Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ni check Kwa vitabu vya ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyeji
 
Nauza kuku wa kienyeji majogoo 20000 makubwa na majike kuanzia 12000 na mayai yao trei moja ni 15000
 
salaam greathinkers!

sasa nimeamua kuacha woga, na nataka kuanza kufuga kuku wa kienyeji rasmi. Kwa sasa najenga banda litakamilika next saturday (26/4), kwa kuanzia banda langu lina ukubwa wa mita 25 kwa 11.

Je kwa ukubwa huo naweza kufuga mpaka kuku wangapi wa kienyeji?
 
Kitabu bora cha ufugaji wa kuku wa kienyeji kinapatikana kwangu 0758303090
 
Nimerudi wakuu,
Sikuwa na access ya mtandao,
baada ya kurudi bongo ninaishi mbugani mtandao hakuna,
nikienda mjini sikupata nafasi kuingia internet Cafe!!
Lakini ivi sasa problem is solved !!!
Mama Joel, ninafuga Vyotara, sirudi nyuma kwenye pure kienyeji, wanakua kwa spidi sana,
Mama Timmy, Asigwa, Liverpool FC, wachangiaji wote na wasomaji wetu,
nimefurahi kukuta Thread haijapelekwa Archive !!
Nyote nawapenda sana, tuendelee kujuzana!

Tupo pamoja sana mkuu

Nafikiria kuanza kufuga kuku wa kienyeji kwa large scale pale Rufiji huku niki-intergrate na ufugaji samaki japo bado nakusanya ushauri wa ufugaji wa samaki , maana seems utaalamu wa tilapia aquaculture kwa hapa Bongo bado ni kidogo na watu wanafuga kimazoea sana.

Vipi mkuu kulikoni kukimbia kuku wa kienyeji na kuhamia kwenye chotara??

Mie wa kienyeji siwaachi maana ni wavumilivu mno na watanifaa sana kama nitafanikiwa kuwaunganisha na mabwawa ya samaki
 
Mm naomba ushauri ,nimenunua kuku wa mayai 26 size ya miezi mitatu cha kushangaza nimewaweka ktk chumba ambacho muna godoro ukutani leo nimeamka wamelitoboatoboa wanakula je hakuna madhara yeyote?

Mkuu hao kuku unawalisha chakula cha kutengeneza mwenyewe au ni cha kununua??

Kama ni cha kutengeneza hakikicha unaweka na madini ya chokaa ya wanyama(ni tofauti na chokaa ya kupaka nyumba), ukienda duka lolote la mifugo watakupa hii kitu.

Kama ukishidwa kabisa , wachanganyie majani ya mlongelonge yaliyokaushwa bila kuanikwa juani i.e yaliyokaushwa kivulini, tatizo lako litaisha kabisa
 
Kubota, Tutor B, Mama Joe, Zipuwawa na wadau wa uzi huu wa ufugaji kuku wa kienyeji, uzi huu ulinishawishi kuanza ufugaji. Nilianza na kuku watatu kwa majaribio, jogoo 1, matetea 2. Baadae nikaongeza jogoo 2 na matetea 9. Hivi sasa nina kuku 32 wakubwa, 16 umri wa miezi 3, 16 umri wa miezi 2, 25 umri wa mwezi 1 na vifaranga 12 vya umri wa siku 5.

Sasa kuna ugonjwa umekamata kuku 2 wa umri wa miezi miwili ambao sijajua kama ni ndui au coryza au uvimbe tu. Naomba msaada wa mawazo tafadhali kwamba huu ni ugonjwa gani na niukabili vipi kabla sijaenda kumwona doctor wa mifugo. Picha inayoonyesha ugonjwa wa mmoja wa kuku hao nimei-attach. Asanteni sana.
Mkuu kuku wako anavimba usoni kwa kukosa madini ya vitamini A. Tiba ya dharura ni kuwapaka mafuta ya alizeti kama ilivyokwishaelezwa humu, lakini kwa long run solution tafuta vyakula vyenye wingi wa madini ya vitamini A ambavyo vingi ni majani jamii ya mikunde kunde, au majani laini mapana yanayopendwa na kuku. Lakini pia kama unapata muda tafuta majani ya mlonge longe uwachanganyie kwenye chakula chao ni tiba murua sana, utasahau hili tatizo forever
 
mradi wa ufugaji kuku ni mzuri nina kuku wa kienyeji 11 ambao nafuga tu kwa ajili ya kula nyama ila nimevutiwa kuwafuga kibiashara baada ya kusoma uzi huu hata ivyo changamoto kubwa kuliko zote ni wizi juzi jirani yangu kaibiwa kuku 61.
 
Hivi mkuu wale wadudu wanaokula mayai mfano .vicheche au kenge dawa yao ni nini maana wamenitia hasara sana mayai km ishirini waliyala yote karibu wiki waweze kuangua iliniuma sana
 
MI nimeanza na kuku 11 jike 10 dume moja mwezi sasa umeisha,
wamekufa wawili kwa ugojwa na mmoja kaliwa na mbwa.
wamebaki 8 mmoja tu ndio anataga.
 
Back
Top Bottom