Mkuu nilisahau kukuuliza iwapo unasababu maalumu kuwaacha vifaranga kwenye mashine siku 3 baada ya kutotolewa! Nadhani siku tatu bil
a chakula nazo ni nyingi, pamoja na kuwa kifaranga huweza kuhimili kuishi muda mrefu baada ya kutotolewa lakini hakuna sababu kuwaweka muda wote huo wa siku tatu bila kula wala kunywa. Pengine utakuwa na uzoefu fulani ulijifunza mahali tusaidiane kwa hilo maana hapa tunabadilishana uzoefu na maarifa, ni kutoa na kupokea, kwa nini unawaacha siku 3 ndani ya mashine, naomba nijifunze na mimi ndiyo nasikia kwa mara ya kwanza. Glucose mara nyingi hupewa vifaranga wanaonunuliwa na kusafirishwa mbali maana hufika wamechoka sana, katika kubana matumizi sioni kama ni ya muhimu sana kwa vifaranga wako. Hii mbinu yako hai-work maana mwenyewe unaona vifaranga wanavyokufa kwa wingi. Na wengine watajazia.