Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

apo Kubota ndio nilikuwa nasubiri kwa hamu coz nakosa usingiz na hesab za ujenzi

Mkuu Ankojei kumbuka hapa ninaongelea ufugaji wa kuku wa kienyeji! Kwa mwenye nafasi anaweza kujenga mabanda yenye hadhi kubwa na mwonekano wa kuvutia zaidi kulingana na kiwango cha uchumi wake. Isipokuwa kibiashara wakati mwingine ukitumia material cheap zaidi unapata faida kubwa zaidi. Kwa hiyo mimi sikutaka kutumia material ghari kwa makusudi. Jamii yoyote ikizidi kuwa na maendeleo kiuchumi watu hupenda kujenga vitu nadhifu vyenye kuvutia macho ikiwemo mabanda ya mifugo. Kwa hiyo Mkuu Ankojei hunasababu kukosa usingizi shauri ya ujenzi wa mabanda ya kuku, tumia materils kulingana na pale mkono wako unapofika, na zingatia zaidi faida kubwa! Kuku wa kienyeji asilimia kubwa ya muda wanakuwa nje kwa hiyo mabanda haya huwa zaidi ni kwa ajili ya kulala usiku, kutagia mayai na kuatamia! Hauhitaji kuwa na mabanda makubwa kama ya kuku wa kufugia ndani muda wote! Kuku wa kienyeji wanapolala usiku huwa na tabia ya kubanana, kwa hiyo hata kibanda kidogo sana kinaweza kulaza kuku wengi tofauti na mabanda ya kuku wa kisasa. Kitu cha kuzingatia ni kuwa na madirisha makubwa ili kuweza kuingiza hewa na kuruhusu mzunguko wa hewa bandani pia usafi kutoa kinyesi bandani mara kwa mara kwa vile kuku huwa wanarundikana sehemu moja.

Kwa hiyo unaweza kuona mfano wa picha ya mabanda yangu, tazama size ya madirisha na kibanda utapata picha. Kama unaweza kuezeka kwa mabati ni sawa, au makuti au nyasi ni uchaguzi wako. Pia unaweza kupiga lipu ndani kwa urahisi wa kufanya usafi au inategemea nafasi yako. Unaweza kuwa na vibanda vingi vya mfano huu kadri uwezavyo kuliko kuwa na banda moja kubwa maana inakuwa rahisi kutenga kuku wa makundi tofauti kila kibanda na kuku wanakuwa mbali mbali. Ndani ya hayo mabanda hayo nilikuwa nasambaza pumba za mpunga au kutandaza manyasi chini kina cha inchi 6, au sm 15. Kila mara nilikuwa najisikia hamu kwenda kuchungulia mifugo ndani mabanda hayo.
 
Nashukuru mkuu Kubota, mbinu ya JELA na kuweka alama kwenye mayai imenisaidia saaana, naendelea kuitumia.

Mkuu Yekevalia nashukuru kuleta mshindo nyuma (feed back) ni ushirikiano unaotarajiwa, huo ushuhuda wako ndiyo unaofundisha wasomaji kuliko hata story yenyewe, nashukuru na endelea kutekeleza na mengine na usichoke kutujulisha kama ulivyofanya.
 
Mkuu Kubota asante sana kwa huu uzi, nimenufaika sana, nilikuwa na vitetea vyangu 3 ile february ulipoanzisha hii thread, na tulikuwa tunafuga kwa kula tuu with no extra care kwa hao kuku lakini baada ya kusoma uzi huu nikajifunza kitu, nikasema hao watatu watakuwa ni mtaji kangu! kwa sasa nina vinyoya vya miezi miwili na nusu kumi na mbili na wale matetea watatu wana wanatamia mayai ishirini na tano jumla! ntakuja kushare na nyinyi changamoto zangu , lakini nyingi nakabaliana nazo kupitia maelezo ya uzi huu...mbarikiwe!
 
