Kwenye kuatamisha kila kuku nilimpa aatamie mayai 15 baada ya kutotoa nilikuwa kila kuku mmoja ninamkabidhi vifaranga 30!
Asante YATIMA, kwa hivi sasa napokea michango na maswali kwa mada ya leo huku nikiendelea kuandaa topic zijazo! Maswali yako matamu hadi nafuta machozi kwa kucheka! Mkuu usichezee kitu inaitwa Hobby!! Hapa ndiyo namkubali mkuu CHASHA pale anaposema unaweza kufanikiwa sana ukibadili HOBBY yako kuwa business idea! Yaani nikitoka kwenye tanuri zangu za mkaa nikifika tu home roho inanituma nitue bandani, nikiingia humo natoka nimebebelea mayai yaani ni rahaa kishenzi!! Usiku huingia bandani ninapokuwa ninawawekea mayai kuku wanaoatamia siku hiyo ndiyo huchora mayai ni maramoja kwa mwezi! Tochi mayai hupigwa mara moja tu kwa mwezi siku 10 baada ya kuatamia! Hakuna raha kama kukusanya vifaranga na kuwahamisha, nayo hutokea mara moja kwa mwezi. In fact kama ni ubize ni kule kwenda kuokoto mayai na kuwafunua kuku walioatamia, kucheki kama kuna yai jipya. Sometimes huwa naona kama nafanya faulo maana kwa kweli huwa nawafunua funua kila siku kuchungulia kama kumchungulia mtu mzima baada ya kumfunua. Kuku wengine ni wapole kweli unamfunua kakuacha tu, wengine wakali kweli kweli ukisogeza mkono tu keshakudonoa! Burudani yote hii kwanini nisikae bandani!! Sorry for this!very interesting ............ lakini inaonyesha muda mwingi unakuwa bandani??? Yaani kuangalia mayai, kuchora, kumulika na tochi ............ kuhamisha vifaranga ............... kufunga kuku (wafungwa) jela............. etc.
Hebu TAFADHALI tuelimishe .. ulikuwa unakaa bandani muda gani??? Ulikuwa unapata muda wa kutoka kidogo au????
otherwise HONGERA SANA.
Mkuu huwa naona kuku ukimpa vifaranga ambao sio wake anawapiga. Umefanikiwaje katika hili?
mkuu hongera sana..umefanya kazi hii kwa kujitoa na kila siku umekuwa mbunifu wa kazi yako.na ni kweli ukifanya kitu kwa hobby uwa unajitoa kweli na unaenjoy hata ukikutana na changamoto haukati tamaa.pia haukukatishwa tamaa na mazingira yako bado umeweza kuyatumia mazingira uliyopo kwa ufanisi.pia unaweza kumfanya kuku asiatamie kwa kumzamisha kwenye maji na kuacha shingo tu juu kwa dk chache.nimeshawahi kusikia ukiweka ufuta kuzunguka mayai yanayoatamiwa kuku uwa haondoki ataatamia hadi amalize kutotoa sijawahi kujaribu hii mbinu.hongera sana mkuu
Wana JF natumaini hamjambo, ni siku nyingine naomba niendelee na simulizi ya mihangaiko yangu ya ufugaji wa Kuku wa Kienyeji!
Naomba nisisitize kutokana na nilichoshuhudia ni kuwa wafugaji wengi huishia kubaki na idadi ndogo ya kuku, hii hasa kutokana na utotoaji duni au vifo vingi sana vya vifaranga. Mbinu ya kuwatenganisha vifaranga na mama zao na kuwakuza peke yao ikifanywa kwa uangalifu hupanua kundi la kuku kwa haraka sana. Kuna utenganishaji ambao hufanyika mara tu vifaranga wanapototolewa aina hii huwezesha kuku kuwa na awamu nyingi za utagaji na uatamiaji kufikia hadi awamu 6 kwa mwaka. Kwa wale wenye mashine za kutotolesha vifaranga ambako kuku hawaachwi kuatamia kabisa, kuku hao huweza kutaga mayai mengi zaidi kwa mwaka kulingana na uwezo wa aina ya kuku.
Mimi sikuwa na mashine ya kutotolesha na wala sikuweza kuwatenganisha vifaranga mara baada ya kutotolewa kwa kuwa sikuwa na miundo mbinu yenye kuwezesha kufanya hivyo. Niliwategemea kuku hao hao kuatamia na kukuza vifaranga. Isipokuwa sasa tofauti na kawaida, mimi nilipunguza idadi ya kuku wa kuatamia kwa kuwapa mayai mengi kuku wachache wayaatamie ili wengine badala ya kuatamia mayai machache wakaendelee kutaga, pia baada ya hawa kuku wachache kutotolesha, vifaranga vyao nilivikabidhi kwa kuku wachache zaidi kama nilivyosimulia jana, ili na hawa nao warudi kundini kutaga! Kuwa na kuku wengi wanaotaga kulisaidia kupata lishe na kuuza mayai ambapo nilikuwa napata pesa ya kununulia chakula na dawa za kulea vifaranga na kuku wote.
Baada ya kumudu kuweza kutotolesha vifaranga kwa wingi liliibuka tatizo la vifo vya vifaranga kiasi ambacho kilianza kunikatisha tamaa kabisa! Ilinichukua muda sana nikijiuliza kwa nini? Hadi kufikia napata ufumbuzi nilikuwa nimeshatupa vifaranga wengi sana, nitalielezea hili vizuri wakati wake ukifika hapo baadae.