Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
usisikilizie ,ukianza post ya kwanza kusoma ,mpaka hapa ilipofikia utakua umeshiba na kuanza kutendea kazi yale yaliyojadiliwaNouma kweli' endelea kutoa elimu bana nakuckilizia beste.
Mkuu chama2chawa: Umeleta hoja ngumu na pana sana kuweza kuielezea kwa utoshelevu ikaweza kukidhi haja. Ni hoja inayoweza kuzua malumbano yasiyoisha kiasi cha kuharibu uelekeo wa hii THREAD. Maana hoja hii imejikita kwenye imani zilizojichimbia sana kwenye jamii nyingi za kiafrika na imani hizi zinatutafuna sana tusiweke juhudi ya kungangania zaidi kuyatafuta yale tunayoamini yanaweza kutuinua kimaendeleo. Imani hizi ndiyo kwa mapana yake watu wanajikuta kwenye kutafuta ndumba zinazodhuru hadi maisha ya watu ili wapate kinachoitwa ngekewa au waondoe nuksi!
Suala hilo linawatatiza zaidi watu ambao hawajaelimika. Kadri jamii au watu wanavyoelimika zaidi ndiyo jinsi ambavyo imani kama hizo zinapungua! Mtu aliyeelimika hutamjua kwa kumiliki vyeti na madigrii bali utamjua kwa anayojiamini na kwa matendo yake, mtu aliyeelimika anatarajiwa ahusishe kufikiri juu ya ukweli wa lile analoliamini na siyo kukariri mambo kama tunavyokaririshwa bila kuhoji vitabu vya dini!
NGEKEWA au NUKSI ni maneno ambayo huyatumia watu wanaojifariji kwa kutafuta majibu rahisi kwa masuala magumu! Mtu aliefanikiwa watu humwelezea kuwa ana NGEKEWA na mtu aliyeshindwa kufanikiwa humchukulia ana NUKSI. Dunia ya leo (ya sayansi na technolojia) mtu ambaye bado anaamini hivyo atachelewa sana au ataishia kubaki nyuma! Mtu anaedhani ana mkono mbaya na akaamini hivyo huyo maendeleo hawezi kuyapata kamwe!
Hakuna binadamu anaengangania kujifunza jambo akashindwa kulijua, tunaweza kutofautiana spidi ya kuelewa jambo tunapojifunza lakini mwisho wa siku mtu utaelewa tu, ndiyo maana tunavaa suluali, mashati na viatu kwa usahihi, kwenye vyoo vyetu vya shimo tunalenga vizuri tu, yote haya tulijifunza hatukuzaliwa tukijua yote haya na kama huamini kumbuka jinsi mtoto anavyopishanisha matundu anapoanza kufunga vifungo vya shati siku za mwanzo, au kubadili viatu mguu kulia kuvaa kushoto.
Ikitokea mtu umefanya jambo mara moja, mbili, tatu hata mara nne usifanikiwe siyo sahihi kujichukulia kwamba una nuksi au unadamu mbaya! Kama una imani juu ya jambo unalolifanya kwamba ukilimudu kulifanya linaweza kukuinua basi wewe endelea kulifanya tu maana kadri unavyoendelea kupiga mieleka ndiyo unavyozidi kulielewa vizuri zaidi mwishoni kitaeleweka tu.
Kuhusu mfano wa mpandaji wa hoho ulioutoa anaweza akawa na mkono mbaya kwa maana ya kwamba hajui kupanda hoho! Je alikuwa anapanda kwa usahihi? Ni rahisi sana kufanya utafiti ili kujua kama ni mwili wake ndiyo wenye nuksi na siyo kwamba hajui kupanda. Aende akapande sehemu tatu tofauti na watu wengine ili ionekane kama kote huko matokeo ni yale yale! Ikitokea hivyo tueleze hapa JF tumtangaze huyo Bwana maana wenzetu wa nchi zilizoendelea huyo jamaa kwao atakuwa kivutio kikubwa sana cha utalii na itabidi wampime hata damu yake waichunguze! Kwamba yeye kila akipanda hoho haziponi au hazizai au hazisitawi lol!
Kupanda miche au mbegu siyo ni kule kufukia mche kwenye udongo tu, kuna mbinu zake! Kwenye kilimo cha vitunguu na mpunga mimi mwenyewe nimewahi kukutana na baadhi ya wapandaji wangu vibarua kadhaa ambao wamewahi kunisababishia hasara kwa miche waliyopanda kufa au kutokusitawi vizuri! Hii ilitokana na wao wanapopanda wanashika miche vibaya, wanaishikia katikati ya mche na kuizamisha hivyo hivyo kwenye udongo na inajikunja kama herufi ya U, yaani majani na mizizi inatokeza juu, shina ndiyo linazamishwa chini! Yaani mche unapandikizwa lakini ukiutazama unakuta mizizi yote imetokeza juu ya udongo! Mpandaji huyo unakuta ile strip aliyopanda yeye ama miche inakufa au inakuwa dhaifu tofauti kabisa na walikopanda wengine! Mpandaji huyu akisakamwa kuwa akipanda miche inakufa au haizai vizuri atajiona ana mkono mbaya! Kuna mifano mingi tu ya aina hii ambapo watu kwa kuwa makini wengine wanafanikiwa na kuitwa wana ngekewa au damu nzuri na wengine kwa kutokuwa makini hawafanikiwi na wanaonekana wana damu mbaya au nuksi!
