe cha Ajabu![]()
![]()
Mkuu weka wavu wa juu hapo bandani kwaoUko wapi mkuu?
Nilikuwa sijaliona hili swali (Samahani)1. Huu kwa juu ni wavu?
2. Wanakaa humu kwa muda gani baada ya kutotolewa?
3. Unaweza taa au chungu chenye moto ili wapate joto?
4. Chakula unawapa kiasi gani kwa siku let's say wapo 15 kwenye box?
Samahani kwa maswali mengi mkuu.
Asantee sana kwa majibu yako yaliyoshiba na kujitosheleza...kwa kweli umenipa elimu kubwa sana sana,Mungu akubariki mno...Nilikuwa sijaliona hili swali (Samahani)
Kwanza haya unayoyaona ni mabox ya pikipiki, huku tunanunu 5000 mpaka 10,000
na wakati mwingine huwa yanatupwa na wauzaji. (Uliza kwa watengenezaji au wauza pikipiki)
1.Hayo maboksi yanakuja na mifuniko, mimi nimekata sehemu ya juu ya mfuniko nikaziba
kwa waya wa Dirishani kama unavyoonekana.
2. Wengi huwaweka hadi pale wanapoweza kuruka na kutoka nje ya box, binafsi sina mudaa maalumu
Wakishatotoa wengine huwa naangalia box ambalo wamekomaa nawaondoa na kuwaweka wapya
3. Wakati wa joto siweki chohote, wakati huu wa baridi huwa nawawekea hiyo mitungi
ambayo nimeiweka kwenye picha huku tunanunua kwa 3000 mpaka 5000. Kunambinu nili
fundishwa ya kuufanya mkaa udumu muda mrefu bila kuzimika au kuisha, huwa njaza unga
unga au chenga za mkaa hapo juu, pia huwa naloweka jivu na kuliweka (Uliza kwa wauza kahawa
watakuelekeza vizuri zaidi)
4.Huwa nawakadiria tu, wakimaliza nawaongezea tena. Machicha ya nazi, pumba za mahindi
' Pumba za dagaa n.k isipokuwa siku 3 za mwanzo naweza kuwapa kile kilichochanganywa kwa
ajili ya vifaranga, maa nyingi nanunua kwenye maduka ya kilimo.
Ahsante kwa maelezo mazuri mkuu...Ni hivi Kuku wa Kienyeji wanapenda Kujiachia Tengeneza Vidude Vya Kutagia juu. Kuku wakishatotoa wakae na Watoto Wiki Moja Nenda kwa wauza Dawa za Mifugo mwambie akupe Dawa ya Makoti na Baadhi ya Dawa za Vitamin
Baada ya Hapo wale Watoto wanatunzwa Tofauti wakuu hasa Ujiku inatakiwa wakae kwenye Joto sasa kuna Mawili Unaweza ukawasha jiko la mkaa Usiku na Asubuhi au Ukafunga Bulb zenye Joto hadi wapate Mikia tetea huwa wana mikia mirefu vijogoo vina mikia mifupi utaviona tuu na vichwa Huwa vikubwa vikipata mikia Hapo Uwezekano wa Kupona Vyote upo
Chakula Please Usiwalishe Pumba Mwanzo Mwisho na hizo Dawa watakua wanakunywa kila baada ya siku tatu Isikae masaa 24 huwa ni Sumu ikae Masaa 8 tuu then Unabadilisha
Walishe
-Pumba
-Mboga za Majani Fungu hata Moja la Chinese
Sasa baada ya Kuwapa hivyo vyakula Mimi kimsingi huwa nafurahia wanavyokula vikishashiba Unaweza Ukawapa Chenga za Dagaa ndo uwape Maji au Ukawapa Maji ndo ukawapa Dagaa.
Kuna Siri Moja Dagaa hata kama kinaumwa kitakula tuu ni chakula ambacho Watoto wanakipenda sana na wanakua haraka ukiwapa Dagaa
Mara Moja Moja vipe Mchele pia vinaupenda Mahindi hawawezi Kumeza
Ukizingati ndani ya mwezi vinakua Vikubwa tayari kwa kutoka Nje
Hakikisha Banda lako Unasehemu za Kuwatenga kutokana na Umri si vizuri Kuku wadogo unaenda kuwachanganya na Waliozeeka kuna baadhi ya Jogoo huwa wanawaua Watoto.
Hakikisha Vyombo vya Maji Unavisuuza na wakiwa watoto usiwape Pumba uliyoloweka kwenye maji, pia Wakishakunywa Maji toa Yale Maji At least wapewe Mara 3 kwa Siku lakini kama uko Busy Maji yasikua na Dawa wanaweza Kushinda Nayo
Mkuu ukizingatia hayo kama Una matetea 15 wakitaga wote Nategemea Utawaponesha Kuku 160. Pia control Kwenye kuatamia at least atamie Mayai 13 hadi kwenye 10 pia uwe Mjanja kuchagua koo za Kuku kuna wengine wanataga sana wengine wao kufikisha Mayai 12 issue kuna wengine wanatotoa sana kuna mwingine akiatamia Mayai 14 anatotoa Watoto 2 Kuku hawa ni stress na Ukishaona Hivyo subiri anenepe tuu Umle Kuku wa aina hii Mara Nyingi Ni wale uliowanunua wakiwa wakubwa na Unajua mbongo anauza Kitu Kikiwa kina matatizo.
Uko wapi? Unafanya Nini? Nataka nijue mwingine yupo kwenye Nyumba za Kupanga anataka Kufuga KukuAhsante kwa maelezo mazuri mkuu...
Mimi nina kamtaji ka 2.2m, je katatosha kuanza ufugaji wenye tija mkuu.
Pia naomba kujua ni kipi bora kati ya kufuga kuku wa kienyeji na wale matahira(wa kisasa)?
Note: nahita kufuga kwaajili ya biashara na sio kitoweo tu.
Nipo Dar mkuu....Uko wapi? Unafanya Nini? Nataka nijue mwingine yupo kwenye Nyumba za Kupanga anataka Kufuga Kuku
wapi umekumbukaUmenikumbusha mbali sana hii pic
Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.Nipo Dar mkuu....
Na nipo kwenye nyumba ya kupanga,
Nashukuru kwa ushauri mkuu... Kwa sasa kuondoka Dar haitakuwa rshisi maana kuna sehemu bado fanya kazi japo kipato sio kikubwa sana lakini nashukuru kimeniwezesha kuweka akiba ya hicho kiasi mkuu... Pia nimeoa mkuu........!!Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.
1.Vifaranga vya kuku bei gani,,
Jibu:
Umri Bei (Tsh)
Siku 1 2,000/=
Wiki 2 3,000/=
Mwezi 1 3,500/=
2.ni vya umri gani
Jibu:
Kulingana na uhitaji wa mhusika tunaanza kuuza kuanzia wa siku moja na kuendelea
3.mnaanza kumplkea mtu kwake akichukua idadi kuanzia vingap
Jibu:
Order yeyote hata 1,000pcs tunapokea
4.je kuna ushauri wowote mnatoa kwa mtu hasa anaeanza ufugaji mara ya kwanza namn ya kufuga
Jibu:
Ndio tunatoa ushauri kabisa
5.Pia chanjo za mwanzoni mnazo hapo kwenu au mpka mtu aende duka la madawa ya mifugo kupata hizo chanjo,,,,asante…!!