Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ndg yetu Kubota, sijui nianzie wapi kukushukuru wewe na wachangiaji wakuu wote wakiwamo ASIGWA, MAMA JOE, MAMA TIMMY na LIVERPOOLFC. Mimi niliona thread hii mara tu ilipoanza lakini nikasoma kidogo halafu nikaacha. Kwetu Ukaguru nina banda kubwa ambalo hadi sasa halina kuku hata mmoja. Nililijenga mwaka 2008. Sikuwahi kufuga ingawa nililijenga kwa madhumuni ya kufuga kuku wa kienyeji.

Leo kwa masaa kadhaa nimesoma thread nzima na ku- copy yaliyo muhimu. Nimepata ENCYCLOPEDIA YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI ya kurasa 55. Hiki ni encyclopedia ambayo wachangiaji wake ni wengi wakiwamo niliowataja hapo juu. Mbunifu na mchangiaji mkuu wa encyclopedia hiyo ni KUBOTA. Sijui nimshukuru vipi? Naondoka Dar hivi karibuni kurudi kijijini na nitaunda makundi ya vijana, tufuge. AHSANT JAMIIFORUMS, AHSANTE KUBOTA NA WACHANGIAJI WOTE. Nasubiri ili mbele ya safari nipate VOLUME TWO ya encyclopedia hiyo. Nami nitawajuza maendeleo yangu mara tu nikianza ufugaji. Mubarikiwe nyote.
 
Naomba kufahamu namna ya kuepuka wanyama walakuku,magonjwa ya kuku,ukubwa wa banda kwa idad ya kuku ili mwez ujao nianze nk
 

Mkuu LiverpoolFC nakukumbushia ushauri wa Mama Joe nae aliowahikukupa huko nyumba kanunue hizo dawa kwenye maandishi mekundu hapo juu ukawanyweshe kwa kuwafuatilia kama Mama Timmy alivyoshauri. Nadhani tuko pamoja mkuu!
 
wakuu kuna shemeji yangu alikuwa akifuga kuku wa kienyeji waliokuwa wanakaa humo humo bandani,
Mwanzo alikuwa anaendelea vizuri ila huko mbele lilitokea tatizo la Mayai kupotea katika hali ya kutatanisha kidogo.
Nasema hali ya kutatanisha kwasababu banda lake ni chumba cha kisasa cha matofari na kilichopigwa ripu vizuli pia kimeezekwa vizuri kwa bati na madirisha yamewekwa wavu wa kashata ila mayai yamekuwa yakiotea uoni mabaki ya maganda wala nini je anaweza kuwa mdudu gani huyu?
Awali tulidhani kunamtu anachakachua ila hata baada ya kupiga kufuri kwenye mlango hali haikubadilika
 

Hii simulizi yako ina fanana na kile kisa cha Juma Nature.....
 
Naomba kufahamu namna ya kuepuka wanyama walakuku,magonjwa ya kuku,ukubwa wa banda kwa idad ya kuku ili mwez ujao nianze nk

Kama ungekuwa na muda majibu ya kuhusu jinsi ya kuepuka wanyama wala kuku na magonjwa ya kuku ungeyaona yalivyochambuliwa na wachangiaji kuanzia ukurasa wa 9. Nakushauri usome uzi wote ili upate story kamili! Kuhusu ukubwa wa banda na idadi ya kuku hilo linakuja karibuni fuatilia tu huu uzi mkuu, uzi huu hautakatika kamwe!!!
 

Inawezekana ni viumbe wadogo wadogo, mmoja wa kiumbe maarufu anaefahamika siyo tu kwa kula mayai bali saa zingine hata vifaranga ni PANYA!! Panya kwenye mabanda ya kuku ni adui mkubwa hula chakula kilichosalia kwenye vyombo, hula mayai na hata vifaranga wadogo wanapototolewa!
 
Kuku wenyewe huwa wanataba ya kula mayai hadi magand hawachi, hii huwa inatokea hasa wanapokosa chakula chenye virutubisho vya kutosha
 
Naomba kufahamu namna ya kuepuka wanyama walakuku,magonjwa ya kuku,ukubwa wa banda kwa idad ya kuku ili mwez ujao nianze nk
Kuku mmoja anatakiwa square foot 2, yaani upana futi 2 na urefu 2. Zidisha mara idadi ya kuku unaotaka kuwafuga then utapata ukubwa wa banda lako.
 

Mkuu Msuruhishi, tunashukuru sana kwa kututia moyo tutashukuru sana iwapo utatimiza lengo lako maana hapo ndipo lengo na manufaa ya JF yatakapodhihirika! Tutashukuru sana kama mara moja moja ukipita na kuchangia chochote utakachokutana nacho huko kuweza kujazia mawazo, ukikutana na changamoto zozote tushirikishane, na usiache kutoa mwendelezo wa harakati zako huko! Hongera kwa kutengeneza Encyclopedia ninaamini Volume two itakuwa ni ushuhuda wa wachangiaji!!
 
