Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi kuna vifaranga vinajaa maji kichwani na kufa
Hongereni mkuu...kidogo kidogo utafika tu
Umenihamasisha aisee.
mkuu,
hao kuku ni dili sana sana, wape growers after 3 months wape layers, milo yote changanyia na pumba nyeupe ili ubudget msosi, jioni hivi waache watoke waokoteze okoteze mayai yao yawe ya kienyeji au unaweza wakatia majani mchicha etc humo humo bandani, watataga balaa.
Nitapataje hao kuku ase ninawahitaji sana, nipo arusha.
Pamoja kaka! Tujitume man! Nina target ya kuku 200 by Xmas this year! Mungu atanisaidia
Mimi kuna vifaranga vinajaa maji kichwani na kufa
Mimi kuna vifaranga vinajaa maji kichwani na kufa

nahisi ni ukosefu wa lishe bora jitaidi waweza wapa na vitamin pia
View attachment 198146
Ee bhana ee, hilo ni banda la kukuzia vifaranga teknolojia niliyoicopy na kuipaste home kutoka maonyesho ya nanenane.
Kama inavyoonekana banda lina sehemu 2. Upande wa kulia ni banda la mduara lililosanifiwa mahsusi kwa ajili ya vifaranga kulala. Kwa nje kama linavyoonekana limezungushiwa sheet za ceiling boards na kufunikwa juu yake kwa material yaleyale. Kwa ndani limewekwa pumba za mpunga kuzunguka mzingo wote pamoja na kifuniko chake. Ilielezwa muundo huu unasaidia kuhifadhi joto linalohitajika kwa ajili ya vifaranga hivyo kuviepusha na baridi na ni mbadala wa joto ambalo vingepata kutokana na kulaliwa na mama yao.
Upande wa kushoto ni sehemu ya chakula na kunywa. Haina usipesheli wowote mwingine zaidi ya kuwa na uzio huo kuzuia vifaranga hivyo kutoroka.
Sehemu hizo mbili zinaunganishwa na mlango mdogo tu kwa ajili ya kuruhusu vifaranga kuingia na kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ilielezwa kuwa banda hili linaweza kutumika kuhifadhi vifaranga vya umri wa kuanzia siku 2 na kuendelea.
Bhana ee, nilicopy nikapaste na ndo hilo mnaloliona.
Heheee, kwani limefunction!! Kila kifaranga tuliyeweka humo hajakatiza. Limeua vifaranga wa home na wengine nilionunuanunua hapa kijijini zaidi ya 30.
Ama basi kuna step nakosea? But I bet I did it right, but why then?
Kama kuna watalaam walokuwa wakinadi teknolojia hii waseme walifake au nini, maana hii sasa hasara tupu jamani!!!
huwa nacheka sana mambo yako ila nimefurahi kuwaona kuku wako poa. Ukiamini utafika hadi elfu moja na zaidi. Pambana
Ushaangalia prison break? Waweke uone dehydration hata ww humalizi siku moja humo ukiwa hai
Kwa hiyo hii teknolojia ni fake? Mkuu kama ulibahatika kuhuzuria maonyesho ya nanenane nadhani uliona baadhi ya mabanda ya halmashauri mbalimbali yalikuwa yanatoa elimu kuhusu teknolojia hii.Nahisi kitendo cha kuwafunika kimekupa matokeo hayo'vifaranga wanahitaji hewa safi pia najoto likizidi ni hatari pia.