Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Atakuja jamani tumsubirie!!
Kanipm kuwa wanajukwaa mnampa sana presha, naombeni mtulie ili apakue mzigo wote vizuri, otherwise ataharibu coz atalazimika kupakua under pressure na mwishowe kuku wanaweza kufa!!

Tahadhari:
kubota ukipakua mzigo vibaya ujue utazamisha jahazi la wengi kwa hio stay calm na upakue kitu cha maana, hivyo hivyo kwa wanajamvi mkimshinikiza sana kupakua kabla haujaiva vizuri mjiandae kwa side effect yake!!
So kizuri hakitaki papara!!
Poleni anyway naona mmedhamiria kuua shetani umaskini kwa damu, machozi na jasho, nawatakia kila la kheri katika hili!!
 
Mkuu Kubota inabidi ushushe nondo za kutosha wadau wana kiu sana na diyo maana ukichelewesha unawaudhi.

.......................................
Historia haiishiwi wino.
 
sawa tumeelewa tutakusubiri kiongozi
 
very interesting ............ lakini inaonyesha muda mwingi unakuwa bandani??? Yaani kuangalia mayai, kuchora, kumulika na tochi ............ kuhamisha vifaranga ............... kufunga kuku (wafungwa) jela............. etc.

Hebu TAFADHALI tuelimishe .. ulikuwa unakaa bandani muda gani??? Ulikuwa unapata muda wa kutoka kidogo au????

otherwise HONGERA SANA.
 
Halafu Mods tunaomba msaada, thread haionekani kwenye jukwaa husika imejificha!

.......................................
Historia haiishiwi wino.
 
very interesting ............ lakini inaonyesha muda mwingi unakuwa bandani??? Yaani kuangalia mayai, kuchora, kumulika na tochi ............ kuhamisha vifaranga ............... kufunga kuku (wafungwa) jela............. etc.

Hebu TAFADHALI tuelimishe .. ulikuwa unakaa bandani muda gani??? Ulikuwa unapata muda wa kutoka kidogo au????

otherwise HONGERA SANA.
Asante YATIMA, kwa hivi sasa napokea michango na maswali kwa mada ya leo huku nikiendelea kuandaa topic zijazo! Maswali yako matamu hadi nafuta machozi kwa kucheka! Mkuu usichezee kitu inaitwa Hobby!! Hapa ndiyo namkubali mkuu CHASHA pale anaposema unaweza kufanikiwa sana ukibadili HOBBY yako kuwa business idea! Yaani nikitoka kwenye tanuri zangu za mkaa nikifika tu home roho inanituma nitue bandani, nikiingia humo natoka nimebebelea mayai yaani ni rahaa kishenzi!! Usiku huingia bandani ninapokuwa ninawawekea mayai kuku wanaoatamia siku hiyo ndiyo huchora mayai ni maramoja kwa mwezi! Tochi mayai hupigwa mara moja tu kwa mwezi siku 10 baada ya kuatamia! Hakuna raha kama kukusanya vifaranga na kuwahamisha, nayo hutokea mara moja kwa mwezi. In fact kama ni ubize ni kule kwenda kuokoto mayai na kuwafunua kuku walioatamia, kucheki kama kuna yai jipya. Sometimes huwa naona kama nafanya faulo maana kwa kweli huwa nawafunua funua kila siku kuchungulia kama kumchungulia mtu mzima baada ya kumfunua. Kuku wengine ni wapole kweli unamfunua kakuacha tu, wengine wakali kweli kweli ukisogeza mkono tu keshakudonoa! Burudani yote hii kwanini nisikae bandani!! Sorry for this!
 
Mkuu huwa naona kuku ukimpa vifaranga ambao sio wake anawapiga. Umefanikiwaje katika hili?

Mkuu hakuna ukatili wa kuku niliowahi kuumizwa roho kama hicho ulichosema! Kuna kuku ni wakatili kweli kweli! Kuku hawa utawatambua na hutakiwi kuwapa nafasi kulea vifaranga! Hao waishie kutaga tu! Pamoja na hayo zoezi la kumpa kuku vifaranga visivyokuwa vyake lifanyike usiku au kwa namna ambayo asishuhudie unapowaingiza vifaranga wasio wake! Lakini hata hivyo kuna kuku wakorofi na ni makini sana utakuta anawatambua wasiowake na anawadonoa hadi anaua! Ni budi kuwatambua na kuwaepuka kuku wakali na pia kuwahi kuwawekea vifaraga mapema kabla hawajaweza kutofautisha vifaranga wake na wasio wake!
 
mkuu hongera sana..umefanya kazi hii kwa kujitoa na kila siku umekuwa mbunifu wa kazi yako.na ni kweli ukifanya kitu kwa hobby uwa unajitoa kweli na unaenjoy hata ukikutana na changamoto haukati tamaa.pia haukukatishwa tamaa na mazingira yako bado umeweza kuyatumia mazingira uliyopo kwa ufanisi.pia unaweza kumfanya kuku asiatamie kwa kumzamisha kwenye maji na kuacha shingo tu juu kwa dk chache.nimeshawahi kusikia ukiweka ufuta kuzunguka mayai yanayoatamiwa kuku uwa haondoki ataatamia hadi amalize kutotoa sijawahi kujaribu hii mbinu.hongera sana mkuu
 
Wana JF natumaini hamjambo, ni siku nyingine naomba niendelee na simulizi ya mihangaiko yangu ya ufugaji wa Kuku wa Kienyeji!

