Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Du... Kuna Kirusi Kimekula file la uzi huu kwenya PC ya Mleta Uzi... na hakumbuki alichoandika.
 
ndo nimemaliza kujenga banda, mbinu zako zitanisaidia mbeleni
 
Kusema kweli jf ni zaidi ya chuo kikuu! Najifunza mengi humu ndani. Mbarikiwe nyote mnaotoa elimu bure!
 
Kwanza kabisa napenda nikupongeze kwa kuchukua uamuzi wa kutuelimisha namna ya kufuga kuku kwa lengo la kuongeza tija, nilitamani sana kupata mwongozo wa namna gani nifuge kwa muda mfupi nikawa na idadi kubwa ya kuku, kwa mwongozo huu nimeanza kupata picha kamili kuwa ipo siku n'takuwa 'millionaire'. Ombi langu kwako nikwamba kama inawezekana, naomba kila 'EPISODE' unipatie maelekezo kwenye E-mail yangu( lukubayunge@gmail.com) kisha n'takuwanakupa mrejesho wa mafanikio. Kila la kheri
 
Mkuu chama2chawa: Umeleta hoja ngumu na pana sana kuweza kuielezea kwa utoshelevu ikaweza kukidhi haja. Ni hoja inayoweza kuzua malumbano yasiyoisha kiasi cha kuharibu uelekeo wa hii THREAD. Maana hoja hii imejikita kwenye imani zilizojichimbia sana kwenye jamii nyingi za kiafrika na imani hizi zinatutafuna sana tusiweke juhudi ya kung’ang’ania zaidi kuyatafuta yale tunayoamini yanaweza kutuinua kimaendeleo. Imani hizi ndiyo kwa mapana yake watu wanajikuta kwenye kutafuta ndumba zinazodhuru hadi maisha ya watu ili wapate kinachoitwa ngekewa au waondoe nuksi!

Suala hilo linawatatiza zaidi watu ambao hawajaelimika. Kadri jamii au watu wanavyoelimika zaidi ndiyo jinsi ambavyo imani kama hizo zinapungua! Mtu aliyeelimika hutamjua kwa kumiliki vyeti na madigrii bali utamjua kwa anayojiamini na kwa matendo yake, mtu aliyeelimika anatarajiwa ahusishe kufikiri juu ya ukweli wa lile analoliamini na siyo kukariri mambo kama tunavyokaririshwa bila kuhoji vitabu vya dini!

NGEKEWA au NUKSI ni maneno ambayo huyatumia watu wanaojifariji kwa kutafuta majibu rahisi kwa masuala magumu! Mtu aliefanikiwa watu humwelezea kuwa ana NGEKEWA na mtu aliyeshindwa kufanikiwa humchukulia ana NUKSI. Dunia ya leo (ya sayansi na technolojia) mtu ambaye bado anaamini hivyo atachelewa sana au ataishia kubaki nyuma! Mtu anaedhani ana mkono mbaya na akaamini hivyo huyo maendeleo hawezi kuyapata kamwe!

Hakuna binadamu anaeng’ang’ania kujifunza jambo akashindwa kulijua, tunaweza kutofautiana spidi ya kuelewa jambo tunapojifunza lakini mwisho wa siku mtu utaelewa tu, ndiyo maana tunavaa suluali, mashati na viatu kwa usahihi, kwenye vyoo vyetu vya shimo tunalenga vizuri tu, yote haya tulijifunza hatukuzaliwa tukijua yote haya na kama huamini kumbuka jinsi mtoto anavyopishanisha matundu anapoanza kufunga vifungo vya shati siku za mwanzo, au kubadili viatu mguu kulia kuvaa kushoto.

Ikitokea mtu umefanya jambo mara moja, mbili, tatu hata mara nne usifanikiwe siyo sahihi kujichukulia kwamba una nuksi au unadamu mbaya! Kama una imani juu ya jambo unalolifanya kwamba ukilimudu kulifanya linaweza kukuinua basi wewe endelea kulifanya tu maana kadri unavyoendelea kupiga mieleka ndiyo unavyozidi kulielewa vizuri zaidi mwishoni kitaeleweka tu.

Kuhusu mfano wa mpandaji wa hoho ulioutoa anaweza akawa na mkono mbaya kwa maana ya kwamba hajui kupanda hoho! Je alikuwa anapanda kwa usahihi? Ni rahisi sana kufanya utafiti ili kujua kama ni mwili wake ndiyo wenye nuksi na siyo kwamba hajui kupanda. Aende akapande sehemu tatu tofauti na watu wengine ili ionekane kama kote huko matokeo ni yale yale! Ikitokea hivyo tueleze hapa JF tumtangaze huyo Bwana maana wenzetu wa nchi zilizoendelea huyo jamaa kwao atakuwa kivutio kikubwa sana cha utalii na itabidi wampime hata damu yake waichunguze! Kwamba yeye kila akipanda hoho haziponi au hazizai au hazisitawi lol!

