Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

wapendwa
wafugaji nisaidieni ushauri nimekwama.
ni njia ipi rahisi ya kusafirisha kuku, nawatoa rombo to dsm?

wako 18, wamewekwa kwenye tenga, naona watu wa mabasi ya abiria
wanasumbua sumbua.. je kuna alternative nyingine? Your advice plz! Mama Joe chasha Kubota Zogwale na wafugaji wengine
 
Last edited by a moderator:

Unasafirisha kwa qharama zako mikoa yote? Je unaweza kuweka picha tuone
 
Pole sana binti mzuri neggirl. Nilikuwa busy kidogo sikuwa na muda wa kupitia notofications. Ila pia mimi nimfugaji wa kuku ila sijawahi kusafirisha toka mbali na tenga. Kuku wangu nilichukua kidogokidogo kwenye box kutoka kijijini na wengine nikanunua Dar wakazaliana na sasa wako kama 150 na zaidi kwa ajili ya kitoweo tu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wale wa Morogoro sasa najiandaa kuanza kuzalisha vifaranga wa kuku wa kienyeji...........nauza na mayai ya kienyeji pia
 

asante Zogwale.
niliamua kuanzisha thread baada ya kuona nakawia hapa. But nashukuru nimepata mawazo ya watu tofauti na Mungu akijalia wiki hii nategemea nitawasafirisha.

by the way.. wewe wafuga 150 wote hao kwa ajili ya kitoweo? mmh!
 
Last edited by a moderator:
asante Zogwale.
niliamua kuanzisha thread baada ya kuona nakawia hapa. But nashukuru nimepata mawazo ya watu tofauti na Mungu akijalia wiki hii nategemea nitawasafirisha.

by the way.. wewe wafuga 150 wote hao kwa ajili ya kitoweo? mmh!

Ha ha ha ni kweli ni kitoweo tu kwa kuwa sili nyama nyekundu. Hivyo kuna wakubwa na wadogo na inafika idadi hiyo. Mayai nauza kwa oda ya jumla. Na ndugu zako nao wanachukua kwenda kula kwa kuwa hawana muda wa kufuga, si mnajua tena nyie vijana. Ila wanachukua kwa market price!!! Hakuna vya bure eti.
 
Nimeipenda sana hii thread. Wapenzi wa MMU waje wasome hii habari, waimarishe mahusiano Mallu miss neddy mrsleo vaisley
 
Last edited by a moderator:
Kuku wa kienyeji kama unawafuga kwa mtindo wa free range waweza kufuga wengi kulingana na ukubwa wa shamba lako,na hautingia gharama kubwa ya kuwalisha. Na ukitaka kuuza utauza taratibu bila shinikizo lolote
nakubaliana na wewe
 
nashkuru nimepata somo kubwa sana.hii ni baada y kutafuta kaz kwa muda mrefu na kukosa.wana jf juuuuuuuuuuuu!
 
nina sh.100000 kutokana na somo lenu nataka nifuge kuku wa mayai na nyama.inawezekana kama ndio.naomba procedures kibot
 
mkuu umenena kweli ubnafsi unatuuwa Watanzania hasa vijana aisee na twaishia kulalamika..mimi now ni kijana nadhan by November ntakuwa na mtaji wa almost one million anaetaka kuungana na mie npo tayari tushirikiane tondokane na umaskin
 
mkuu umenena kweli ubnafsi unatuuwa Watanzania hasa vijana aisee na twaishia kulalamika..mimi now ni kijana nadhan by November ntakuwa na mtaji wa almost one million anaetaka kuungana na mie npo tayari tushirikiane tondokane na umaskin
safi, kinachotakiwa usichague nini cha kufanya, kwa mfano vijana wenye degree moja na zaidi wanaona uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na ufugaji ni kwa wazee wastaafu na kina mama wajane. hii dhana ikifutika vijana wengi watajiajiri hasa kwenye hii sekta ya kilimo na ufugaji ambayo ipo wazi kabisa katika nchi yetu.

Kuna msemo kijana ukianza kufunga ngombe wa waziwa au kuku - eti unajiandaa kustaafu.
 
Jamani mimi nimenunua incubator bado mpya, nimeitest kwa siku mbili hivi.
Nauliza je kuna dawa yoyote ya kuoshea mayai kabla ya kuyaweka kwenye incubator?
Na je ikitokea umeme ukakatika kwa muda wa masaa manne je mayai yataharibika?
Naomba ujuzi wandugu kesho ndio nataka weka mayai kwenye mashine, nimepata ya kuku wa malawi
 
nlikuwa sijui incubator ni nini kumbe ndo mashine ya kutotolea vifaranga wa kuku ten wa kisasa .
 
nlikuwa sijui incubator ni nini kumbe ndo mashine ya kutotolea vifaranga wa kuku ten wa kisasa .

sio wa kisasa tu hata mayai ya kuku wa kienyeji yanatotolewa na incubator pia. Halafu sio mayai ya kuku tu hata kanga, bata na ndege wengine wanaofugwa.
 

1: Kuhusu dawa ya kusafishia mayai sina uhakika kama ipo au lah. Ninachojua kwa mazingira niliyotumia hiyo incubator nilikuwa nahakikisha mayai ni masafi tu na yale machafu kiasi yalikuwa yanafutwa kwa kitambaa.
2: umeme unapokatika hakikisha joto la ndani ya incubator halishuki chini ya nyuzi joto 37 centigrade. Kama umeme umekatika chini ya masaa manne na upo sehemu za joto kama Dar unaweza kulitunza joto la ndani ya incubator na linaweza lisishuke sana na kuwa na madhara. Kwa kuwa hakuna uhakika katika umeme wetu ni muhimu kuwa na jenereta itakayoweza kusaidia la sivyo ipo siku utapata hasara.

Lingine la kuzingatia hakikisha mayai hayajakaa zaidi ya wiki 2 tangu yalipotagwa au yametunzwa vizuri.

Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…