Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 533
- 1,101
apo Kubota ndio nilikuwa nasubiri kwa hamu coz nakosa usingiz na hesab za ujenzi
Mkuu Ankojei kumbuka hapa ninaongelea ufugaji wa kuku wa kienyeji! Kwa mwenye nafasi anaweza kujenga mabanda yenye hadhi kubwa na mwonekano wa kuvutia zaidi kulingana na kiwango cha uchumi wake. Isipokuwa kibiashara wakati mwingine ukitumia material cheap zaidi unapata faida kubwa zaidi. Kwa hiyo mimi sikutaka kutumia material ghari kwa makusudi. Jamii yoyote ikizidi kuwa na maendeleo kiuchumi watu hupenda kujenga vitu nadhifu vyenye kuvutia macho ikiwemo mabanda ya mifugo. Kwa hiyo Mkuu Ankojei hunasababu kukosa usingizi shauri ya ujenzi wa mabanda ya kuku, tumia materils kulingana na pale mkono wako unapofika, na zingatia zaidi faida kubwa! Kuku wa kienyeji asilimia kubwa ya muda wanakuwa nje kwa hiyo mabanda haya huwa zaidi ni kwa ajili ya kulala usiku, kutagia mayai na kuatamia! Hauhitaji kuwa na mabanda makubwa kama ya kuku wa kufugia ndani muda wote! Kuku wa kienyeji wanapolala usiku huwa na tabia ya kubanana, kwa hiyo hata kibanda kidogo sana kinaweza kulaza kuku wengi tofauti na mabanda ya kuku wa kisasa. Kitu cha kuzingatia ni kuwa na madirisha makubwa ili kuweza kuingiza hewa na kuruhusu mzunguko wa hewa bandani pia usafi kutoa kinyesi bandani mara kwa mara kwa vile kuku huwa wanarundikana sehemu moja.
Kwa hiyo unaweza kuona mfano wa picha ya mabanda yangu, tazama size ya madirisha na kibanda utapata picha. Kama unaweza kuezeka kwa mabati ni sawa, au makuti au nyasi ni uchaguzi wako. Pia unaweza kupiga lipu ndani kwa urahisi wa kufanya usafi au inategemea nafasi yako. Unaweza kuwa na vibanda vingi vya mfano huu kadri uwezavyo kuliko kuwa na banda moja kubwa maana inakuwa rahisi kutenga kuku wa makundi tofauti kila kibanda na kuku wanakuwa mbali mbali. Ndani ya hayo mabanda hayo nilikuwa nasambaza pumba za mpunga au kutandaza manyasi chini kina cha inchi 6, au sm 15. Kila mara nilikuwa najisikia hamu kwenda kuchungulia mifugo ndani mabanda hayo.