asigwa
Kubota
Mama timmy
Mama Joe

Nawasalimu wote katika jina lake Bwana wetu Yesu Kirsto aliye hai na hata sasa!
amen! Tunashukuru kutumbuka, kwa uwezo wa Mungu tunapambana. Nimefurahi kukuta feedback nyingi vilevile na mwl wetu karudi na somo zuri. Kubota, asante kwa darasa nalipitia kwa makini maana niko transition ya kuhamia eneo kubwa. Kweli feedback zinatia moyo sana, lakini pia kama mwl wetu anavyosema watu wakitaka kufuga wanafikiri hadi wawe na mabanda expensive wakati mipango miji inabadilika kila leo unaweza hamishwa au zuiwa kabla hujapata faida. Kuna watu niliwaelekeza ufugaji kuku wa kisasa walianza kwa kujenga mabanda expensive ya tofali, hawajayatumia hata mwaka wameghairi yanatunza buibui tu. Ukianza kidogokidogo haikugharimu, kila mwezi unatumia hela kidogo kuendeleza kuku wako. Baada ya muda wanaanza kujihudumia wenyewe, changamoto zipo, lakini ukivumilia na faida ipo sana. Mbarikiwe sana na weekend njema
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kubota asante sana kwa huu uzi, nimenufaika sana, nilikuwa na vitetea vyangu 3 ile february ulipoanzisha hii thread, na tulikuwa tunafuga kwa kula tuu with no extra care kwa hao kuku lakini baada ya kusoma uzi huu nikajifunza kitu, nikasema hao watatu watakuwa ni mtaji kangu! kwa sasa nina vinyoya vya miezi miwili na nusu kumi na mbili na wale matetea watatu wana wanatamia mayai ishirini na tano jumla! ntakuja kushare na nyinyi changamoto zangu , lakini nyingi nakabaliana nazo kupitia maelezo ya uzi huu...mbarikiwe!

Asante Mkuu Nailyne ni wachache sana wanaotoa feedback ingawa ni wengi sana wanafuatilia maandiko haya, nashukuru na endelea kutupa updates zako maana hizo ndiyo zinasaidia kureinforce maarifa! Fuatilia kwa karibu maelekezo ya wachangiaji humu ni shule tosha Mkuu!
 
amen! Tunashukuru kutumbuka, kwa uwezo wa Mungu tunapambana. Nimefurahi kukuta feedback nyingi vilevile na mwl wetu karudi na somo zuri. Kubota, asante kwa darasa nalipitia kwa makini maana niko transition ya kuhamia eneo kubwa. Kweli feedback zinatia moyo sana, lakini pia kama mwl wetu anavyosema watu wakitaka kufuga wanafikiri hadi wawe na mabanda expensive wakati mipango miji inabadilika kila leo unaweza hamishwa au zuiwa kabla hujapata faida. Kuna watu niliwaelekeza ufugaji kuku wa kisasa walianza kwa kujenga mabanda expensive ya tofali, hawajayatumia hata mwaka wameghairi yanatunza buibui tu. Ukianza kidogokidogo haikugharimu, kila mwezi unatumia hela kidogo kuendeleza kuku wako. Baada ya muda wanaanza kujihudumia wenyewe, changamoto zipo, lakini ukivumilia na faida ipo sana. Mbarikiwe sana na weekend njema

Asante sana Mama Joe, umeongea maneno mazito, una mifano hai, ukweli ndiyo huo!!
 
Mkuu kubota..kwanza shukran kwahii post..ubarikiwe sana...swali langu..nilipata habari kwa jamaa yangu eti ukitaka kuku asiatamie inapokuwa umefikia wakati wake unamtumbukia kichwa kwenye maji baridi!kuna ukweli wowote? Ahsante
Mkuu njia hiyo inatumika na inafanya kazi vizuri sana..Tatizo inahitaji muda na si efficient sana hasa ukiwa na mradi mkubwa na kuku wengi.

Njia rahisi ni ile ya mkuu KUBOTA ya kutumia JELA.Kama huijui pitia post za nyuma kwenye huu uzi utaipenda sana...
 
Mkuu Ankojei kumbuka hapa ninaongelea ufugaji wa kuku wa kienyeji! Kwa mwenye nafasi anaweza kujenga mabanda yenye hadhi kubwa na mwonekano wa kuvutia zaidi kulingana na kiwango cha uchumi wake. Isipokuwa kibiashara wakati mwingine ukitumia material cheap zaidi unapata faida kubwa zaidi. Kwa hiyo mimi sikutaka kutumia material ghari kwa makusudi. Jamii yoyote ikizidi kuwa na maendeleo kiuchumi watu hupenda kujenga vitu nadhifu vyenye kuvutia macho ikiwemo mabanda ya mifugo. Kwa hiyo Mkuu Ankojei hunasababu kukosa usingizi shauri ya ujenzi wa mabanda ya kuku, tumia materils kulingana na pale mkono wako unapofika, na zingatia zaidi faida kubwa! Kuku wa kienyeji asilimia kubwa ya muda wanakuwa nje kwa hiyo mabanda haya huwa zaidi ni kwa ajili ya kulala usiku, kutagia mayai na kuatamia! Hauhitaji kuwa na mabanda makubwa kama ya kuku wa kufugia ndani muda wote! Kuku wa kienyeji wanapolala usiku huwa na tabia ya kubanana, kwa hiyo hata kibanda kidogo sana kinaweza kulaza kuku wengi tofauti na mabanda ya kuku wa kisasa. Kitu cha kuzingatia ni kuwa na madirisha makubwa ili kuweza kuingiza hewa na kuruhusu mzunguko wa hewa bandani pia usafi kutoa kinyesi bandani mara kwa mara kwa vile kuku huwa wanarundikana sehemu moja.

