Unawezaje kutambua mayai bora?
Kweli jamani msaada hilo swali ni muhimu pia kwangu, kuyatambua mayai bora
Hata mm nasubiria jibu pia
Mayai yawe na sifa zifuatazo:
1. Yasiwe ya mviringo. Chagua mayai yenye nca
2. Yasiwe makubwa sana, na yasiwe madogo sana. Yawe ya wastani.
3. Yasiwekwe/yasikae kwenye joto kabla ya kuanza kuatamiwa.
4. Weka mayai ambayo kuku anaweza kuyafunika yote. Yasitokeze nje. Yote yaenee kwa kuku.
5. Kwa matokeo mazuri chagua mayai ambayo hayajakaa zaidi ya siku saba tangu kutagwa.
6. Mayai yawe yametokana na kuku waliopandwa na jogoo. Kwa matokeo bora, jogoo mmoja ahudumie majike kati ya 7 na 10 tu.
7. Sehemu anayoatamia kuku isiwe inapitisha upepo/baridi. Kuku atengenezewe kiota kinachomkinga na upepo/baridi.
8. Kiota cha kuku kiwekwe maranda ya mbao, pumba za mpunga, majani makavu laini au mchanga laini ili kiweza kisaidia kutunza joto.
9. Ni vema ukanyunyiza dawa ya kuua wadudu ili kuzuia wadudu wasumbufu.
10. Kuku wasipate usumbufu kutoka kwa kuku wengine kama vile kugombania mayai au kudonolewa/kupigwa na kuku wengine.
Nimejaribu kutoa dondoo zaidi ya swali. Hizo siyo sifa za mayai bora tu bali pia na njia za kuwezesha kuku kutotoa vifaranga wengi. Nadhani itasaidia.