Kwa hiyo Mkuu chama2chawa kujibu hoja yako kuwepo ngekewa au kutokuwepo ngekewa kwenye eneo lolote la maisha inategemea wewe ni mtu wa mlengo gani! Watu walioelimika hilo wala siyo suala la kujadili kabisa!
Kuna jambo moja tu kwa uhakika kabisa ambalo lipo nalo linaitwa CHANCING hilo kwa hakika lipo! Kwa mfano ugonjwa wa kuku unaweza kukumba eneo fulani tu eneo lingine kuku wakasalimika; mvua inaweza kunyesha eneo fulani watu wakaokoa mazao na eneo lingine isinyeshe yakakauka; mtu anaweza kuuza hoho sokoni leo, kesho yake jirani yake akaingiza mzigo sokoni akakuta bei imeshuka au imepanda, unaweza kununua chanjo imekufa bila kujua kuku wako wakaugua na kufa jirani yako akaenda nunua kwingine chanjo nzima akatibu kuku wake wakabaki salama n.k. Lakini wataalamu wanasema kuwa kunachochangia sana kwenye mafanikio ya shughuri mbalimbali asilimia 5% ni CHANCING, na 95% inatokana na Management! Kwa hiyo iwapo kama chancing ni NGEKEWA (au NUKSI) mchango wake kwenye kufanikiwa ni asilimia 5% tu si kitu cha kutegemea wala si kitu cha kuhofia.
Kwanza kabisa napenda nikupongeze kwa kuchukua uamuzi wa kutuelimisha namna ya kufuga kuku kwa lengo la kuongeza tija, nilitamani sana kupata mwongozo wa namna gani nifuge kwa muda mfupi nikawa na idadi kubwa ya kuku, kwa mwongozo huu nimeanza kupata picha kamili kuwa ipo siku n'takuwa 'millionaire'. Ombi langu kwako nikwamba kama inawezekana, naomba kila 'EPISODE' unipatie maelekezo kwenye E-mail yangu( lukubayunge@gmail.com) kisha n'takuwanakupa mrejesho wa mafanikio. Kila la kheri
Kweli wewe ni mwalimu, nimenufaika nawewe Kubota. Ubarikiwe sana
Wadau hadithi yangu bado inaendelea, sijasimulia bado kuhusu ujenzi wa mabanda yangu na mpangilio wake ulivyokuwa, nitakuja pia na kitu kinaitwa grazing pattern. Kwa wanaotaka kufuga maeneo makubwa ufugaji huria, kwa wale watakaopata nguvu na kujipanua kufuga maeneo makubwa kuku kuanzia miatano na hadi zaidi ya alfu moja, kuna design inakuja. Hakuna haja ya kukata tamaaa, Tanzania yetu fursa zipo nyingi sana tatizo fursa ya kupata elimu hii ndiyo finyu, tumieni JF hapa ni zaidi ya chuo. Ninakuja kivingine. Hata nikichelewa maana nimeanzisha tena kuchoma mikaaaa, STAY TUNED..................!!!!!
Mungu akubariki Mama Joe! Bado kuna watu wema katika Taif Letu! Idumu Jamii Forums!
Ni kweli unachozungumza lakini nilichokua natoa hapo ni kama dira tu jinsi kuku wanavyoweza kuwa mtaji muhimu. Ujenzi wa banda na mahitaji mengine yanategemea na mahali ulipo, Mtu aliye kijijini au mwenye shamba ana nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.jambo muhimu kuhusu gharama za kujenga banda linategemea zaidi na changamoto za mahali ulipo. Mfano Mtu wa Dar atatakiwa kujenga banda ambalo licha ya kuwaweka kuku katika hali nzuri pia atatakiwa aangalie jinsi ya kuwalinda kuku hao na wezi. Wako ambao watakabiliwa na changamoto za mwewe na kadhalika. Mwisho nimetoa ushauri watu wafanye utafiti zaidi kwani mimi naweza kueleza lakini nikawapoteza kulingana na utofauti wa jiografia ya mahali niliko.
Wadau hadithi yangu bado inaendelea, sijasimulia bado kuhusu ujenzi wa mabanda yangu na mpangilio wake ulivyokuwa, nitakuja pia na kitu kinaitwa grazing pattern. Kwa wanaotaka kufuga maeneo makubwa ufugaji huria, kwa wale watakaopata nguvu na kujipanua kufuga maeneo makubwa kuku kuanzia miatano na hadi zaidi ya alfu moja, kuna design inakuja. Hakuna haja ya kukata tamaaa, Tanzania yetu fursa zipo nyingi sana tatizo fursa ya kupata elimu hii ndiyo finyu, tumieni JF hapa ni zaidi ya chuo. Ninakuja kivingine. Hata nikichelewa maana nimeanzisha tena kuchoma mikaaaa, STAY TUNED..................!!!!!