Kwa hiyo unaweza kuona mfano wa picha ya mabanda yangu, tazama size ya madirisha na kibanda utapata picha. Kama unaweza kuezeka kwa mabati ni sawa, au makuti au nyasi ni uchaguzi wako. Pia unaweza kupiga lipu ndani kwa urahisi wa kufanya usafi au inategemea nafasi yako. Unaweza kuwa na vibanda vingi vya mfano huu kadri uwezavyo kuliko kuwa na banda moja kubwa maana inakuwa rahisi kutenga kuku wa makundi tofauti kila kibanda na kuku wanakuwa mbali mbali. Ndani ya hayo mabanda hayo nilikuwa nasambaza pumba za mpunga au kutandaza manyasi chini kina cha inchi 6, au sm 15. Kila mara nilikuwa najisikia hamu kwenda kuchungulia mifugo ndani mabanda hayo.
Mkuu hapo kwenye point ya kuku wa kienyeji kulala wakiwa wanapenda kubanana umenikuna sana, Hii kwangu naona kama ni advantage sana kwani ninajenga banda la kawaida halafu sehemu ya kulala naweka fito kama ngazi mbili hivi halafu napanua size ya madirisha ili hewa iingie.

Nafikiri kwa kutumia mfumo huu naweza kulaza kuku wengi ndani ya sehemu ndogo bila kuwa na athari za kiafya kwao...
 
Mkuu Yekevalia nashukuru kuleta mshindo nyuma (feed back) ni ushirikiano unaotarajiwa, huo ushuhuda wako ndiyo unaofundisha wasomaji kuliko hata story yenyewe, nashukuru na endelea kutekeleza na mengine na usichoke kutujulisha kama ulivyofanya.
Nimeipenda hii ya mshindo nyuma yaani feedback...ha ha ha ha kaazi kweli kweli mzee wa vitanuru vya mkaa......
 
Wakuu msishangae kwamba hii kitu ninapost hapa ni nini tena?!! Remember this is my story, ninasimulia nilikotokea, nilikoanzia, ilikuwa ni simple kama hivyo, kwangu ndiko nilikoanzia, kulikoni kuonesha high level nilipofikia leo inaweza kuonekana kama vile mimi nilikuwa na nguvu sana ya mtaji hapana, nilianza as simple as you can see! Hivi vibanda nimevibakisha kama ukumbusho (museum) na sitavivunja kamwe! Kwa hiyo msijisikie vibaya kuona structure too simple and too ugly to look at, that is where everything originated!! Ninawasilisha kwenu kibanda cha kukuzia vifaranga! Nursery! Ghorofa moja! Imeezekwa kwa makuti! Kila foor ilikuwa ina vyumba 3! Juu vyumba vitatu, chini vitatu! Partitions za vyumba nilikata kwa kumia chicken wire mesh na kusupport na old used carpet. Kila kijichumba kilijitegemea kwa kuwa na mlango wake. Huyo mbwa kasimama mlangoni mwa moja ya chumba cha chini. Juu ya mbwa kuna mlango wa chumba cha juu uko wazi pia ukitazama kwa makini utauona mlango uko wazi, chumba kinachofuata ghorofani kuna ndoo iko kwenye mlango wa chumba hicho na uko wazi ukitazama utauona uko wazi, chini ya mlango huo kuna mlango wa chumba cha floor ya chini nao uko wazi, banda liliendelea hivyo hivyo hapo vimesalia vyumba viwili cha juu na cha chini ndiyo vimekatwa kwenye picha! Kila chumba niliweka mama na watoto 30 baada ya kunyanganya wengine kule banda la kutotolea! Kichumba kimoja nilikitumia kama JELA! Dirisha na sehemu za uwazi zilizibwa kwa chicken wiremesh, ndani ya kila chumba ili kupuguza baridi ya upepo nilifunika uwazi kwa used carpets (carpet za plastic zilizotumika) kwenye floor nilisambaza pumba za mpunga! Kila chumba niliweka chombo cha maji na cha chakula! Nimeweka pia picha ya kuku mwenye vifaranga 30, utaona vyombo vya chakula na maji, utaona jinsi nilivyofunika carpet dirishani na mazingira ya chumba kwa ujumla! Wakuu hako kalikuwa ni kakiwanda kadogo (minifactory) ka kufyatulia vinyoya! Hapo kuna yule mlinzi wangu alietukuka (mbwa jina lake SUNCHE mwenzake anaitwa KAPETO) yuko hapo kukuonyesha size halisi ya banda hilo (scale). With great love I PRESENT TO YOU A CHICKEN NURSERY !!!!!!!!!!!!!!!!!!!! (msinicheke he he heee!!)
 
