Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Dawa ni hii

Wapake rangi ya Ukili au ile rangi inayopakwa kwenye Mikeka yaani wapake kiwiliwili chote, kuna rangi nyekundu,blue manjano au yeyote ile hii itamfanya kuku aonekane kiumbe cha Ajabu
 
Hugo no kipanga mkuu,mbaya sana Hugo kiumbe,akikosa vifaranga atahangaika na hao kuku wakubwa hata anyofoe bwawa tu.
Na hivi keshajua hapo kuna ulaji hachomoki ng'o, fugia bandani hata kwa muda skate tamaa kuja hapo.
 
Dawa ni hii

Wapake rangi ya Ukili au ile rangi inayopakwa kwenye Mikeka yaani wapake kiwiliwili chote, kuna rangi nyekundu,blue manjano au yeyote ile hii itamfanya kuku aonekane kiumbe cha Ajabu
Umenikumbusha mbali sana hii pic
 
1. Huu kwa juu ni wavu?
2. Wanakaa humu kwa muda gani baada ya kutotolewa?
3. Unaweza taa au chungu chenye moto ili wapate joto?
4. Chakula unawapa kiasi gani kwa siku let's say wapo 15 kwenye box?

Samahani kwa maswali mengi mkuu.
Nilikuwa sijaliona hili swali (Samahani)
Kwanza haya unayoyaona ni mabox ya pikipiki, huku tunanunu 5000 mpaka 10,000
na wakati mwingine huwa yanatupwa na wauzaji. (Uliza kwa watengenezaji au wauza pikipiki)

1.Hayo maboksi yanakuja na mifuniko, mimi nimekata sehemu ya juu ya mfuniko nikaziba
kwa waya wa Dirishani kama unavyoonekana.

2. Wengi huwaweka hadi pale wanapoweza kuruka na kutoka nje ya box, binafsi sina mudaa maalumu
Wakishatotoa wengine huwa naangalia box ambalo wamekomaa nawaondoa na kuwaweka wapya

3. Wakati wa joto siweki chohote, wakati huu wa baridi huwa nawawekea hiyo mitungi
ambayo nimeiweka kwenye picha huku tunanunua kwa 3000 mpaka 5000. Kunambinu nili
fundishwa ya kuufanya mkaa udumu muda mrefu bila kuzimika au kuisha, huwa njaza unga
unga au chenga za mkaa hapo juu, pia huwa naloweka jivu na kuliweka (Uliza kwa wauza kahawa
watakuelekeza vizuri zaidi)

4.Huwa nawakadiria tu, wakimaliza nawaongezea tena. Machicha ya nazi, pumba za mahindi
' Pumba za dagaa n.k isipokuwa siku 3 za mwanzo naweza kuwapa kile kilichochanganywa kwa
ajili ya vifaranga, maa nyingi nanunua kwenye maduka ya kilimo.
 
Asantee sana kwa majibu yako yaliyoshiba na kujitosheleza...kwa kweli umenipa elimu kubwa sana sana,Mungu akubariki mno...
 
Hao vipanga kuwazuia ni rahisi mno. Tengeneza fensi na uweke wavu wenye matundu madogo kama tunazoweka madirishani na juu pia uweke hizo wavu, umemaliza.
 
Ahsante kwa maelezo mazuri mkuu...
Mimi nina kamtaji ka 2.2m, je katatosha kuanza ufugaji wenye tija mkuu.
Pia naomba kujua ni kipi bora kati ya kufuga kuku wa kienyeji na wale matahira(wa kisasa)?
Note: nahita kufuga kwaajili ya biashara na sio kitoweo tu.
 
Uko wapi? Unafanya Nini? Nataka nijue mwingine yupo kwenye Nyumba za Kupanga anataka Kufuga Kuku
 
Nipo Dar mkuu....
Na nipo kwenye nyumba ya kupanga,
Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.
 
Tafuta sehem ujenge banda kubwa tu na lakutosha watazurura humo ndani kwa usalama
 
Kama Dar Hakuna Ulazima wa Kukaa nakushauri hii Shughuli itapendeza zaidi Mikoani na 2.2M ni Kiasi Kikubwa sana Kama haujaoa hauna Kazi yeyote unaweza ukaachana na Dar na Kwenda hata hapo Mkurunga Utafanikiwa.
Nashukuru kwa ushauri mkuu... Kwa sasa kuondoka Dar haitakuwa rshisi maana kuna sehemu bado fanya kazi japo kipato sio kikubwa sana lakini nashukuru kimeniwezesha kuweka akiba ya hicho kiasi mkuu... Pia nimeoa mkuu........!!
Pengine itapendeza ukiendelea kinipa mawazo mkuu hata ambayo ni tofauti na ufugaji maana naona option hii inanilazimu kuwa kijijini.
Nawasilisha mkuu
 

Jibu:
Chanjo zote zinazotakiwa kabla hujawachukua tunakuwa tumewapa.


1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…