Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

I like the coloured part....well said well thought

 
Mama Joe mambo vipi?

Mnaweza ona nawatenga ila hakika cjawatenga hata kidogo jamani. Ni mambo yameingiliana tu na kunifanya kuwa busy muda mwingi na unajua jukwaa letu lilivyokuwa makini. Ila hakika nitarudi hapa soon kwn mambo yamesogea na yametulia tuli.

Copy kwa;
Kubota
Mama timmy
mito
asigwa

Na wote wale wa jukwaa lengwa!

Karibu ndugu mie nimejifunzia hapa mengi. Ni kweli 600 na aliuza wote nilipoenda baada ya mwezi nilikuta wameisha. Uzuri wa hawa huna pressure kama broiler maana huku unauza kuku huku unaokota mayai. Wateja wakiishakujua huna haja kuwafata.
 
Last edited by a moderator:

karibu tena mkuu, tumemis uzoefu wako
 
Nimefurahi sana kukusikia hapa darasani.miminiko katika maandalizi ya kufuga chotara baada ya kutiwa moyo na mama joe!hakika jf ni darasa tosha.
 
Mambo safi mkuu, salaam. Tunashukuru umetukumbuka maana ulipotea sana. Sisi tupo tunashukuru Mungu.
 
Waaoooo Mama Timmy karibu sana, mie pia kwa michango yenu najaribu kutanuka niwe kienyeji zaidi nitajifunza mengi kwenu.
Ahsante sana rafiki yangu mama joe!twende pamoja , na tuweke uthubutu kwenye ufugaji wetu na tutafika pale tunapopatamani.wao wameweze wana nini hata sisi tushindwe?
 
samahani mkuu nimefatilia hii thread muda mrefu , vishingo ni kuku wa aina gani au nitawatambuaje nami niweze kuwafuga
 
Asante dear tukipambana tunaweza tu twende mdogodogo tutafika tu. Barikiwa sana.
Ahsante sana rafiki yangu mama joe!twende pamoja , na tuweke uthubutu kwenye ufugaji wetu na tutafika pale tunapopatamani.wao wameweze wana nini hata sisi tushindwe?
 
Nimefurahi sana kukusikia hapa darasani.miminiko katika maandalizi ya kufuga chotara baada ya kutiwa moyo na mama joe!hakika jf ni darasa tosha.

Ndugu wana-jamvi,
michango yenu imekua taa kwa miradi yetu ya ufugaji kuku wa kienyeji.
Kwa kipindi sasa nimekua nikiliangalia kwa karibu kundi la kuku <40. Kwa nia ya kupata picha ya KIBIASHARA.
Kwa upeo wangu, kufanya ufugaji huu unafaida kiasi kwa mazingira ya mjini, faida inaweza kuongezeka iwapo
¡. Tutaweza kupunguza vifo vya vifaranga kufikia <10%
¡¡. Tutaweza kupunguza muda wa kuku kufikia uzito wa soko (miezi 6 ni mingi).
¡¡¡. Tutaweza kuongeza uwezo wa kuku kubadilisha chakula kua nyama na si mafuta.
iv. Tutaweza kupunguza uwezo wa kuatamia.
Kwa ufupi, macho nayaelekeza walipo chotara nafikiri [kwakua sijawahi kuwafuga] wanaweza kuleta majibu, kwenye baadhi ya maswali, na njia bora za ufugaji kwa yanayobaki.
Haya ni machache niliyoyapata kwa kuangalia kundi la kuku wa kienyeji niliobahatika kuwa nao.
Kwakua si mtaalamu wa kuku nitafurahi kupata picha ya KIBIASHARA kwa mazingira ya mjini, toka kwa wana-jamvi, kama wataalamu au wazoefu kwenye kada.
Wasalaam.
 
