Wakuu, nimeanza tena ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mara hii natumia mfumo
wa NUSU HURIA nimeanza na kuku 15 mwaka Jana mpaka sasa wako 369
Nimeuza kuku 271 kwa bei za kati ya Tsh 17,000 mpaka 23,000 namshukuru
Mungu nimeweza kupunguza ukata.
Mwakahuu kuna ttizo kubwa limejitokeza nashindwa jinsi ya kulikabili, Kuna ndege
Mdogo kwa umbo anafanana sana na njiwa, anakamata vifaranga balaa. Tena
anakamata wale vifaranga wakubwa ambao wanajitegemea. Ndani ya wiki mbili
hizi amekamata vifaranga 18.
Sijajua jinsi ya kumdhibiti yaani huyu mshenzi ananipa hasira si mchezo.