Mkuu Marire pole ila usikate tamaa, kuna wenzio wananunua wanakufa banda zima hata alfu, songa mbele. Kuhusu kutaga umri wamefikia? Ulikowatoa kama walifikia muda wa kulalia watasimama kidogo. Vipi chakula chao? Pia kama wote waliumwa hasa mafua hukata kutaga kwa muda hivyo imarisha afya zao kwa lishe kwanza.
Mama Joe umenikumbusha juzikati hapa. Nilinunua mayai 90 ya "austrolorp" ili kuwatotolesha kwa kuku wangu. Loooooo!, mayai 36 yakapasuka, yaliyobaki nikajipa moyo kuatamisha. Heee! kumbe nayo yalishakuwa disturbed. Nimeambulia patupu. Hata hivyo, nimechukua mengine tena. Hakuna kukata tamaa.
Hongera kwa kudhamiria, kwakweli maisha ukianguka unainuka haraka na kuendelea. Kikubwa kagua wapi ulijikwaa na rekebisha. All the best
Inaweza kuwa ndui. Nunua dawa fanya usafi wa banda
Nauza kuku wa mayai..wanataga sasa mwezi wa 5..wako kama 600..bei ni 8500 kwa 1...Karibuni
Mama Joe nina kuku wa kienyeji 30 ambao wameanza kutaga mayai. Wiki moja iliyopita walipata chanjo ya Newcastle ambayo wamekuwa wakiipata kila baada ya miezi 3 tangu wakiwa wadogo.
Jana baadhi yao (4) wameanza kusinzia na kuharisha kijani na nyeupe, na nikiwashika wana joto kali.
Unaweza kuwa ni ugonjwa gani na naweza kuwapa dawa gani?
Msaada tafadhali
| UMRI | BEI |
| SIKU MOJA | 1,800/= |
| MWEZI MMOJA | 2,500/= |
| MIEZI MIWILI | 5,000/= |
| MIEZI MITATU | 7,500/= |
| MIEZI MINNE | 10,000/= |