mkuu pleo hapo n0.3 unamaanisha nini, sijapaelewa vizuri
 
Last edited by a moderator:
mkuu pleo hapo n0.3 unamaanisha nini, sijapaelewa vizuri

ndugu Mito,
naomba nijaribu kwa mfano mwepesi. Ukiweka kuku wa chotara/wanyama na wakienyeji, katika mazingira ya kufungiwa, wa awali watajenga misuli na nyama kwa % (kwa kulinganisha na mafuta mwilini) kubwa ukilinganisha na wa kienyeji. Hivyo chakula, muda (rasilimali).... vitakua vinatumika chini ya kiwango, hivyo kupelekea kupunguza faida kwa kuweka wa kienyeji katika mazingira ya kufungiwa.
 
Last edited by a moderator:

nashukuru sasa nimekuelewa vizuri
 
Wakuu woote,

Mtanisamehe kwa kupotea siku mbili tatu hapa jamvini, majukumu tu yanabana..

Juzi nilibahatika kumtembelea mama mmoja ni mfugaji wa kuku wa kienyeji na chotara maeneo fulani nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, na yeye anafuga kibiashara ila kitaalamu kidogo maana amekwenda shule na ni mtafiti sana.

Yeye alianza kama Kubota kwa kuatamisha kuku watagaji ili kupata vifaranga kwani mwanzoni hakuwa na mashine ya kutotoreshea na alikua anatumia JELA kama ya Kubota, ila kuna kitu anakifanya zaidi ya hapo.

Anadai alipogundua kuku fulani ni watagaji wazuri aliwatenga na kuwapa alama maalumu, na alikua hawaruhusu kabisa kuatamia mayai, alikua na JELA MBILI. Moja kwa ajili ya kumfungia kuku anapotoka kutaga ili asahau kuatamia lakini ya pili ni kwa ajili ya kupandishia hawa kuku machachari kwa kutaga kwa kutumia majogoo machachari wa kupanda.

Kipindi amabacho kuku wanakuwa wamefikisha idadi ya mayai kadhaa mabayo yeye anayataka, huwakamata majogoo wake machachari na kuwafungia kwenye JELA YA PILI huku akiwapa chakula na maji bila kuruhusu jike yeyote kuingia humo ndani, Anadai majogoo nao wako kama binadamu tu, wakikaa siku nyingi wenyewe bila kuona majike wanapandisha sana ashiki ya kupanda majike.

Pindi yale majike yaliyokua yanataga yanapoondolewa kwenye JELA YA KWANZA basi huingizwa kwenye JELA YA PILI ambapo kuna MAJOGOO YENYE ASHIKI ZAO yanakua yanawasubiri, na hapo ndipo utajua kuwa ZINAA NI MCHEZO HATARI.
Anadai majogoo hupanda yale majike usiku na mchana kama hayana akili nzuri huku majike yakiwa hayana uhuru wa kukimbia kimbia maana eneo limebanwa.

Faida yake ni kuwa kuku anapotaga mayai baada ya kutoka kwenye jela karibu mayai yoote yanakua na mbegu yaani mayai viza ni kidogo mno na hutokea kwa bahati mbaya sana, Mayai yanayopatikana kwa staili hii ukiyaatamisha kwa kuku wengine au kwenye mashine ya kuangulia vifaranga, basi una uhakika wa kupata vifaranga zaidi ya 95% kwa mayai uliyoatamishia/kutotoresha,

Nitaleta tena hapa baadhi ya mambo kadri nitakavyokua nayanyaka katika pita pita zangu.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu wote,

Nimeamua kuwaletea tiba za asili kwa kuku wa kienyeji hasa kutokana na uzoefu wa wafugaji wa vijijini, kama mnavyojua ufugaji kwa kutumia madawa ya madukani ni gharama sana hasa ukiwa na kundi kubwa.

Nitaanza na ugonjwa wa KIDERI (Newcastle desease).

