View attachment 198146
Ee bhana ee, hilo ni banda la kukuzia vifaranga teknolojia niliyoicopy na kuipaste home kutoka maonyesho ya nanenane.
Kama inavyoonekana banda lina sehemu 2. Upande wa kulia ni banda la mduara lililosanifiwa mahsusi kwa ajili ya vifaranga kulala. Kwa nje kama linavyoonekana limezungushiwa sheet za ceiling boards na kufunikwa juu yake kwa material yaleyale. Kwa ndani limewekwa pumba za mpunga kuzunguka mzingo wote pamoja na kifuniko chake. Ilielezwa muundo huu unasaidia kuhifadhi joto linalohitajika kwa ajili ya vifaranga hivyo kuviepusha na baridi na ni mbadala wa joto ambalo vingepata kutokana na kulaliwa na mama yao.
Upande wa kushoto ni sehemu ya chakula na kunywa. Haina usipesheli wowote mwingine zaidi ya kuwa na uzio huo kuzuia vifaranga hivyo kutoroka.
Sehemu hizo mbili zinaunganishwa na mlango mdogo tu kwa ajili ya kuruhusu vifaranga kuingia na kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ilielezwa kuwa banda hili linaweza kutumika kuhifadhi vifaranga vya umri wa kuanzia siku 2 na kuendelea.
Bhana ee, nilicopy nikapaste na ndo hilo mnaloliona.
Heheee, kwani limefunction!! Kila kifaranga tuliyeweka humo hajakatiza. Limeua vifaranga wa home na wengine nilionunuanunua hapa kijijini zaidi ya 30.
Ama basi kuna step nakosea? But I bet I did it right, but why then?
Kama kuna watalaam walokuwa wakinadi teknolojia hii waseme walifake au nini, maana hii sasa hasara tupu jamani!!!