Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hii habari ya chakula inabidi kuifanyia kazi hii hebu Kubota atwambie kama aliweka kila kitu kinachohitajika na kwa uwiano halisi? mimi naona tukikwamuka hapa kwenye chakula itakuwa mteremko sana maana mfuko wa chakula unafika hadi 45000 kipindi sasa vifaranga vikiwa vingi itakuwaje?
Mama Joe kwenye chakula na hicho kipindi cha mwezi mmoja wa kwanza kweli kuna changamoto.na nahisi tatizo sio kuweka kila kitu na kwa ratio inatakiwa.Inawezekana matatizo yakawa mawili makubwa.mosi, ni size ya punje za mahindi, dagaa na pumba.katika hali ya uchanganyaji wa mikono ni ngumu hivi vitu kusagika na kuwa katika punje ndogondogo kwa kifaranga wa siku moja hadi wiki tatu kuweza kula.mara nyingi inatokea punje za mahindi ni kubwa hata kama zimeparazwa.Tatizo la pili nahisi ni uchanganyaji wenyewe mana kwa kuchanganya na mikono ili vichanganyio vyote vichanganyike vizuri nayo sio rahisi sana hata kwa kuchanganya kilo 50 tu.Kwa mtazamo wangu nahisi hivyo ndo vinavyochangia.Asante.
Ushauri mzuri sana.mdogo mdogo ndio mwendo.Tutafika tu.Kubota endelea basi kutupa shule.Katika Utengenezaji wa Chakula cha Kuku, Kwenye vifaranga wa One day old, huwa inashauriwa kutumia Unga wa Dona ambao tiyali umesgwa ndo utumike badala ya Pumba,au mahindi, so kwenye kuchanganya unashauriwa kutumia unga wa Dona, Ila hakikisha mahindi hayana Dawa make unaweza ua vifaranga,
Ukiachiulia mabali formula ya ratio ya kila kimoja, kwenye ku changanya napo kuna Formula ya Kuchanganya si kuchanganya tu ilimuradi unachanganya, Kuna makundi unatakiwa kugawa vyakula katika makundi kama mawili hivi na kila kundi lina changanywa kivyake na mwisho unacompail pamoja hayo makundi mawili
Mkuu kuna Ile Manula ya RLDC kama sijakosea speling, wana manual nzuri sana ya jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, niliipenda sana Manual yao, na kuna moja wa Kenya nao walikuwa na ya maelezo ya kila chakula na altenative yake, ukisoa Damu utumie nini, ukikosa hiki utumie nini,
Jamani shule nzuri sana asanteni wadau wote kwa micahngo mizuri sana, ngoja niwahi kuku wangu.
Hizo doc Chasha anazosema nawawekea hapa,
weekend njema
Mhh! Wakuu Mama Joe na Chasha huu ukarimu wa kudumbukiza hizi documents hapa you make me crazy!! Mungu awabariki kwa ukarimu huu ambao mitaani ni adimu isipokuwa JF pekee!
Mkuu Somoche uko hadi huku?Mimi pia nafuga ajabu wale kuku wangu mimi sijisikii kuwala kabisa sijui kwanini na mke wangu ndio kabisaa hali kuku tunafuga anasema roho inamuuma!!
Mkuu kuna Ile Manula ya RLDC kama sijakosea speling, wana manual nzuri sana ya jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, niliipenda sana Manual yao, na kuna moja wa Kenya nao walikuwa na ya maelezo ya kila chakula na altenative yake, ukisoa Damu utumie nini, ukikosa hiki utumie nini,
Chasha; Hebu tuwekee mawasiliano ya hawa jamaa hapa tafadhali!
Mimi pia nafuga ajabu wale kuku wangu mimi sijisikii kuwala kabisa sijui kwanini na mke wangu ndio kabisaa hali kuku tunafuga anasema roho inamuuma!!
Mkuu Kubota nakusubiri kwa hamu kwenye magonjwa, kwakweli shule hii ni kiboko. Nimiekuwa nikifuga kwa sasa ni miezi mitatu. Tatizo ni vifaranga nimekuwa nikiwalisha starter toka kutotolewa mpaka week ya tano. niliwachanja chanjo ya jicho. wakakua vizuri mpaka wakaanza kuota manyoya. week ya tano nikaanza kuwatoa nje, mara nikaona kama
watatu hivi ghafla wakaanza kuvaa makoti.
kwanini wakati nimewachanja na wataalamu waliniambia nikiwachanja chanjo ya jicho hawatapata huo ugonjwa. nimechanganyikiwa maana nategemea kupata vifaranga wasiopungua arobaini maana kuna kuku wanne wanaatamia mayai 15 kila mmoja.
Uko wapi mkubwa uniuzie?