Naomba nisisitize kutokana na nilichoshuhudia ni kuwa wafugaji wengi huishia kubaki na idadi ndogo ya kuku, hii hasa kutokana na utotoaji duni au vifo vingi sana vya vifaranga. Mbinu ya kuwatenganisha vifaranga na mama zao na kuwakuza peke yao ikifanywa kwa uangalifu hupanua kundi la kuku kwa haraka sana. Kuna utenganishaji ambao hufanyika mara tu vifaranga wanapototolewa aina hii huwezesha kuku kuwa na awamu nyingi za utagaji na uatamiaji kufikia hadi awamu 6 kwa mwaka. Kwa wale wenye mashine za kutotolesha vifaranga ambako kuku hawaachwi kuatamia kabisa, kuku hao huweza kutaga mayai mengi zaidi kwa mwaka kulingana na uwezo wa aina ya kuku.

Mimi sikuwa na mashine ya kutotolesha na wala sikuweza kuwatenganisha vifaranga mara baada ya kutotolewa kwa kuwa sikuwa na miundo mbinu yenye kuwezesha kufanya hivyo. Niliwategemea kuku hao hao kuatamia na kukuza vifaranga. Isipokuwa sasa tofauti na kawaida, mimi nilipunguza idadi ya kuku wa kuatamia kwa kuwapa mayai mengi kuku wachache wayaatamie ili wengine badala ya kuatamia mayai machache wakaendelee kutaga, pia baada ya hawa kuku wachache kutotolesha, vifaranga vyao nilivikabidhi kwa kuku wachache zaidi kama nilivyosimulia jana, ili na hawa nao warudi kundini kutaga! Kuwa na kuku wengi wanaotaga kulisaidia kupata lishe na kuuza mayai ambapo nilikuwa napata pesa ya kununulia chakula na dawa za kulea vifaranga na kuku wote.

Baada ya kumudu kuweza kutotolesha vifaranga kwa wingi liliibuka tatizo la vifo vya vifaranga kiasi ambacho kilianza kunikatisha tamaa kabisa! Ilinichukua muda sana nikijiuliza kwa nini? Hadi kufikia napata ufumbuzi nilikuwa nimeshatupa vifaranga wengi sana, nitalielezea hili vizuri wakati wake ukifika hapo baadae.
 
Masimulizi yangu jana niliwagusia kuwa nilikuwa nina banda kubwa lenye chumba na sebule, pia nilikuwa nina JELA ambapo mwanzoni nilitumia matenga au mabox! Baada ya kuanza kutotolesha vifaranga, ilibidi nijenge kibanda cha kukuzia vifaranga (Nursery)! Kilikuwa kibanda kidogo kidogo tu mfano wa kigorofa hivi nitaelezea siku nyingine nilivyokitengeneza na mchoro wake mtauona. Picha ya Kuku niliewaonyesha huko nyuma yumo ndani ya moja ya vyumba sita ambapo vyumba vitatu viko chini na vitatu viko ghorofani. Vyumba hivyo vilikuwa vya kukuzia vifaranga.

Mara baada ya kutotolewa kwenye banda kubwa vifaranga na mama zao niliwahamishia kwenye hii nursery. Kila chumba niliweka chakula na maji ya kutosha siku nzima kila siku asubuhi. Kuku walikuzwa humo kwa muda wa mwezi mmoja ambapo baada ya vifaranga kuota manyoya mwili mzima ndipo mama zao niliwatoa. Kisha hawa vifaranga wakubwa ambao nitakuwa nawaita VINYOYA niliwasambaza wote kwenye vyumba vingine vitano na nilibakisha chumba kimoja tu ambacho ndiyo hicho nilikitumia kama JELA! Nilishawaelezea tayari juu ya matumizi ya hii Jela.

Hao VINYOYA baada ya kuwatengenisha na mama zao niliwaacha wiki moja kisha nao nikawa nawafungulia waanze kuokoteza chakula na kuchunga. Wakati huu kwenye banda kubwa kulikuwa na kuku wanaoatamia ambao niliwawekea mayai siku 10 baada ya kutotolewa hawa VINYOYA! Kwa hiyo kwa kujua kuwa kuna vifaranga ambao wangetumia hii nursery hapo baadae, ilibidi nijenge banda lingine kwa ajili ya kuwakuzia hawa Vinyoya. Baada ya kuwahamishia hawa vinyoya kwenye banda lao nilikuwa ninawaaacha hadi miezi miwili au zaidi kabla ya kuwahamishia kwenye banda kubwa.

