Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Next time summarize your post. Its too long especially for mobile users.


Find a PC and do your stuff...............mobile connection is meant to expedite things and not a total solution for everything you want to communicate!
 

mkuu saafi sana
 
mkuu Gazeti unafugia wapi hao kuku.
nimependa approach yako ya kulima mazao fulani fulani kwanza

Nilikuwa nafuga, kwa kuwa nilikuwa nimesomea uhasibu nikashawishika
kuajiriwa hapo ndipo nilipoharibu. Najipanga kurudi tena na nimeshaanza maandalizi
kwani nimepata shamba maeneo ya JARIBU MPAKANI. Nauli ni Tsh 3000 kutoka
Mbagala.
 
Ni kweli mkuu ufugaji wa kuku unalipa cha kuzingatia ni taratibu za ufugaji bora pia kuwa karibu na wazoefu ili wakupe mbinu za kukabiliana na changamoto za ufugaji pindi zitakapojitokeza
 
Ni uhifadhi tu, Inategemea utakavyo yahifadhi nitakupa melekezo yoote we karibu tu usiwe na shaka
mi nadhani ntakuwa mteja wako soon lakin naskia mayai ya kienyeji yanaharibika mapema, hayakai muda mrefu kama ya kuku hawa wa kisiasa,ni kweli?
 

nipo TABORA MANISPAA.nahitaji moderm ya 25000 nitaipataje?
 
Tengeneza tangazo nikupe offer ya kutangaza kwenye my blog,ni pm kijana,angalia hapa kama panakufaa
GSHAYO
 

nimependa sana mpango wako wakijasiriamali unanikumbusha siku za nyuma. Baba yangu alikuwa akifuga kuku zaidi ya 2000 tabora mjini miaka ya 1977-1995. Nimezaliwa nimekuta akiifanya tena nikilinganisha na sasa wafugaji wengi hawajafikia kiwango chake. Kwani nakumbuka tulikuwa na mashine zakukatia midomo. Maji kulikuwa na pipe zimezunguka kwenye banda kwa juu nazo zilikuwa na vitundu ambapo mipira migumu myembamba ilitiririsha maji mpaka kwenye chombo cha kunywea kuku. Nimejaribu kutembelea wafugaji wengi hapa dar sijaona hatu aliyo fikia mzee wangu lakini kilakitu na wakati alikuja pata matatizo ya kufungwa kilakitu kiliharibika nami nilikuwa mdogo. Hata kulikuwa na ng'ombe wamaziwa zaidi ya 20 wote waliteketea. Kwa sasa mi sifanyi ila natamani kufanya najiweka sawa tu. Ama niwekeze dar na njombe lakini nikiwa nauzoefu wa mzee wangu pale tabora mjini chemchem na nga'mbo. Al maarufu mze hassan.....,..,.
 

kwa ufugaji aliokuwa akiufanya kwasasa utaweza kusema ni wakisasa. More info email me sanekomb@yahoo.com Pia waweza call me 0713665909
 
HONGERA SANA.Nashawishika, ndo kwaaaaaanza nimemaliza chuo.Ni ajira tosha, nikichanganya na hiki KILIMO cha msimu hapa kijijini-maisha yataenda.Kwa sasa kikwazo kwangu ni rasilimali(fedha), mifumo ya taasisi zetu za fedha ni migumu kidogo.But NAWASHUKURU coz ushauri wenu na mawazo vimeninipa mwanga wanaJF.
 
Wadau,

Mimi sijawahi kufanya biashara ya kuku wa kienyeji, ila nina ndugu yangu ambaye amekua akifuga kuku wa kienyeji kwa muda sasa na anatarajia kuanza kuwauza kwa ujumla (rejareja watakuwepo lakini sio lengo kuu).

Kuku wapo wengi (around 2,000+), ni wakienyeji asili (sio wale hybrid).

Naomba kwa wale ambao mnafahamu kwa undani biashara wa kuku wa kienyeji mnidokeze mawili matatu kuhusu soko.

Vitu ambavyo ningependa kujua ni kama ifuatavyo:

- Wateja wakuu wa kuku wa kienyeji
- Bei ya mtetea/jogoo saizi ya kati na majogoo makubwa. (kwa sasa sifahamu uzito halisi)
- Kuku wa ukubwa gani wenye uhitaji mkubwa zaidi (mtetea/jogoo kimo cha kati au majogoo makubwa)

Soko tunalotazamia ni soko la ujumla, i.e. kuanzia order ya kuku 20 na kuendelea.

Kwa sasa soko nalofahamu ni baa na restaurants ambazo wanatengeneza supu ya kuku wa kienyeji.

Pia, kama kuna thread ilishawahi kulizungumzia hili, ntashukuru ukipost link hapa.

Natanguliza shukrani.
 
Habari mkuu soko lipo kubwa tu wala usipate shaka,sina details kamili za wanunuzi ila tembelea migahawa mikubwa kama BREAKPOINT,ROSE GARDEN,ROUND ABOUT YA KWENDA BANDARINI na kwingineko pia hawa jamaa wenye bucha hapa ubungo shell huwa wanauza kuku wa kienyeji jaribu kuwaona kama watahitaji kununua,otherwise ni wale wachuuzi wa kwenye masoko kama pale shekilango,kimara,mbezi,afrika sana wanaweza pia nunua ila kwa bei ya chini ili na wo wapate riziki.Vp upande wa mayai ya hao kuku yanapatikana?
 
Thanks mkuu,

Ntakupa jibu kamili next time kuhusu mayai. Ila nayo yapo kwa wingi tu.
 
Hao kuku wako wapi?
Tuangalie namna ya kufanya biashara (if possible tuchukue kuku wote hadi vifaranga!)
Kwa bei ya jumla kuku wote ni sh. ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…