Kitabu bora cha ufugaji wa kuku wa kienyeji kinapatikana kwangu 0758303090
Mimi ninahitaji MASHINE ya kutotolesha vifaranga 200 Ya mafuta name umeme 0767448447Ni nani anahitaji majogoo chotara ya miezi miwili kwa bei nafuu?tuwasiliane kwa no:0755155782
Nimeumwa na kichwa ghafla....umaskini ni kujitakia tu...heko sana mkuu....
Mkuu hebu tuma hiyo database...so impressed by your set up
Nimerudi wakuu,
Sikuwa na access ya mtandao,
baada ya kurudi bongo ninaishi mbugani mtandao hakuna,
nikienda mjini sikupata nafasi kuingia internet Cafe!!
Lakini ivi sasa problem is solved !!!
Mama Joel, ninafuga Vyotara, sirudi nyuma kwenye pure kienyeji, wanakua kwa spidi sana,
Mama Timmy, Asigwa, Liverpool FC, wachangiaji wote na wasomaji wetu,
nimefurahi kukuta Thread haijapelekwa Archive !!
Nyote nawapenda sana, tuendelee kujuzana!
Mm naomba ushauri ,nimenunua kuku wa mayai 26 size ya miezi mitatu cha kushangaza nimewaweka ktk chumba ambacho muna godoro ukutani leo nimeamka wamelitoboatoboa wanakula je hakuna madhara yeyote?
wakuu pia kuna website hii :Cheap Nike Free Run Online - Nike Air Max Wholesale Australia au Home ina mabo mengi sana kuhusu ufugaji wa kuku na wanyama wengineo unaweza download vitabu vyao buree pdf format!!!!
Mkuu kuku wako anavimba usoni kwa kukosa madini ya vitamini A. Tiba ya dharura ni kuwapaka mafuta ya alizeti kama ilivyokwishaelezwa humu, lakini kwa long run solution tafuta vyakula vyenye wingi wa madini ya vitamini A ambavyo vingi ni majani jamii ya mikunde kunde, au majani laini mapana yanayopendwa na kuku. Lakini pia kama unapata muda tafuta majani ya mlonge longe uwachanganyie kwenye chakula chao ni tiba murua sana, utasahau hili tatizo foreverKubota, Tutor B, Mama Joe, Zipuwawa na wadau wa uzi huu wa ufugaji kuku wa kienyeji, uzi huu ulinishawishi kuanza ufugaji. Nilianza na kuku watatu kwa majaribio, jogoo 1, matetea 2. Baadae nikaongeza jogoo 2 na matetea 9. Hivi sasa nina kuku 32 wakubwa, 16 umri wa miezi 3, 16 umri wa miezi 2, 25 umri wa mwezi 1 na vifaranga 12 vya umri wa siku 5.
Sasa kuna ugonjwa umekamata kuku 2 wa umri wa miezi miwili ambao sijajua kama ni ndui au coryza au uvimbe tu. Naomba msaada wa mawazo tafadhali kwamba huu ni ugonjwa gani na niukabili vipi kabla sijaenda kumwona doctor wa mifugo. Picha inayoonyesha ugonjwa wa mmoja wa kuku hao nimei-attach. Asanteni sana.