Attachments

  • Chicken nursery.jpg
    Chicken nursery.jpg
    51.5 KB · Views: 566
  • Chicken Nursery 2.JPG
    Chicken Nursery 2.JPG
    315.2 KB · Views: 423
  • Chicken nursery 3.JPG
    Chicken nursery 3.JPG
    290.2 KB · Views: 423
Asante sana Kubota, anayecheka nadhani sio mjasiriamali, mimi nataka nione mtu alikotokea kama hivi inatia moyo sana, hako kaghorofa naona ndio nitaanza nako huku wanapoongezeka nabadili materials au kuongeza ukubwa wa mabanda basi sitaki pressure.
Kwa walio kwenda Sabasaba JKT waliweka vibanda design hizi na kuku, bata maji, bata mzinga na contacts zao ukihitaji, mwaka huu pia wadau mkipata nafasi njooni kuna mengi ya kujifunza. Pia kuna mbegu mbalimbali nyingi za Mlonge, mahindi ya miezi 3, miti ya matunda, incubators na machine zinginezo.
Kubota na wengineo mbarikiwe sana
 
Kubota
Hakika atakayecheka ni wale wajasiriamali feki na siyo majasiamali bali ni sharo tu!
Hapo ulipo tuonyesha hakika wewe ni mpango mzima full.

Mama timmy
Mama Joe
asigwa
Kubota

Kumbukeni niliwaambia ya kwamba nina vinyoa visiopungua 65 vilivyolivyototolewa tar 25.02 na kwa msaada wa thread hii hawajafaga mpaka majuzi nimewatenganisha na mama yao na ndipo nikaanza kuona kama watatu wanne wameshusha mabawa na mpaka juzi wakafa watatu na leo asubuhi niliporudi toka kibaruani nikakuta tena mmoja kafa. Loh! Nikasema niwajuze kama kuna namna ya kuwanusuru na mnijuze wadau wenzangu.
Ila tangu wiki ile iliyopita nilileta dawa aina hii na Ancoban Amprolium 20% + na NORFLOX 20% na hii ya pili ni kwa ajili ya mafua.
Ila bado wangine kama watatu wanazinzia wajamen.
Ni hayo tu na kwa kuwa tu pamoja hakika nategemea ushauri mzuri zaidi.

ASANTENI!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu popiexo pamoja na dawa zote utakazoona zinafaa kuwapa kuku pia unatakiwa uzingatie lishe bora kwa kuku.na hapa naomba niweke vzr unatakiwa uhakikishe kuwa kuku mgonjwa ametengwa na wazima na anakula chakula cha kutosha pamoja na dawa.ili kujua Kama amekula ni lazima uangalie kifuko chake cha chakula na Kama ukiona hakina chakula basi umlishe Kama mtoto mpaka utakapojiridhisha kuwa ameshiba na umnyweshe dawa kiasi Fulani ili uwe na uhakika kuwa amekunywa dawa.uendelee kumfuatilia kwa ukaribu sana pale utakapoona kuna Shida umsaidie.usiweke tu chakula na dawa halafu uondoke.utakuta mizoga tu bandani.siku njema

LiverpoolFC ushauri huu wa Mama Timmy alioutoa kwa Popiexo siku za nyuma naomba nawe uuzingatie, utakapokuwa unawahudumia hawa wagonjwa wako zingatia umaridadi huo kwa kiwango hicho cha Mkuu Mama Timmy!
 
Back
Top Bottom