Msuruhishi Mkuu
Kama hutajali Naomba tuwekee Hiyo encyclopedia hapa ili nasi tufaidi
 

Naweza kukubaliana nawe mkuu maana kwenye nyumba yapo mapanya ya kutosha hata mimi nilimueleza hivyo ila hakuamini kabisa maana licha ya mayai kupotea moja moja eneo la kuatamia lilikuwa kavu kabisa halina dalili yoyote ya kuvunjwa yai so jamaa alifikia uhamuzi wa kuipiga bei mifugo yote hapa napoongea banda lipo tupu miezi kadhaa na jamaa hana hamu ya kufuga.
Mimi nataka nijaribu mbinu za Kubota ila ufumbuzi wa hili tatizo la mayai kupotea sijajua bado!!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Shaffin Simbamwene kama kuna panya wa kutosha jambo la kuanza nalo ni kupambana na panya. Hii thread huko nyuma nadhani page kuanzia ya 14 kuna sehemu nilizungumzia jinsi ya kudhibiti panya. Wakati huo huo jiridhishe iwapo kuku wenyewe wanakula au hawali mayai kama alivyochangia Popiexo hapo juu. Pia angalia kama hakuna uwezekano wa nyoka, kenge, au mbwa kuingia na kula mayai bandani. Mwisho ninakusihi wewe na wasomaji wote wenye nia ya dhati kupata mbinu mbadala tulieni msome kwanza thread nzima ndiyo muanze kuuliza kero maana majibu mengi yamo tayari humu!!!
 

pamoja kamanda
 
Karibu sana mkuu...

Shukrani sana kwa mkuu Kubota kwani ndiye mwenye kushikilia mpini hasaa wa thread hii bila yeye tusingepata maujuzi tuliyoyapata hapa...

Karibu sana
 
Last edited by a moderator:

kuna uwezekano mkubwa kuna kenge anaekula mayai kwenye hilo banda.
 
Naomba kufahamu namna ya kuepuka wanyama walakuku,magonjwa ya kuku,ukubwa wa banda kwa idad ya kuku ili mwez ujao nianze nk
Japo haya yalishaongelewa sana huko nyuma ila kwa kifupi kuhusu magonjwa dawa ni kuwachanja kuku wakiwa bado wadogo na kuwapa dawa pale wanapoanza kuonesha dalili za ugonjwa wowote, ila kama ukitaka wawe na afya nzuri na kuogopa kuugua ugua ni bora kila wiki ukawa na kautaratibu ka angalau mara mbili kwa wiki unawapa maji yaliyowekewa mwarobaini, au mlongelonge au aloe vera, u
kifanya hivi kuku wanakua na afya sana na magonjwa hayawanyemelei hasa ukizingatia kuwa kuku wa kienyeji ni wagumu sana kushambuliwa na maradhi
Kitu kingine cha kuzingatia ni kuepuka kuchanganya kuku na bata kwani bata ni carriers(wabebaji) wakubwa wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao haviwadhuru, na hili ni kosa kubwa sana wafugaji wengi wanalifanya hasa vijijini

Kuhusu ukubwa wa mabanda, kwa kawaida kuku wakubwa wanatakiwa 16 kwa mita moja ya mraba kwa mabanda ya kulala, so kama una banda la mita 5 kwa 5 unaweza kulaza kuku 400 yaani (5 x 5 x 16) ila kwa eneo la kuchunga kwa wale wanaofuga nusu huria inafaa kuku kuwekwa 1 kwa mita 10 za mraba, kwa maana kwamba kama una hekari moja ya eneo ambayo ni 70 X 70 unaweza kuweka kuku 490 kwa maana ya (70 x 70 x 0.1). Nafikiri kwa ufupi utakua umenipta
 
Wakuu Kubota, Mama timmy, Mama Joe, LiverpoolFC na wachangiaji woote heshima kwenu..

Katika pita pita zangu nimekutana na hili tena ambalo nadhani japo nimeliongelea kidogo hapo juu nilipokua nachangia uzi ila si vibaya nikalipa msisitizo hapa.

Wataalamu wamegundua kuwa BATA na KANGA hawafai kuchanganywa na kuku katika ufugaji hasa wa kijasiriamali kwani ndege hawa hubeba vimelea, bacteria na virus hatari sana wanaowadhuru kuku kwa maana ya magonjwa, Kati ya hawa mbaya zaidi ni bata kwani huwa na uwezo mkubwa sana wa ku-survive na hawa vimelea kama carrier maisha yake yote bila yeye kudhurika au kuonesha dalili ypyote ya ugonjwa na vimelea hawa wana uwezo wa kujizalisha kwenye mwili wake kwa kasi ya ajabu sana.

Kwa maana kuwa, kwa kuwa kuku wengi hushambuliwa na magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi huja kwa msimu(baadhi ya miezi ya mwaka kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa),msimu wa magonjwa unapopita vimelea huamia kwenye miili ya BATA na kuishi humo na kama kuku wako hawajachanjwa basi utakua na MLIPUKO WA MAGONJWA kwa mwaka mzima hata kama kuku wa jirani hawaugui lakini wako wataugua, kifupi ni kuwa BATA ni kiwanda cha magonjwa ya kuku hata kama hakuna mlipuko wa magojwa.

Bado nafuatilia kwa undani kuhusu KANGA na uwezo wake wa kubeba vimelea ila nikipata details nzuri nitaleta hapa..

Heshima kubwa sana kwenu

NB
Ningependa kufahamu kama kuna athari zozote wanazoweza kupata kuku wa kienyeji kiafya kama nitawachanganyia ALOE VERA, MCHUNGA,PILI PILI KICHAA, MLONGELONGE na MUAROBAINI kwenye maji vyoote kwa pamoja. Nimeuliza maana naona karibu kila kimoja ni dawa ya kuku wa kienyeji, so naona kama kuna uwezekano wa kuandaa tiba mbadala ya kuku kwa kuchanganya vyoote hivi halafu navisaga kuwa unga nakuwa nawapa kuku wangu angalau mara mbili kwa wiki kuwaongezea kinga ya mwili japokuwa nitakuwa nimeshawachanja

Kama kuna mtu anaweza kujua ratio ya uchanganyaji huu amwage hapa jamvini ili tufaidishane woote
 
Asigwa nashukuru sana kwa kunipa taarifa hii.hapa nina bata mzinga na kanga wachache nitawatenga ili kuepusha hayo matatizo.ubarikiwe ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…