Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kupitia maswali na majibu ya uzi huu nimejitengenezea Kijarida kidogo ambacho kitakuwa very useful especially kwenye changamoto za Ufugaji wa Kuku ...Ahsanteni sana Wadau kwa spirit hii ya Mafanikio ya Pamoja...Mungu aendelee kuwabariki kadri ya kujitoa kwenu..
 
Reactions: Qj_
Huyo anaitwa kipanga mkuu,tafuta nyavu umtegeee lazima anase.
 
Habari wanajamii forums,mimi nimgeni humu natokea Geita. Wanajamii naomba kufahamu changamoto katika, ufugaji wa kuku wa kienyeji,na je, ni ufugaji unaofaa kibiashara?Naombeni ushauri kidogo watanzania wenzangu.
 
Changamoto katika biashara yoyote ipo...
Kwa case yako ni magonjwa, Masoko, usimamizi wake n.k

Hiyo biashara ukiisimamia vizuri inalipa..Kila la heri mkuu
 
"Uandaaji wa chakula cha mifugo kwa njia ya hydroponics fodder",kuna mtu anaandaa hii kwa malisho ya kuku?kama yupo naomba atupatie uzoefu.
 
Naomba kufahamishwa kuhusu tabia hii ya kuku wa kienyeji
Nina kuku wangu wa kienyeji pure ametaga kafikisha mayai 10 na ndio mtago wake wa kwanza lakin ameanza tabia ambayo sijaielewa ikifika jion anaenda kwenye kiota chake cha mayai analalia ikifika asubui wakati nafungua banda anatoka na harud tena kulalia mpaka ikifika jion muda wa kuingia bandani na leo ni siku ya pili kafanya hivyo :
1.sasa nilitaka kujua ndio inavyokuwa kwa kuku anaeanza kulalia/kuatamia kufanya hivi kwa siku za kwanza au sio mlaliaji mzuri
2.je mayai yatakua salama kwa style hii aliyoifanya kulalia usiku tu kwa siku mbili
3.je nifanye nini kuyaokoa mayai yasiharibike kama itakua bado hayajaharibika?
 
kuku wa kienyeji ... da nilidhani kuku wa kienyeji ninayemjua mimi....
 
SIYO KAWAIDA MTENGE NAYO UYAKAGUE VINGINEVYO YATAHARIBIKA
 
Kuku wanatofautiana mkuu, ndomana kabla ya kutaka kufuga kuku unashauliwa kutafuta breed yenye sifa nzuri ya kuweza kulalia, hivo huyo wako hana sifa hiyo na ni vigumu kumbadili, labda endapo utaamua kutengenezea banda na kutoruhusu atoke nje na chakula uwe unampa wewe na sio kujitaftia

Issue ya mayai, ni kweli akiendelea hivo mayai yataharibika, sasa ili kuyanusuru inabidi uyapeleke kwenye mashine ya kutotoresha
 
anajiandaa kulalia huyo,toa mayai muachie matatu mpaka atakapochanganya kulalia,pia muandalie sehemu nyingine nzuri ya kulala,kuku hata asiyetaga anapenda kulala kwenye kiota kizuri
 
Kama humpi chakula unategemea nini mkuu? Lazima akatafute msosi ashibe kwanza
 

Unataka kuniambia hiz siku mbili alizolalia usiku tu mayai yatafaa kwenda kwenye incubator na vifaranga nikapata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…