Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Hata mimi niko moshi mkuu! Unaweza niunganisha na huyo mwenye hao kuku wa kienyeji?? Je ni wa kienyeji au ni wale wa malawi???Mimi mbegu nimeutoa uko moshi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata mimi niko moshi mkuu! Unaweza niunganisha na huyo mwenye hao kuku wa kienyeji?? Je ni wa kienyeji au ni wale wa malawi???Mimi mbegu nimeutoa uko moshi
TUPIA NAMBA YAKO KAMA UKO DAR NATAKA KUKU WAWILI WA KIENYEJI KWAAJILI YA PASAKAMimi kuku wangu wore wamekufa na ugonjwa he nitumie DAWA gani
Dah nafurahi sana napoona mambo mazuri namna hii yanawekwa atika picha...yaani nakutamaniajeee...
Hongera sana kwa kuweza kukuza 240 kati ya 246 kwa kipindi choote cha miezi miwili maana dangerous zone ushaivuka, Hapo inabidi uanze kujiandaa kwa mazoezi ya mikono kwa ajili ya kuokota mayai....Hongera sana
Inawezekana mkuu, kama ukisoma mwanzo mwa huu uzi mkuu Kubota ameelezea vizuri sana.asigwa mkuu, wewe ni kati wa member waliotoa michango yao kwenye huu uzi wa kubota ambaye upo active JF.
Naomba nikuulize hili swali baada ya kutoa maelezo yangu. Matete yangu 3 yanataga. Moja ameanza tarehe 01/04, wa pili tarehe 02/04 na wa tatu jana tarehe 06/04.
Hawa kuku wote natoa mayai yao nayaifadhi mimi nikitegemea kuja kuwawekea siku moja ili vifaranga vizaliwe vya umri moja yaani siku moja.
Je kwa utofauti wa kuku wa kwanza na wa tatu ambao ni siku sita, hili jambo litawezekana kweli?
Asante mkuu!! Umenitoa wasiwasiInawezekana mkuu, kama ukisoma mwanzo mwa huu uzi mkuu Kubota ameelezea vizuri sana.
Unachotakiwa ni kuchukua mayai yote kwa pamoja halafu unachagua kuku wawili wazuri wanaoweza kuatamia, dhen pale ambapo wanaaza kuonesha dalili ya kuanza kuatamia unawawekea, kuku hana shida kabisa.
Kumbuka kuwa kuna watu wenye kuku wengi ambao huwa wanahifadhi mayai viza, wao huwa kuku akianza tu kuonesha dalili za kuatamia wanamzubaisha kwa kumuwekea mayai viza, na anaweza kuyalalia hata wiki mbili ili asubiri wenzake wakamilishe mayai mengi ya kuatamiza.
Mayai yakishakuwa mengi unamtegea usiku unatoa mayai viza unaweka yale mazuri, kuku anaendelea kuatamia tu.
Zoezi hili hufanyika usiku kwa kuwa kuna baadhi ya kuku "wana nyodo" kama watu na wako makini mno, ukimpa mayai sio yake anasusa kuatamia, lakini hizi ni kesi chache sana ni kesi moja kati ya 1,000.
Karibu sana mkuu.
Karibu sana....Asante mkuu!! Umenitoa wasiwasi
Hii nimependa sana mazeeWana Jf,
Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!
Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.
Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.
Stay tuned and keep on visiting this thread!!
===============
UPDATE
===============
Mkubwa tunakusubiria bila shaka kabisa Kubota; kwani hakika ni na imani ni mbinu mbadala kabisa unakuja nayo mkubwa wangu! Hii uzi ninaisave left kabisa nikitegemea newz toka kwako! Asante sana! Hapa ndiyo Jf jamani!
Mkubwa tunakusubiria bila shaka kabisa Kubota; kwani hakika ni na imani ni mbinu mbadala kabisa unakuja nayo mkubwa wangu! Hii uzi ninaisave left kabisa nikitegemea newz toka kwako! Asante sana! Hapa ndiyo Jf jamani!
Safari yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10 kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10 unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu sana! Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!
Safari ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia. Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja! Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapajoto la kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!
Ili utotoreshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia incubator, tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga kwa pamoja hufikia wakati mayai huishatumboni unakuta wamelala kwenye viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15. Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120. Kwa kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya. Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!
