Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kaka asante sana kwa elimu nzuri natumaini utakua umetusaidia wadau wengi tu wenye ndoto kama zako.....hamna kitu kizuri kama kufanya ujasiriamali kwa kujifunza kutokea kwa waliokutangulia.
 

Umesema kweli kabisa kwamba kumudu kujitengenezea chakula hasa hiki cha vifaranga ni ukombozi mkubwa! Wajuzi wanasema katika gharama za uzalishaji wa kuku 70% ni chakula! Niliweka ingredients zote muhimu! Mimi nimeafikiana na ushauri wako tuendelee kufanya ubunifu na utundu hadi tuweze! Na kama kuna alieweza atatuongoza! Kwa maneno yako Mama Joe nitarudi tena kambini kwa nguvu zaidi nijaribu tena kutengeneza na kuchanganya kichinachina!
 

Asante sana Mkuu Dafo yaani ulivyoandika ni kama nilikushikia kalamu, na mimi nawaza hivyo hivyo, siongezi wala kupunguza hata nukta! Ukiona hivyo ujue hapa kunatatizo! Sasa tutaepukaje hiyo 45,000 kwa mfuko wa chakula cha vifaranga? Hiyo ni changamoto!
 
Ushauri mzuri sana.mdogo mdogo ndio mwendo.Tutafika tu.Kubota endelea basi kutupa shule.
 

Asante mkuu kwa maelezo yako...ningependa kama ungeweza kutwekea hiyo manul ingekuwa vizuri sana.na pia kwenye damu kwa sasa naona baadhi ya wataalaamu wanashauri damu isitumike baada ya kutokuwa na uamnifu kwa wauzaji kutoka machinjioni wamekuwa wakiweka kinyesi ili kuongeza uzito.ambayo ni inaweza pelekea maambukizi kwa kuku.
 
Jamani shule nzuri sana asanteni wadau wote kwa micahngo mizuri sana, ngoja niwahi kuku wangu.
Hizo doc Chasha anazosema nawawekea hapa,
weekend njema

Mhh! Wakuu Mama Joe na Chasha huu ukarimu wa kudumbukiza hizi documents hapa you make me crazy!! Mungu awabariki kwa ukarimu huu ambao mitaani ni adimu isipokuwa JF pekee!
 
Mhh! Wakuu Mama Joe na Chasha huu ukarimu wa kudumbukiza hizi documents hapa you make me crazy!! Mungu awabariki kwa ukarimu huu ambao mitaani ni adimu isipokuwa JF pekee!


Hata mimi nawashukuru sana wakuu hawa. JF home of hospitality.

.......................................
Historia haiishiwi wino.
 
Chasha; Hebu tuwekee mawasiliano ya hawa jamaa hapa tafadhali!


 
Last edited by a moderator:
Chasha; Hebu tuwekee mawasiliano ya hawa jamaa hapa tafadhali!

Wapi hao wa RLDC au jamaa wa Mashine ya Kuchanganya chakula Cha kuku? Hawa wa RLDC wako Dom na wanaproject za kuku huko Singida, zinazo fadhiliwa na wathungu,
Ila wa Mashine ya Chakula cha kuku yuko A town, nita wekana namba yake baada ya kuwasiliana naye, make si kila mtu anapenda namba yake kuwa open si unajua, ila kwa PM utapata
 
Kubota; Mama Joe;

Msisite kutujuza hata kwa vifaranga wenye kutotolewa na mpaka miezi miwili dawa stahiki ni ipi?

Na hata dawa nzuri kwa hawa kuku wakubwa hasa kuhusu dawa ya minyoo kuku kuhara njano na hata nyeupe ni nini haswa chanzo ya hilo? Kubota; pitia kipande hii!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kubota nakusubiri kwa hamu kwenye magonjwa, kwakweli shule hii ni kiboko. Nimiekuwa nikifuga kwa sasa ni miezi mitatu. Tatizo ni vifaranga nimekuwa nikiwalisha starter toka kutotolewa mpaka week ya tano. niliwachanja chanjo ya jicho. wakakua vizuri mpaka wakaanza kuota manyoya. week ya tano nikaanza kuwatoa nje, mara nikaona kama watatu hivi ghafla wakaanza kuvaa makoti. kwanini wakati nimewachanja na wataalamu waliniambia nikiwachanja chanjo ya jicho hawatapata huo ugonjwa. nimechanganyikiwa maana nategemea kupata vifaranga wasiopungua arobaini maana kuna kuku wanne wanaatamia mayai 15 kila mmoja.
 
Last edited by a moderator:
guta;
Hapo kwenye red nakwambia mwaka jana niliwapoteza vifaranga kama 120 hivi na hapo Mi nasema wamevaa SUTI! Kha ha ha ha ha ha ha ha haaaaa!



Kubota; Usitusahau hata kwa post hii!

Hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…