Kupanda miche au mbegu siyo ni kule kufukia mche kwenye udongo tu, kuna mbinu zake! Kwenye kilimo cha vitunguu na mpunga mimi mwenyewe nimewahi kukutana na baadhi ya wapandaji wangu vibarua kadhaa ambao wamewahi kunisababishia hasara kwa miche waliyopanda kufa au kutokusitawi vizuri! Hii ilitokana na wao wanapopanda wanashika miche vibaya, wanaishikia katikati ya mche na kuizamisha hivyo hivyo kwenye udongo na inajikunja kama herufi ya U, yaani majani na mizizi inatokeza juu, shina ndiyo linazamishwa chini! Yaani mche unapandikizwa lakini ukiutazama unakuta mizizi yote imetokeza juu ya udongo! Mpandaji huyo unakuta ile strip aliyopanda yeye ama miche inakufa au inakuwa dhaifu tofauti kabisa na walikopanda wengine! Mpandaji huyu akisakamwa kuwa akipanda miche inakufa au haizai vizuri atajiona ana mkono mbaya! Kuna mifano mingi tu ya aina hii ambapo watu kwa kuwa makini wengine wanafanikiwa na kuitwa wana ngekewa au damu nzuri na wengine kwa kutokuwa makini hawafanikiwi na wanaonekana wana damu mbaya au nuksi!

Kwa hiyo Mkuu chama2chawa kujibu hoja yako kuwepo ngekewa au kutokuwepo ngekewa kwenye eneo lolote la maisha inategemea wewe ni mtu wa mlengo gani! Watu walioelimika hilo wala siyo suala la kujadili kabisa!

Kuna jambo moja tu kwa uhakika kabisa ambalo lipo nalo linaitwa CHANCING hilo kwa hakika lipo! Kwa mfano ugonjwa wa kuku unaweza kukumba eneo fulani tu eneo lingine kuku wakasalimika; mvua inaweza kunyesha eneo fulani watu wakaokoa mazao na eneo lingine isinyeshe yakakauka; mtu anaweza kuuza hoho sokoni leo, kesho yake jirani yake akaingiza mzigo sokoni akakuta bei imeshuka au imepanda, unaweza kununua chanjo imekufa bila kujua kuku wako wakaugua na kufa jirani yako akaenda nunua kwingine chanjo nzima akatibu kuku wake wakabaki salama n.k. Lakini wataalamu wanasema kuwa kunachochangia sana kwenye mafanikio ya shughuri mbalimbali asilimia 5% ni CHANCING, na 95% inatokana na Management! Kwa hiyo iwapo kama chancing ni NGEKEWA (au NUKSI) mchango wake kwenye kufanikiwa ni asilimia 5% tu si kitu cha kutegemea wala si kitu cha kuhofia.

Kweli wewe ni mwalimu, nimenufaika nawewe Kubota. Ubarikiwe sana
 
Kwanza kabisa napenda nikupongeze kwa kuchukua uamuzi wa kutuelimisha namna ya kufuga kuku kwa lengo la kuongeza tija, nilitamani sana kupata mwongozo wa namna gani nifuge kwa muda mfupi nikawa na idadi kubwa ya kuku, kwa mwongozo huu nimeanza kupata picha kamili kuwa ipo siku n'takuwa 'millionaire'. Ombi langu kwako nikwamba kama inawezekana, naomba kila 'EPISODE' unipatie maelekezo kwenye E-mail yangu( lukubayunge@gmail.com) kisha n'takuwanakupa mrejesho wa mafanikio. Kila la kheri

Sawa Mkuu nitajitahidi kufanya hivyo mrejesho wako ndiyo manufaa makubwa kwa wanajamii hapa JF.
 
Wadau hadithi yangu bado inaendelea, sijasimulia bado kuhusu ujenzi wa mabanda yangu na mpangilio wake ulivyokuwa, nitakuja pia na kitu kinaitwa grazing pattern. Kwa wanaotaka kufuga maeneo makubwa ufugaji huria, kwa wale watakaopata nguvu na kujipanua kufuga maeneo makubwa kuku kuanzia miatano na hadi zaidi ya alfu moja, kuna design inakuja. Hakuna haja ya kukata tamaaa, Tanzania yetu fursa zipo nyingi sana tatizo fursa ya kupata elimu hii ndiyo finyu, tumieni JF hapa ni zaidi ya chuo. Ninakuja kivingine. Hata nikichelewa maana nimeanzisha tena kuchoma mikaaaa, STAY TUNED..................!!!!!
 
Mkuu Pole na majukumu hakika tuko pamoja bega kwa bega. thanks.
 
