Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wadau nauza kuku wangu wa Mayai..wanataga sasa mwezi wa 5..wako 600 na nauza 8500 kila mmoja..karibuni
 
Nauza kuku wa mayai..wanataga sasa mwezi wa 5..wako kama 600..bei ni 8500 kwa 1...Karibuni
 
Mkuu Marire pole ila usikate tamaa, kuna wenzio wananunua wanakufa banda zima hata alfu, songa mbele. Kuhusu kutaga umri wamefikia? Ulikowatoa kama walifikia muda wa kulalia watasimama kidogo. Vipi chakula chao? Pia kama wote waliumwa hasa mafua hukata kutaga kwa muda hivyo imarisha afya zao kwa lishe kwanza.

Mama Joe umenikumbusha juzikati hapa. Nilinunua mayai 90 ya "austrolorp" ili kuwatotolesha kwa kuku wangu. Loooooo!, mayai 36 yakapasuka, yaliyobaki nikajipa moyo kuatamisha. Heee! kumbe nayo yalishakuwa disturbed. Nimeambulia patupu. Hata hivyo, nimechukua mengine tena. Hakuna kukata tamaa.
 
Hongera kwa kudhamiria, kwakweli maisha ukianguka unainuka haraka na kuendelea. Kikubwa kagua wapi ulijikwaa na rekebisha. All the best

Mama Joe nina kuku wa kienyeji 30 ambao wameanza kutaga mayai. Wiki moja iliyopita walipata chanjo ya Newcastle ambayo wamekuwa wakiipata kila baada ya miezi 3 tangu wakiwa wadogo.
Jana baadhi yao (4) wameanza kusinzia na kuharisha kijani na nyeupe, na nikiwashika wana joto kali.
Unaweza kuwa ni ugonjwa gani na naweza kuwapa dawa gani?
Msaada tafadhali
 
Duh pole sana jana sikupita uku, kijani huwa ni kideri pia, natumaini famasi wamekupa dawa? Hofu yangu umewachanja wakiwa wagonjwa, halafu ukiwapa chanjo ambazo ni kama uambukizo mdogo wa ugonjwa ili kuwajengea kinga, unapaswa kuwapa vitamin kabla na baada ili iwaimarishe kinga dhidi ya vidudu vya chanjo. Ukienda famasi waeleze dalili zote na kuhusu chanjo watakupa antibiotic kutibu hiyo homa.
Mama Joe nina kuku wa kienyeji 30 ambao wameanza kutaga mayai. Wiki moja iliyopita walipata chanjo ya Newcastle ambayo wamekuwa wakiipata kila baada ya miezi 3 tangu wakiwa wadogo.
Jana baadhi yao (4) wameanza kusinzia na kuharisha kijani na nyeupe, na nikiwashika wana joto kali.
Unaweza kuwa ni ugonjwa gani na naweza kuwapa dawa gani?
Msaada tafadhali
 
Nakushukuru Kubota na wadau wengine woote..nataraji kuwa na vifaranga mia chotara, je Mama Joe niwatenge ktk mafungu au naweza waweka wote ktk chumba kimoja, hofu yangu nimesikia kuwa wanalaliana kupelekea wengine kufa..
 
Naomba mods huu uzi wa Kubota muuweke pale juu, ukae hapo milele utakomboa wengi kwani una VITENDO ndani yake..pia aina hii ya uandishi-vitendo ipigiwe DEBE na italifanya jukwaa hili kuwa la kipekee kabisa hapa Tanganyika..aina hii ya uandishi ni FUNZO kwa wataalam wetu ambao wanakalia utaalam/tafiti mbalimbali ilihali Watanganyika tumechoka...UZI huu nimeupeleka kwa wadau huko Kintinku, Saranda, Itigi (Singida), Wilaya ya Chemba, Malongwe na Goweko-Tabora...Basi KILA mmojawetu akileta michango yake kwa namna ya KUBOTA tutawapita Wakenya na hatimaye Wachina, ndiyo hakuna mafundi wa kukopy kama Wabongo..
 
VIFARANGA WA KIENYEJI WANAUZWA
VIFARANGA BORA WA KUKU WA KIENYEJI (ASILI NA MALAWI) WANAUZWA KWA BEI NAFUU KAMA IFUATAVYO
UMRI
BEI
SIKU MOJA
1,800/=
MWEZI MMOJA
2,500/=
MIEZI MIWILI
5,000/=
MIEZI MITATU
7,500/=
MIEZI MINNE
10,000/=

SIFA ZA VIFARANGA HAWA:

  1. WANATAGA MAYAI MENGI (WASTANI WA MAYAI 5 KWA WIKI)
  2. WANAUWEZO MKUBWA WA KUSTAHIMILI MAGONJWA
  3. WAMEPEWA CHANJO DHIDI YA MAREK’S DISEASE
  4. KUKU HAWA NI WAZITO NA WANAFAA KWA NYAMA NA MAYAI
  5. WANAKUA TAYARI KWA NYAMA NDANI YA MIEZI MINNE NA NUSU TU
  6. SOKO LA MAYAI NA NYAMA YA KUKU HAWA NI KUBWA
MTEJA ATAPATA USHAURI MUDA WOTE JINSI YA KUWALEA MPAKA WANATAGA

WASILIANA NASI KWA NJIA ZIFUATAZO:
EMAIL: irpoultry2014@gmail.com
PHONE: +255685637670
TANZANIA, IRINGA, MTWIVILA, KITUO CHA KWA MSHONA VIATU
 
Wakuu tafadhali ninaombeni muongozo namna ya kuhudumia kuku wa kienyeji tangu akiwa kifaranga mpaka anapokuwa mkubwa.Hasa kwa kuanza na chanjo na zaidi ya chanjo ni dawa gani ambazo wanatakiwa wapewe ili kuepukana na maradhi ya mara kwa mara yanayo wapata kuku.
 
Kwa anayejua jinsi ya kuwafuga kuku wa kienyeji kwa style ya kisasa zaidi atueleze, lengo ni aina ya chakula (cha bei nafuu) na mchanganuo wake.
 
Fatilia kwenye watu wanao miliki migahawa na hotel, hata shule za sekondari mu- asign kijana awe anapeleka kifaa cha mabaki ya vyakula, muwezeshe, utatoka kuliko chakula cha special cha kuku wakati mwingine ratio ya kuchanganya lishe inakuwa pungufu matokeo yake wanadonoana.
 
Habari zenu wanajamvi, ama baada ya salam naomba ushauri wako wewe mwanajamvi aina na jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji na inacost kiasi gani. Ahsanteni
 
Back
Top Bottom