Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

kwa wale wafugaji wa kuku nichekini hapa 0625923470 niwaunganishe na magroup ya wafugaji, huku utapata elimu nzuri kuhusu ufugaji, madawa, vyakula n.k
pia anayehitaji vifaranga, mayai ya kutotolesha na huduma ya incubator yaan KITOTOLESHI, huduma zote hizo zinapatiaka.
0625923470, karibuni
 
Wadau me naomba mnisaidie ushauri kidogo,nahitaji kuanza kufanya hii biashara,binafsi sitaki kuwaajiri vijana na niwalipe mshahara,ila nataka niwalipe based na mauzo,labda kwa percent fulan ya faida au kiwango fulani,naombeni mnishauri juu ya gharama kiasi gani zinahitajika kumtunza kuku mmoja wa kienyeji ukizingatia madawa na vyakula kwa ufugaji wa kisasa na nitegemee wastani wa faida kiasi gani kwa kuku.asanteni sana.
 
kwa wale wafugaji wa kuku nichekini hapa 0625923470 niwaunganishe na magroup ya wafugaji, huku utapata elimu nzuri kuhusu ufugaji, madawa, vyakula n.k
pia anayehitaji vifaranga, mayai ya kutotolesha na huduma ya incubator yaan KITOTOLESHI, huduma zote hizo zinapatiaka.
0625923470, karibuni
Kama kuna uwezekano fanya kutuwekea link ili tuingie
 
Unawezaje kutambua mayai bora?

Kweli jamani msaada hilo swali ni muhimu pia kwangu, kuyatambua mayai bora

Hata mm nasubiria jibu pia

Mayai yawe na sifa zifuatazo:
1. Yasiwe ya mviringo. Chagua mayai yenye nca
2. Yasiwe makubwa sana, na yasiwe madogo sana. Yawe ya wastani.
3. Yasiwekwe/yasikae kwenye joto kabla ya kuanza kuatamiwa.
4. Weka mayai ambayo kuku anaweza kuyafunika yote. Yasitokeze nje. Yote yaenee kwa kuku.
5. Kwa matokeo mazuri chagua mayai ambayo hayajakaa zaidi ya siku saba tangu kutagwa.
6. Mayai yawe yametokana na kuku waliopandwa na jogoo. Kwa matokeo bora, jogoo mmoja ahudumie majike kati ya 7 na 10 tu.
7. Sehemu anayoatamia kuku isiwe inapitisha upepo/baridi. Kuku atengenezewe kiota kinachomkinga na upepo/baridi.
8. Kiota cha kuku kiwekwe maranda ya mbao, pumba za mpunga, majani makavu laini au mchanga laini ili kiweza kisaidia kutunza joto.
9. Ni vema ukanyunyiza dawa ya kuua wadudu ili kuzuia wadudu wasumbufu.
10. Kuku wasipate usumbufu kutoka kwa kuku wengine kama vile kugombania mayai au kudonolewa/kupigwa na kuku wengine.

Nimejaribu kutoa dondoo zaidi ya swali. Hizo siyo sifa za mayai bora tu bali pia na njia za kuwezesha kuku kutotoa vifaranga wengi. Nadhani itasaidia.
 
Asante sana mkuu
 
Hapa nyumbani nina banda la mita 2 × 4 na height ya mita 2. Je idadi ya kuku wanapaswa wasizidi wangap? N:B nimezungushia waya kwa mbele wenye ukubwa kama wa banda
 
Inashauriwa 1 sq mita kwa kuku watano. Sasa kama una banda la 2 x4 hizo ni 8 sq mita. Uki-cross na ku-multiply hapo utakuwa na kuku 40 pekee. Ila kibongo bongo unaweza kulazimisha wakafikia hadi 50 Kiongozi.
 
Napoishi pana mahitaji makubwa ya kuku balaaa kuku mkubwa wa kienyeji ni 15,000-20,000 bila chenga kabisa ,sasa na-plan kufuga Kuku hao wa kienyeji naomba nipate muongozo je baada kutotolesha vifaranga hai naanzaje kuvilea chanjo,banda langu ni la upana wa futi 4 1/2 kwa 4 1/2
urefu ni futi 5 na lina ngazi mbili ndani ,na je watachukua muda gani kuwa na saizi ya kibiashara.
 
1.upo maeneo gani?
2.ingawa watakuja kukupa maelezo,lakini pia pitia nyuzi zilizopita utajifunza mengi.
 
Habari wakuu, poleni na mvua za Dar

Natarajia kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji au chotara hivi karibuni lakini sina elimu ya kutosha katika hili

Ningependa mnisaidie ushauri juu ya vifaa bora vya kulishia kuku, maeneo wanapouza vyakula vya kuku au jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, wakati sahihi wa kuwalisha kuku, chanjo ya kuku, wakati sahihi wa kuwapa chanjo na mengineyo yanayohusiana na ufugaji wa kuku

Natanguliza shukrani.
 
kuna thread ipo huku sikumbuki jukwaa gani ina maelezo mazuri ya ufugaji wa kuku wa kienyeji
 
Habari wakuu, poleni na mvua za Dar

Natarajia kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji au chotara hivi karibuni lakini sina elimu ya kutosha katika hili

Ningependa mnisaidie ushauri juu ya vifaa bora vya kulishia kuku, maeneo wanapouza vyakula vya kuku au jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, wakati sahihi wa kuwalisha kuku, chanjo ya kuku, wakati sahihi wa kuwapa chanjo na mengineyo yanayohusiana na ufugaji wa kuku

Natanguliza shukrani.
Unataka kuanza na vifaranga wangapi? Cha msingi unatakiwa kuwa na banda bora, chakula cha vifaranga na kujua ratiba ya chanjo
 
Nauza kuku wa kienyeji 15000 tetea .... Jogoo 20000 ....... Call 0714111058..
 
Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..

*_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
* _Popote ulip0 dar unaletewa..*_
 
Back
Top Bottom