Kuku akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine wanambinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tega, au Box kubwa au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA. Hawa kuku wakitoka JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia. Pia kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai lililotagwa siku hiyo! Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo. Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi! Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto la Mama bure!
Ndugu zangu wana JF naendelea kuelezea utotoleshaji bado sijamaliza hebu niwarushie hii kwanza maana nimeona nimechelewesha kuwakilisha na nimewaudhi, poleni, mwenzenu nilikuwa nahangaika kufukia tanuru la mkaa nimekuta limefunguka! Si mnajua maisha jamani!
Karibu sana....
Dah mkuu hili swali lako ni la kitaalamu sana, inabidi kufuatilia mzunguko wa "hedhi ya kuku" au kitaalamu ovulation cycle yake inatokeaje.Mkuu! Pole na majukumu ya kila siku. Nina swali naomba unisaidie.
Wakati nimenunua hawa matetea nilinunua na jogoo moja, mwezi wa tatu mwanzoni.
Jogoo sikumpenda sana kutokana na umbo lake, ila alikuwa mshuhulikiaji mzuri kwa hawa matetea.
Siku moja kabla ya Pasaka nilipata jogoo mwingine ambaye mimi nilimpenda kwa umbo lake. Yule jogoo wa kwanza nikamchinja Pasaka.
Huyu jogoo wa sasa toka nimnunue, siku tano tetea wa kwanza akaanza kutaga, mwanzoni mwa mwezi wa nne. Pia hili jogoo ni mshuhulikaji mzuri kwa matetea.
Swali langu, jee vifaranga vikitotolewa, vitakuwa vya jogoo yule wa kwanza au huyu wa pili?
Amina!Dah mkuu hili swali lako ni la kitaalamu sana, inabidi kufuatilia mzunguko wa "hedhi ya kuku" au kitaalamu ovulation cycle yake inatokeaje.
Ngoja nichimbe kwanza kwenye vyanzo vyangu muhimu nitakuletea mrejesho.
Ila kwa sasa siwezi kukujibu maana hili swali ni la kitaaluma sana mkuu, na hii kesi binafsi sijawahi kukutana nayo.
Ngoja nichimbue vitabuni na kuuliza wataalamu wangu wa mifugo nitaleta mrejesho, naogopa kukupa jibu la moja kwa moja maana maandishi haya hukaa vizazi na vizazi.
Asante sana mkuu Asigwa, ubarikiwe sana. Umenipa shule nzuri, sasa ubongo wangu umetuliaNaam mkuu kwamtoro kulingana na mtaalamu wangu ishu iko hivi.
Anatomy ya kuku iko hivi, Kuku jike ameumbwa na sehemu moja iko karibu na uke wake yenye uwezo mkubwa wa kutunza mbegu za kiume(shawaha ya jogoo) kwa muda wa siku 10 mpaka 14.
Kwamba hata kama kuku hajaanza kutaga, kama ndani ya wiki moja au mbili alipandwa na jogoo basi hizo mbegu(shahawa) hupelekwa kwenye store maalumu(special glands) na kuhifadhiwa huko kwa kati ya siku 10 mpaka 14 kabla ya kuharibika na kutolewa nje ya mfumo wa uzazi.
Kuku anapoanza kutaga tu, shawawa hizo hutolewa kutoka kwenye hio store(gland) na kupelekwa sehemu ya kurutubisha yai.
Kwa msingi huo basi huyo jogoo wako uliyemchinja bado shahawa yake ilikuwa imetunzwa ndani ya tetea wako, na kuna uwezekano mkubwa akataga mbegu ile ile hata kama atakuwa amepata jogoo mpya.
Lakini pia kuna ishu moja kuwa kama kuku anayetaga akipandwa na jogoo mpya, zile mbegu zilizohifadhiwa kwanza kwenye gland huingizwa katika ushindani na mbegu za jogoo mpya na zenye nguvu ndizo hurutubisha yai, na uwezekano wa kushinda huwa ni 50% kwa 50%.
Kwa hiyo generally ni kwamba kuku wako huyo mpya vifaranga atakavyoangua vitakuwa na 30% ya jogoo wa zamani na 70% ya jogoo mpya.