Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Pia ni vyema kama mna species tofauti ungezitoa ili kujua ni zipi nzuri hasa katik kukua ,,utagaji wa mayai na kuhimili magonjwa…!!


Tunao
Kuku wa malawi - weusi wanafaa kwa mayai na nyama pia, hustahimili magonjwa, huwa na uzito mkubwa
Chotara - Wanafaa kwa mayai na nyama, huwa na uzito mkubwa
Kloiler - Wanakuwa kwa haraka na wanafaa kwa mayai na nyama. huwa na uzito mkubwa
 
Tunao
Kuku wa malawi - weusi wanafaa kwa mayai na nyama pia, hustahimili magonjwa, huwa na uzito mkubwa
Chotara - Wanafaa kwa mayai na nyama, huwa na uzito mkubwa
Kloiler - Wanakuwa kwa haraka na wanafaa kwa mayai na nyama. huwa na uzito mkubwa
Asante sana ndgu kwa maelezo yako mazuri,, ntakuja tuoane ,tufany biashara mkuu…!!
 
vidonda huo ni ugonjwa unaitwa ndui na una chanjo yake unatakiwa kuwachanja hao kuku kabla hawaugua na wakiugua tumia iodine kuwapaka baada ya kuwasafisha vidonda, kwa sasa kuna dawa ya tiba pia hebu muone mtaalam alie karibu nawe. Kwa upande wa kuku chanjo ni muhimu sana na pia usikose kufanya kazi kwa karibu na wataalam wa mifugo.
Kiongozi ni iodine tincture au ipo ingine? maana hata WA kwangu naona ugonjwa unaanza.
 
Mkuu kwanza pole,nenda duka la dawa na nunua vidonge vya PEN V. Chukua vidonge 5 weka kwenye maji Lita moja na wape hao kuku wako kwa ck 3-5. Utaona matokeo ndani ya ck 3. Nakuomba ulete mrejesho maana hio dawa ni mujarabu.

Mkuu nashukuru na Juma tatu ntaianza hii kisha ntaleta Mrejesho
 
Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.
Kaka Troll na wana jf mliomo humu naomba munipe mawazo yenu katika hili,,,

Mimi niko chuoni, nimeona nianze ufugaji kupitia boom langu, nimeamua ninunue kuku kumi huku mbeya but mimi nyumbani ni mwanza, mbeya ni kwa dada yangu, dada yeye ana uwanja mkubwa sana hivyo nilipomtem
Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.
Kaka Troll na wana jf mliomo humu naomba munipe mawazo yenu katika hili,,,

Mimi niko chuoni, nimeona nianze ufugaji kupitia boom langu, nimeamua ninunue kuku kumi mbeya but mimi nyumbani ni mwanza, mbeya ni kwa dada yangu, dada yeye ana uwanja mkubwa sana hivyo nilipomtembeea nikaona nimuulize kama naweza kuweka mifugo yangu kwake akaitunza , alikubali, yeye dada ni mkulima hivo ni mtu wa shambani sana, naombeni mnipe ujuzi jinsi navoweza kumwelekez ili kuku wakue vizuri mimi nikiwa mbali na ukizingatia pia ndio kwanza nimeanza ufugaji, na mawazo haya ni kutokana na inspiration kubwa niliyoipata hapahapa jf, hivyo naombeni sana ndgu zangu, mdogo wenu nimeamua nifanye kufuga hivyo mawazo yenu ni muhimu sana, naombeni msinikatishe tamaa ikiwa ndio niko stage za mwanzoni…!!
 
mimi nilikuwa na changamoto ya kuibiwa kuku mama watoto akaenda kwa mtaalam mwizi alipatikana kesho yake baada ya kuiba jogoo kubwa nakulila na mkewe. Jamaa alijileta mwenyewe akiwa anaumwa tumbo balaa na mke wake huku jogoo akiwika mfululizo tumboni alitaja mwenyewe kila alichoiba kwangu na kwa majirani. Alitozwa faini ya ng'ombe sita kama fidia kwangu na majirani ng'ombe moja wakachinja nyama. Tangu siku hiyo mambo swali kabisa , mwaka huu hata shamba la mahindi sikuweka mlinzi. Kumbe duniani kuna ulinzi asilia sikuwa naamini.
KAMA NI KWELI NAOMBA MSAADA WAKO TAFADHALI
 
Kuna Babu huku kwetu Aliibiwa Jigoo lake kubwa tu, akaamua kutangaza kijiji kuzima ya kwamba aliyeiba kwa makusudi au bahati mbaya ajitokeze na aendee.

Ikapita kama siku kadhaa hivi kimyaa hakuna aliyejitojeza, basi akatangaza kusoma HALALBADIRI pia hakuna aliyejitokeza.

Baada Ya siku tatu Akasoma HALALBADRI Kabla kumaliza kusoma Kilichotokea Sitasahau maana Lilitoka CHATU porini kubwa kweli kweli likamtema yule Jogoo pale kijijini mbele za watu. Ilikuwa Nouma sana

Hawa Wazee ni nouma
 
Huyo ndege atakuwa ni kipanga au mwewe. Zamani utotoni tulikuwa tunawatega na tunawakamata tunawachoma na kuwala.
 
Wakuu, nimeanza tena ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mara hii natumia mfumo
wa NUSU HURIA nimeanza na kuku 15 mwaka Jana mpaka sasa wako 369
Nimeuza kuku 271 kwa bei za kati ya Tsh 17,000 mpaka 23,000 namshukuru
Mungu nimeweza kupunguza ukata.

Mwakahuu kuna ttizo kubwa limejitokeza nashindwa jinsi ya kulikabili, Kuna ndege
Mdogo kwa umbo anafanana sana na njiwa, anakamata vifaranga balaa. Tena
anakamata wale vifaranga wakubwa ambao wanajitegemea. Ndani ya wiki mbili
hizi amekamata vifaranga 18.

Sijajua jinsi ya kumdhibiti yaani huyu mshenzi ananipa hasira si mchezo.

Dawa hapo nikuwapaka RANGI NYEKUNDU ya ukili ile tu.
 
Habari wana jamii..
Nauza mayai ya kienyeji trey kwa 13500 nipo moshi kilimanjaro ila wing wa trey punguzo lipo kwa mawasiliano 0718221890
 
Pole sana mkuu fanya kuweka uzio itakusaidia sana kweli kinga ya Vifaranga vyako
 
Back
Top Bottom