Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

ki ukweli si biashara ya faida, bali inahitajika fedha kidogo tu mkuu kwani nimevipata kwa gharama,hivyo tunashare cost tu!!

ingependeza kukiwa na bei zake pia na ukienda mbali ukatupa walau dibaji ya kila kitabu ingekuwa bora zaidi
 
Mie sikubahatika kuona, lakini nitafika nane nane grounds nimeambiwa ni project endelevu, Mkuu Hossam unaweza kutupia michoro na vipimo vya banda lako, ...Hongera kwa usafi nimejifunza kitu hapo, pia ningeomba picha za banda lako la vifaranga
 
Mimi napenda sana kufuga bata mzinga naomba unipe mwongozo ili niweze kufuga bata hao
 
Nilikuwa na vifaranga 25 vina week 2 vimeshakufa 7 vimebaki 18 nifanyeje ili waendele kuishi nipate faida
 
Nilikuwa na vifaranga 25 vina week 2 vimeshakufa 7 vimebaki 18 nifanyeje ili waendele kuishi nipate faida

Mkuu,

Fuatilia yafuatayo
1. Maandalizi na nazingira ya banda la kuwalelea
2. Chakula
3. Kinga

Mie nilishauriwa kuwapatia vifaranga wa siku 2 vitamins, siku ya tatu au ya nne , unawapa kinga ya Gomboro na baadaye ya Mdondo ...haya ni magonjwa hatari sana kwa ndege wafugwao na has wakiwa vifaranga
 
Kinga inaitwaje nahiyo ya mdondo inaitwaje nifahamishe vizuri ili nielewe asante kwa msada wako
 
Kinga inaitwaje nahiyo ya mdondo inaitwaje nifahamishe vizuri ili nielewe asante kwa msada wako

suala la kinga linaweza kufanywa kwa huo Mdondo ama Newcastle desease na hiyo Gumboro ...nisemapo kinga nikuwa unawachanja kuku wako kuwakinga na hatari ya kuugua magonjwa mbalimbali ..lkn zaidi nikushauri utafute muda uonane na mtaalamu wa mifugo aliye karibu ama unayeweza kuwasiliana naye
 


hii ndio jf bana

ukifanikiwa tuchangie kidogo ila zaka ni muhimu zaidi mbarikiwe
 
Mimi nimenunua mitetea 30 na madume 4 toka kwa wafugaji mbalimbali, kwa lengo la kufuga. Hawa kuku hawajawahi kunywa chanjo ya dawa yeyote ile toka kutotolewa. Je naweza anza na kuwapa chanjo ipi kwa sababu nataka nifanye biashara ya kuuza kuku na hao ndo mtaji wangu? Nataka niwafungie ndani kwani nina eneo la kutosha hapa nyumbani kwangu kwa kutosha kuku 50. Naomba mnisaidie wajasiriamali wenzangu nianze na chanjo ipi ili niweze niwanusuru kuku hawa?
Wana umri wa miezi 5 mitetea na majogoo miezi 7
 

Mkuu, kwenye ukurasa huu huu wa ujasiriamali uliopost kuna maelezo mengi sana yanayohusiana na hiki ulichouliza. Angalia hizo nyuzi zilizowekwa sticky hapo juu ambazo zinahusiana na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Yaliyomo humo yanajibu swali lako na utapata na maarifa mengine mengi tu ya ziada! Cha msingi usiwe tu na uvivu wa kusoma kwa sababu yaliyomo humo ni mengi.
 
Fuata ushauri hapo juu. Zipo nyingi soma moja moja ..hutojuta
 
TaarFa
MKUU Gazeti na shauri twawezapatanames zenu

Natafuta jinsiyakutengeneza chakulachakuku wa kienyeji jamania
 
Wale wanaotaka vifaranga wa kuku wa kienyeji wasio chotara wanaweza kunitafuta. Vifaranga ni kwa oda. Acha ujumbe kwenye 0784222293 wakati wowote ukitaja idadi unayotaka.
Oda bila bei simimbampwa anakuachia funguo ya vits tena oldmod
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…