Mungu akubariki Mama Joe! Bado kuna watu wema katika Taif Letu! Idumu Jamii Forums!
 
Last edited by a moderator:
apo Kubota ndio nilikuwa nasubiri kwa hamu coz nakosa usingiz na hesab za ujenzi
 
Last edited by a moderator:
Oh asante sana ila umshukuru Kubota kwa kujitoa toka mwanzo kuturithisha ujuzi wake. Sie wengine wanafunzi tu, pamoja tunawezeshana. Karibu sana ndugu tujifunze.
Mwl wetu Kubota tunalusubiri kuhusu grazing kwa hamu. Asante Reti kwa somo la ndui, vipi hakuna chanjo ya kunywa? Hii ya mmoja naona ngumu.
Mungu akubariki Mama Joe! Bado kuna watu wema katika Taif Letu! Idumu Jamii Forums!
 
Last edited by a moderator:
ndugu yangu mm nataka sana kuwa tajiri ila jambo 1 nikuulize sasa kwa sisi watu tuliopanga kwenye nyumba za watu tutafanyeje ili tuweze kuanzisha huo mradi wa kuku uliotuorodheshea namna ya kufanya hapo maana wenye nyumba wengi hawapendi kuharibu mazingira yao nisaidie nifanyeje ilia nami niondokane na hali hii ya kimaskini na nnijikwamue kivipi mkuu msaada pls
Ni kweli unachozungumza lakini nilichokua natoa hapo ni kama dira tu jinsi kuku wanavyoweza kuwa mtaji muhimu. Ujenzi wa banda na mahitaji mengine yanategemea na mahali ulipo, Mtu aliye kijijini au mwenye shamba ana nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.jambo muhimu kuhusu gharama za kujenga banda linategemea zaidi na changamoto za mahali ulipo. Mfano Mtu wa Dar atatakiwa kujenga banda ambalo licha ya kuwaweka kuku katika hali nzuri pia atatakiwa aangalie jinsi ya kuwalinda kuku hao na wezi. Wako ambao watakabiliwa na changamoto za mwewe na kadhalika. Mwisho nimetoa ushauri watu wafanye utafiti zaidi kwani mimi naweza kueleza lakini nikawapoteza kulingana na utofauti wa jiografia ya mahali niliko.
 
Wadau hadithi yangu bado inaendelea, sijasimulia bado kuhusu ujenzi wa mabanda yangu na mpangilio wake ulivyokuwa, nitakuja pia na kitu kinaitwa grazing pattern. Kwa wanaotaka kufuga maeneo makubwa ufugaji huria, kwa wale watakaopata nguvu na kujipanua kufuga maeneo makubwa kuku kuanzia miatano na hadi zaidi ya alfu moja, kuna design inakuja. Hakuna haja ya kukata tamaaa, Tanzania yetu fursa zipo nyingi sana tatizo fursa ya kupata elimu hii ndiyo finyu, tumieni JF hapa ni zaidi ya chuo. Ninakuja kivingine. Hata nikichelewa maana nimeanzisha tena kuchoma mikaaaa, STAY TUNED..................!!!!!

Mkuu Kubota mbona umetuachia njiani mkuu...
Tunaomba hii knowledge ya kujenge mabanda ya kufuga maeneo makubwa mfano hekari kumi...

Tuko pamoja sana mkuu....
 
Last edited by a moderator:
Ladyfurahia naomba nikujibu swali lako hapo juu, nyumba ya kupanga kama ina fence unaweza kufuga kuku kwa kutumia vile vibanda vidogo vya kuwalaza usiku kisha mchana unawaachia nje kama kuna fence haina neno ila tatizo wanaharibu vimimea vidogo kama mboga na hata maua ila miti mikubwa haitaadhirika. Kuna mtu alitoa hapa tangoza anaviuza vile nimobile unahama nacho na ni vya ghorofa kiasi wanakaa kuku wengi. wenye nyumba jawapendi ujenge mabanda wanasema yanaharibu mwonekano na pia yaweza leta ugomvi na majirani kama si msafi. Endapo huna fence basi nakushauri tafuta eneo lako taratibu uweke mtu akutunzie.
 
Mkuu asigwa ulipotea kabisa jamvini kwetu, ngoja naweka sawa picha na michoro maana picha na michoro zinaongea maneno zaidi ya maelezo matupu, afu mvua zikizidi ile biashara ya mkaa inachanganya sana, mgodi unatema kiaina. Nitaleta somo hilo punde. Tuko pamoja.
 
Mimi jukwaa la siasa halina faida kwangu.,napenda sana hili jukwaa wa wajasiriamali,bsness &econmy.
I like it,yani mtu unapat vitu vya kukukomboa,afu hili jukwaa watu wapo serious na kazi,halina waropokaji na wazozaji kama kuuule politics forum.
 
Back
Top Bottom