Hadi kufikia hapo mzunguko wangu wa mabanda ya kuku ukawa umekamilika! Yaani nilikuwa na banda kubwa sebuleni kwa ajili ya kulala na kutaga kuku wakubwa, chumbani kwa ajili ya kuatamia na kutotoleshea, banda la kukuzia vifaranga (nursery) na banda la kukuzia vinyoya. Vipimo na michoro na vifaa nilivyotumia kujenga miundombinu hii itakuja peke yake na siku yake itawadia.

Wana JF kuna mtoto hapa nilipo kaja kuniambia kwamba huko kijiweni kwangu (porini) kimenuka, tanuru langu la mkaa limeachia mwee, ngojeni nikimbie nikalizibe nitarudi baadae mwenye maswali atupie, nikirudi nitakuja yajibu au mwenye mchango tushirikishane! ITAENDELEA……!
 
mkuu hongera sana..umefanya kazi hii kwa kujitoa na kila siku umekuwa mbunifu wa kazi yako.na ni kweli ukifanya kitu kwa hobby uwa unajitoa kweli na unaenjoy hata ukikutana na changamoto haukati tamaa.pia haukukatishwa tamaa na mazingira yako bado umeweza kuyatumia mazingira uliyopo kwa ufanisi.pia unaweza kumfanya kuku asiatamie kwa kumzamisha kwenye maji na kuacha shingo tu juu kwa dk chache.nimeshawahi kusikia ukiweka ufuta kuzunguka mayai yanayoatamiwa kuku uwa haondoki ataatamia hadi amalize kutotoa sijawahi kujaribu hii mbinu.hongera sana mkuu

Yes Dafo hii mbinu ya kumzamisha kuku kwenye maji huwa ninaisikia ikitajwa mara nyingi, kama inaufanisi ni njia nzuri zaidi, maana dosari ya JELA ikitokea umepitiwa ukasahau kuwafungulia kuku muda muafaka inakuwa ni kizaa zaa!

Wana JF natumaini hamjambo, ni siku nyingine naomba niendelee na simulizi ya mihangaiko yangu ya ufugaji wa Kuku wa Kienyeji!

Naomba nisisitize kutokana na nilichoshuhudia ni kuwa wafugaji wengi huishia kubaki na idadi ndogo ya kuku, hii hasa kutokana na utotoaji duni au vifo vingi sana vya vifaranga. Mbinu ya kuwatenganisha vifaranga na mama zao na kuwakuza peke yao ikifanywa kwa uangalifu hupanua kundi la kuku kwa haraka sana. Kuna utenganishaji ambao hufanyika mara tu vifaranga wanapototolewa aina hii huwezesha kuku kuwa na awamu nyingi za utagaji na uatamiaji kufikia hadi awamu 6 kwa mwaka. Kwa wale wenye mashine za kutotolesha vifaranga ambako kuku hawaachwi kuatamia kabisa, kuku hao huweza kutaga mayai mengi zaidi kwa mwaka kulingana na uwezo wa aina ya kuku.

Mimi sikuwa na mashine ya kutotolesha na wala sikuweza kuwatenganisha vifaranga mara baada ya kutotolewa kwa kuwa sikuwa na miundo mbinu yenye kuwezesha kufanya hivyo. Niliwategemea kuku hao hao kuatamia na kukuza vifaranga. Isipokuwa sasa tofauti na kawaida, mimi nilipunguza idadi ya kuku wa kuatamia kwa kuwapa mayai mengi kuku wachache wayaatamie ili wengine badala ya kuatamia mayai machache wakaendelee kutaga, pia baada ya hawa kuku wachache kutotolesha, vifaranga vyao nilivikabidhi kwa kuku wachache zaidi kama nilivyosimulia jana, ili na hawa nao warudi kundini kutaga! Kuwa na kuku wengi wanaotaga kulisaidia kupata lishe na kuuza mayai ambapo nilikuwa napata pesa ya kununulia chakula na dawa za kulea vifaranga na kuku wote.

Baada ya kumudu kuweza kutotolesha vifaranga kwa wingi liliibuka tatizo la vifo vya vifaranga kiasi ambacho kilianza kunikatisha tamaa kabisa! Ilinichukua muda sana nikijiuliza kwa nini? Hadi kufikia napata ufumbuzi nilikuwa nimeshatupa vifaranga wengi sana, nitalielezea hili vizuri wakati wake ukifika hapo baadae.

Usipapite hapo kwenye red na hata kwenye vyakula lengwa kamanda wetu Kubota; na ni vema ukatupatia kwa vipimo unavyowapa na ukizingatia hawa kuku wapo ndani ya fenzi!
 
Last edited by a moderator:
Kubota, asante sana kwa mafunzoo mazuri, inavutia na kutia moyo, ila naona inataka ujasiri kuku ni wakali wengine pia kuwafungia jela unaweza kuwaonea huruma....Ndo nimeanza na mimi nitajaribu hii mbinua yako nione kama itafaa wakifikia kutaga
 
Back
Top Bottom