neggirl
JF-Expert Member
- Jul 30, 2009
- 4,849
- 2,132
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
VIFARANGA WA KIENYEJI WANAUZWA
VIFARANGA BORA WA KUKU WA KIENYEJI (ASILI NA MALAWI) WANAUZWA KWA BEI NAFUU KAMA IFUATAVYO
UMRI
BEI
SIKU MOJA
1,800/=
MWEZI MMOJA
2,500/=
MIEZI MIWILI
5,000/=
MIEZI MITATU
7,500/=
MIEZI MINNE
10,000/=
SIFA ZA VIFARANGA HAWA:
MTEJA ATAPATA USHAURI MUDA WOTE JINSI YA KUWALEA MPAKA WANATAGA
- WANATAGA MAYAI MENGI (WASTANI WA MAYAI 5 KWA WIKI)
- WANAUWEZO MKUBWA WA KUSTAHIMILI MAGONJWA
- WAMEPEWA CHANJO DHIDI YA MAREKS DISEASE
- KUKU HAWA NI WAZITO NA WANAFAA KWA NYAMA NA MAYAI
- WANAKUA TAYARI KWA NYAMA NDANI YA MIEZI MINNE NA NUSU TU
- SOKO LA MAYAI NA NYAMA YA KUKU HAWA NI KUBWA
WASILIANA NASI KWA NJIA ZIFUATAZO:
EMAIL: irpoultry2014@gmail.com
PHONE: +255685637670
TANZANIA, IRINGA, MTWIVILA, KITUO CHA KWA MSHONA VIATU
Pole sana binti mzuri neggirl. Nilikuwa busy kidogo sikuwa na muda wa kupitia notofications. Ila pia mimi nimfugaji wa kuku ila sijawahi kusafirisha toka mbali na tenga. Kuku wangu nilichukua kidogokidogo kwenye box kutoka kijijini na wengine nikanunua Dar wakazaliana na sasa wako kama 150 na zaidi kwa ajili ya kitoweo tu.
Pole sana binti mzuri
neggirl. Nilikuwa busy kidogo sikuwa na muda wa
kupitia notofications. Ila pia mimi nimfugaji wa kuku ila sijawahi
kusafirisha toka mbali na tenga. Kuku wangu nilichukua kidogokidogo
kwenye box kutoka kijijini na wengine nikanunua Dar wakazaliana na sasa
wako kama 150 na zaidi kwa ajili ya kitoweo tu.
asante Zogwale.
niliamua kuanzisha thread baada ya kuona nakawia hapa. But nashukuru nimepata mawazo ya watu tofauti na Mungu akijalia wiki hii nategemea nitawasafirisha.
by the way.. wewe wafuga 150 wote hao kwa ajili ya kitoweo? mmh!
nakubaliana na weweKuku wa kienyeji kama unawafuga kwa mtindo wa free range waweza kufuga wengi kulingana na ukubwa wa shamba lako,na hautingia gharama kubwa ya kuwalisha. Na ukitaka kuuza utauza taratibu bila shinikizo lolote
Nimeipenda sana hii thread. Wapenzi wa MMU waje wasome hii habari, waimarishe mahusiano Mallu miss neddy mrsleo vaisley
mkuu umenena kweli ubnafsi unatuuwa Watanzania hasa vijana aisee na twaishia kulalamika..mimi now ni kijana nadhan by November ntakuwa na mtaji wa almost one million anaetaka kuungana na mie npo tayari tushirikiane tondokane na umaskinKaka uliyosema ni kweli, sisi watanzania hatuna umoja na ndiyo maana production zetu ni hafifu zikiingia sokoni - mfano nilioutoa hapa ni kwamba
Wafugaji wa kuku nchini kenya wananunua Mashudu ya alzeti, Pumba za mahindi na Mahindi kutoka Tanzania - Then wanarudi kutuuzia mayai tena yenye ubora. Najiuliza je tukiingia kwenye soko huria si watatumaliza kabisa.
Mtu anaweza kusema tusiogope kuingia kwenye soko la pamoja la africa mashariki lakini ndugu zangu wakenya wapo juu sana karibu katika kila sekta. Watanzania tujifunze umoja.
Kwa mafano juzi nilimsikia mama mmoja anasema yeye anapekeka kuku ya nyama somalia na arabuni - wana soko kubwa sana huko - sasa vitu kama hivi ndivyo vya kuanzia kufanyia kazi. Mnaungana watu kama 10 ambao ni wafugaji wa kuku lets say, then mnatengeneza kitu chenye quality mnauza n'gambo.
Kwa sasa mayai mengi sana yanatoka Mombasa na yanauzwa tray kwa Tshs 5000 tena yana ubora mzuri. sisi mayai ya hapa TZ ni 5500 kwa bei ya jumla lakini mengine hayana uzito na ukubwa unaotakiwa sokoni.
Watanzania tuamuke - tusaidieane - tusipende kufanya vitu kipekee pekee - HATUFIKI POPOTE. mfano unakuta wafugaji karibia kumi na ni majirani kila mtu anafuga kuku wa nyama mia mbili, mia tatu tatu hivi - je kama hawa watu wangekuwa na umoja na kutengeneza kitu chenye ubora na kutafuta soko lenye uhakika. Inawezekana, tatizo hatuna hii culture ya kuungana.
safi, kinachotakiwa usichague nini cha kufanya, kwa mfano vijana wenye degree moja na zaidi wanaona uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na ufugaji ni kwa wazee wastaafu na kina mama wajane. hii dhana ikifutika vijana wengi watajiajiri hasa kwenye hii sekta ya kilimo na ufugaji ambayo ipo wazi kabisa katika nchi yetu.mkuu umenena kweli ubnafsi unatuuwa Watanzania hasa vijana aisee na twaishia kulalamika..mimi now ni kijana nadhan by November ntakuwa na mtaji wa almost one million anaetaka kuungana na mie npo tayari tushirikiane tondokane na umaskin
jaman mbna kaweka database hapa
Naona Mkuu ElNINO ametingwa maana hata mm nimemuomba anitumie hiyo database lakini naona hajanijibu!!! Pengine tuendelee kumsikilizia!!!
nlikuwa sijui incubator ni nini kumbe ndo mashine ya kutotolea vifaranga wa kuku ten wa kisasa .
Jamani mimi nimenunua incubator bado mpya, nimeitest kwa siku mbili hivi.
Nauliza je kuna dawa yoyote ya kuoshea mayai kabla ya kuyaweka kwenye incubator?
Na je ikitokea umeme ukakatika kwa muda wa masaa manne je mayai yataharibika?
Naomba ujuzi wandugu kesho ndio nataka weka mayai kwenye mashine, nimepata ya kuku wa malawi