Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Mkuu nilisahau kukuuliza iwapo unasababu maalumu kuwaacha vifaranga kwenye mashine siku 3 baada ya kutotolewa! Nadhani siku tatu bila chakula nazo ni nyingi, pamoja na kuwa kifaranga huweza kuhimili kuishi muda mrefu baada ya kutotolewa lakini hakuna sababu kuwaweka muda wote huo wa siku tatu bila kula wala kunywa. Pengine utakuwa na uzoefu fulani ulijifunza mahali tusaidiane kwa hilo maana hapa tunabadilishana uzoefu na maarifa, ni kutoa na kupokea, kwa nini unawaacha siku 3 ndani ya mashine, naomba nijifunze na mimi ndiyo nasikia kwa mara ya kwanza. Glucose mara nyingi hupewa vifaranga wanaonunuliwa na kusafirishwa mbali maana hufika wamechoka sana, katika kubana matumizi sioni kama ni ya muhimu sana kwa vifaranga wako. Hii mbinu yako hai-work maana mwenyewe unaona vifaranga wanavyokufa kwa wingi. Na wengine watajazia.
 
Kubota
Niliwapa chanjo ya Newcastle. Miguu haina nguvu na wanajisaidia kijani nadhani ni mdondo/Kideri.
Pia niliwapa Antibotics.
Kubota ulinivutia hatua ulizopitia nashukuru sana kwa bandiko lako limekuwa msaada wa mimi kufuga. Pamoja na kupoteza kuku wengi bado sijakata tamaa.
 
Last edited by a moderator:
Poa Mkuu. Jitahidi kuelewa chanzo cha vifo na ufanye maboresho, utaona mafanikio, mwishowe vifo vitapungua sana na haitakuwa kero tena. Usikate tamaa, endelea kujifunza ni sawa na anjifunzae kuendesha baiskeli kudondoka mwanzoni ni lazima. Kuku wanafaida sana ukishafaulu jinsi ya kuwakuza kwa wingi.
 

Kule niliponunua mashine waliniambia niwaache siku 3 kwa kuwapa maganda ya mayai maana yanacalcium ndo maana huwa siwatoi .
Mkuu nikiwapa hiyo stata food kwa wk 6 tatizo litaisha maana maana wengine baada ya miez 2 au 1 na nusu huwa mbawa zao zinashuka ni kama wamevaa koti tatizo ni nini?
Asante kwa kunitia moyo
 
Mkuu Pumba na dagaa siyo lishe iliyokamilika kwa vifaranga na hata kwa kuku waliofungwa ndani full time. Pumba zingine huwa hazina chenga kabisa ni kama manailoni tu. Ni maganda matupu yasiyokuwa na lishe. Ni kuwalisha kuku kwa imani tu kuwa wamekula lakini thamani ya lishe haimo! Nimekusisitizia kuwa lisha hao vifaranga kwa starter marsh hadi wafikie kuwa vinyoya ifikapo wiki 4 hadi 6! Wewe kwenye maelezo yako umeeleza huwa unawalisha starta marsh kwa wiki 2 kisha unawapa mchanganyiko wa dagaa na pumba, nakushauri tena soma thread hii kuhusu lishe na udhibiti wa magonjwa. Hayo makoti yanachangiwa na magonjwa nyemelezi shauri ya LISHE DUNI! Wewe usiende mbali kutafuta chanzo cha makoti na vifo, rekebisha lishe kwanza ndiyo uone kama kuna lingine! Zingatia chanjo na madawa ya matumbo. Kuhusu kuweka vifaranga siku 3 ili wale maganda ya mayai kwa vile yana Calcium hii ni mbinu mpya kabisa na ndiyo neema ya hapa JF! Mkuu Chasha na wadau wengine mtakaobahatika kusoma post hii mnasemaje juu ya mbinu hii ya kuacha vifaranga siku 3 kwa matarajio ya kuku kula maganda. Haiwezi kuwa source ya maradhi pia?
 
Ganda la mayai ni chanzo cha madini karibia sawa na ya chokaa, yanaimarisha mifupa, inabidi yapitishwe kwenye joto la kutosha ili kuua bakteria kabla ya kupewa kuku. Binafsi Vifaranga navitoa mara tu vinapo kauka na kustamili kusimama mara nyingi inakua ndani ya masaa 48
 

Mkuu hiyo ya vifaranga kula maganda yake ndo naisikia, leo nijuavyo vifaranga siku ya kwanzana ya pili nzima huwa hawawezi kula chochote zaidi ya kujifunza na my be kunya maji, na yale magand si yanakwa magumu sana na waawza vipi kudonoa?

Ila maganda ya mayai vile vile yanatumika kutengeeza chakula cha kuku io haina ubishi ila hiyo ya vifaranga kuyala sijui.

