Innocent Henry
Member
- Oct 10, 2017
- 62
- 10
Kama kuna uwezekano fanya kutuwekea link ili tuingiekwa wale wafugaji wa kuku nichekini hapa 0625923470 niwaunganishe na magroup ya wafugaji, huku utapata elimu nzuri kuhusu ufugaji, madawa, vyakula n.k
pia anayehitaji vifaranga, mayai ya kutotolesha na huduma ya incubator yaan KITOTOLESHI, huduma zote hizo zinapatiaka.
0625923470, karibuni
Wengine hatuna whatsap kiongozi...tafadhali tusaidie huku
Unawezaje kutambua mayai bora?
Kweli jamani msaada hilo swali ni muhimu pia kwangu, kuyatambua mayai bora
Hata mm nasubiria jibu pia
Asante sana mkuuMayai yawe na sifa zifuatazo:
1. Yasiwe ya mviringo. Chagua mayai yenye nca
2. Yasiwe makubwa sana, na yasiwe madogo sana. Yawe ya wastani.
3. Yasiwekwe/yasikae kwenye joto kabla ya kuanza kuatamiwa.
4. Weka mayai ambayo kuku anaweza kuyafunika yote. Yasitokeze nje. Yote yaenee kwa kuku.
5. Kwa matokeo mazuri chagua mayai ambayo hayajakaa zaidi ya siku saba tangu kutagwa.
6. Mayai yawe yametokana na kuku waliopandwa na jogoo. Kwa matokeo bora, jogoo mmoja ahudumie majike kati ya 7 na 10 tu.
7. Sehemu anayoatamia kuku isiwe inapitisha upepo/baridi. Kuku atengenezewe kiota kinachomkinga na upepo/baridi.
8. Kiota cha kuku kiwekwe maranda ya mbao, pumba za mpunga, majani makavu laini au mchanga laini ili kiweza kisaidia kutunza joto.
9. Ni vema ukanyunyiza dawa ya kuua wadudu ili kuzuia wadudu wasumbufu.
10. Kuku wasipate usumbufu kutoka kwa kuku wengine kama vile kugombania mayai au kudonolewa/kupigwa na kuku wengine.
Nimejaribu kutoa dondoo zaidi ya swali. Hizo siyo sifa za mayai bora tu bali pia na njia za kuwezesha kuku kutotoa vifaranga wengi. Nadhani itasaidia.
Inashauriwa 1 sq mita kwa kuku watano. Sasa kama una banda la 2 x4 hizo ni 8 sq mita. Uki-cross na ku-multiply hapo utakuwa na kuku 40 pekee. Ila kibongo bongo unaweza kulazimisha wakafikia hadi 50 Kiongozi.Hapa nyumbani nina banda la mita 2 × 4 na height ya mita 2. Je idadi ya kuku wanapaswa wasizidi wangap? N:B nimezungushia waya kwa mbele wenye ukubwa kama wa banda
katavi mkuu1.upo maeneo gani?
2.ingawa watakuja kukupa maelezo,lakini pia pitia nyuzi zilizopita utajifunza mengi.
Unataka kuanza na vifaranga wangapi? Cha msingi unatakiwa kuwa na banda bora, chakula cha vifaranga na kujua ratiba ya chanjoHabari wakuu, poleni na mvua za Dar
Natarajia kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji au chotara hivi karibuni lakini sina elimu ya kutosha katika hili
Ningependa mnisaidie ushauri juu ya vifaa bora vya kulishia kuku, maeneo wanapouza vyakula vya kuku au jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, wakati sahihi wa kuwalisha kuku, chanjo ya kuku, wakati sahihi wa kuwapa chanjo na mengineyo yanayohusiana na ufugaji wa kuku
Natanguliza shukrani.