Hapa mimea mikuu mitatu hutumika sana ambayo ni ALOE VERA, KATANI , MWAROBAINI


  • unachukua KATANI MBICHI(ie ya kijani ambayo haijakauka) unatwanga kwenye kinu, maji au ule uji uji wake unaukusanya, unaweka kwenye vyombo safi na unaongeza maji kiasi ili kupata mchanganyiko mzuri, Kwa kuwa ni dawa ya kienyeji haina kipimo maalumu sana, ila unatakiwa ukadirie isiwe kali sana wala isiwe nyepesi sana, cha msingi lile povu povu lake lisipotee, dawa hii ni kinga nzuri sana kwa KIDERI(New Castle). Wape kuku kwenye maji yao ya kunywa angalau kila mwezi SIKU TATU au SIKU NNE mfululizo na ni kwa umri wowote ila wasiwe vifaranga wadogo sana.
  • Kama huna KATANI unaweza kutumia ALOEVERA, chukua aloe vera twanga na changanya na maji kidogo ili isiwe kali sana na pia zingatia isiwe nyepesi sana kisha wape hiyo juisi kama maji ya kunywa. Baada ya hapo unakaa kama wiki mbili au tatu unawapa muarobaini.. Lakini hii ni kinga tu sio tiba na haina madhara, ila wakiumwa inabidi ufuata ushauri wa daktari wa mifugo.

ugonjwa wa KUHARA(jina la kizungu nimelikosa)

Kama kuku wako wanaonesha wana ugonjwa wa kuhara na ukajaribu dawa za Madukani na zikashindwa kufua dafu, au wanahara na hujui ni ugonjwa gani kwani kuhara kunaambatana na magojwa chungu nzima, basi dawa hapa ni MAJANI YA MPERA.
  • Twanga majani ya MPERA AMBAYO HAYAJAKAUKA na ile juisi yake wawekee kwenye maji, ila kama unataka ifanye kazi vizuri changanya na MUAROBAINI na ALOE VERA, kuku wako watafunga kuhara mara moja na haina madhara yoyote kwani kuku hupenda sana kula majani. Unaweza kuwapa siku nyingi kadiri utakavyo ila ni vizuri ikawa siku tano mfululizo kwa mwezi mmoja.

Note kitu kimoja,
Siku zote madaktari wa mifugo na wanyama wanafurahi sana wakikuta umepanda ALOE VERA, MUAROBAINI na KATANI kwani wanatambua umuhimu wake.
Lakini pia kumbuka kama ilivyo kwa Binadamu usipende kuwapa kuku dozi za hospitali na za kienyeji kwa wakati mmoja, unawageuza miili yao kuwa CHEMISTRY LABOLATORY na kufanya CHEMICAL REACTIONS. Kama umeamua kuwapa dawa za madukani sitisha za kienyeji mpaka watakapo maliza za madukani, kama umeamua kuwapa za kienyeji vivyo hivyo sitisha za madukani.

Nitaendelea na magonjwa mengine na tiba zake mbadala kadri ninavyozidi kuzinyaka.
 
Mkuu Asigwa hii umeleta hapa ni funga mwaka !!! Naandika kwa shida sana kufuta machozi na mafua yanatiririka, mbavu zinaniuma sana umezivunja zote, wewe ni kiboko? Mkuu ufundishaji wa somo kwa mtindo huu somo linakamata kabisa. Nakupongeza sana kwa safari yako hiyo na ulivyo mkarimu kushea maarifa makubwa hayo. Hakika maboresho ya JELA ni makubwa kupindukia. Huyo mama anatisha ni mbunifu hasa. Asigwa hiyo JELA ya pili itafutie jina Mkuu, au tuiite jela ya mapenzi ha ha haaaa!! Asante sana huo utaalamu nimeudaka imefika penyewe ni kutumia tu huo utaalamu ili kupunguza mayai viza na kuhakikisha vijogoo uchwara hawagusi watagaji bora.
 

Mkuu hata mie nilipoona hii kitu nilishangaa sana,

Itabidi tuiite JELA YA WAPENDANAO tu au wasemaje???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…