Na vifarana siku 3 kwenye mashine ni kuwaumiza sana labda kuwe na sababu yamsingi, ila hatchery nyingi hutoa wakiwa na siku moja tu kwaajil ya kupata chanjo ya Mareks, hii chanjo shariti kifaranga iwe na siku moja
 
Mdau wa vifaranga aliyekushauri siku 3 amekosea, huwa wanaachwa kwa ajili ya joto kuwasaidia kukauka ubichi basi nayo ni masaa tu. Kuhusu chakula ni kama walivyokushauri hapo juu wiki ya pili bado wadogo kuanza kuwapa pumba tu na dagaa. Zingatia chakula na chanjo ulizoambiwa vifo vitapungua au kwisha kabisa.
 

.............
Asante sana mkuu
 
binafsi nimechagua kuanza na kuku wa kienyeji, utakaji wao ni mdogo lakini bei ya trey ya mayai ni mara mbili ya hayo ya kiaina.
 
Cheki hiyo imeisha leo - nimefunga mahesabu yangu ya mwezi huu.

nimeangalia ufungaji wa hesabu wako sijui kama kuna uhalisia kweli. Kwa wataalam ambao wameishafuga nawaombeni mpitie then mtoe comments zenu
 
Mkuu mara nying baada ya wiki mbili hiyo hali huwa inajitokeza, na kuku mama zao huwa nachukua mayai ya mama zao kwa ajili ya kutotoleshea vifaranga.asante
Mkuu kwa maelezo yako naona huo ugonjwa na vifo vya vifaranga vyako huwa vinajitokeza baada ya wiki mbili yaani mara tu unapoacha kuwalisha starter na kuanza kuwpa pumba na dagaaa..hii ndio chanzo cha tatizo lako

Tatizo lako si ugonjwa ni lishe kwani starter mara nyingi inakuwa na virutubisho vyoote kitaalamu kwa ajili ya vifaranga na wafugaji hushauriwa kuwalisha vifaranga mpaka wakianza kutoka manyoya ie wiki nne mpaka sita hivi kwani vifaranga visivyokuwa na mama mara zote huwasi vijanja sana kujitafutia chakula yaani vimezubaa...

Inaonekana vifaranga vyako vinakosa madini ya calcium ambayo hutumika kuimarisha mifupa na kinachotokea kwa kuwa vyakula unavyowapa havina hayo madini basi miili ya hao vifaranga huanza kuifyonza kutoka kwenye mifupa yao wenyewe na hasa miguuni ndio maana vifaranga vinakosa nguvu miguuni...

Una option mbili
1)Kuendelea kuwalisha kwa starter mpaka watakapo kuwa na wiki 4 au sita

2)Kuwanunulia chokaa ya mifugo toka kwenye maduka ya mifugo (siyo chokaa ile ya kupaka kwenye nyumba ha ha ha) Ukiwaeleza tu wataalamu wa mifugo anaelewa hii mambo au nunua premix halafu changanya kwenye hizo pumba na dagaa wako halafu watupie na majani hasa ya mimea jamii ya mikunde au yale yanayochipua yaani malaini mambo yatakaa sawa...
 
Hakika sipo kimya ndugu zangu akina Kubota na wengine hakika naendelea vizuri nilianza na kuku 12 leo hii ukijumlisha na vifaranga nina kuku mia na kumi 110. Maendeleo ni mazuri na ninajipa moja kuanzisha shamba kubwa la ufugaji kuku. Ninawapa moyo wafugaji wanaoanza kufuga cha muhimu ni kuwa mvumilivu na kusoma humu ndani kuna kila kitu ambacho kitakufanya ufanikiwe katika ufugaji. Ni wazi hakuna raha kama kufuga muda wote unawaza mifugo yako na hapo unajua magonjwa vyakula hata milio ya kuku.
 

Hongera sana.
 

Mkuu nimefuata ushauri wako na nimenunua starta ya kutosha kwa hawa ninaowatotolesha nitatoa ushuhuda hapa kwa maendeleo zaid. Maana mwisho wa mwez watapatikana vifaranga wengi zaid.
 
Mkuu nimefuata ushauri wako na nimenunua starta ya kutosha kwa hawa ninaowatotolesha nitatoa ushuhuda hapa kwa maendeleo zaid. Maana mwisho wa mwez watapatikana vifaranga wengi zaid.
Haina neno mkuu tuko pamoja.....
 
Safi sana mkuu,

Haya ndiyo mambo tunataka kusikia. Hongera sana kwa uthubutu wako
 
Nimehamasika sana,ninashamba kama heka kumi Nataka nifuge kuku hawa wakienyeji ntaanza na kuku majike 50 majogoo 5 ,kwa kufuata maelekezo nloyapata huku,ntatoa marejesho baada ya miezi 6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…