Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Tengeneza manati wewe ingia windoni.
Hapana Kipanga huwezi Kupiga kwa Manati kwani hata Makazi yake hayajulikani yeye huja wakati wa Kula Kwa spidi ya Ndege zisizo na Rubani ninachowapendea Kuku wa Kienyeji hawajazubaa kama umewawekea mazingira ya Kukimbilia wanaweza Wasikamtwe ila Sehemu ikiwa plain sana ndo Watakamatwa.
 
Mkuu hongera watu wakikuona kwenye siasa wanakuona mlugaluga kama wao. Kumbe sivyo.
Mkuu hizi ndo Changamoto za Humu unaweza Kua Unabishana na Mtu mwenye Miaka 18 Dharau nyingi Mtu kama anakufahamu Vile kila ukimwambia Kitu yeye anaona Ni Uongo tuu.
 
Msaada vifaranga Wamepigwa na Ndui Dawa gani ambayo itawatoa

d91d6412113b1da1f2b61b6b33a37e66.jpg

e48ce1a69365dfa60455d11c455becee.jpg
Mkuu kwanza pole,nenda duka la dawa na nunua vidonge vya PEN V. Chukua vidonge 5 weka kwenye maji Lita moja na wape hao kuku wako kwa ck 3-5. Utaona matokeo ndani ya ck 3. Nakuomba ulete mrejesho maana hio dawa ni mujarabu.
 
Mkuu mimi nataka nianze kufuga kanga hivi naweza kuwa nawachanganya na kuku kwenye banda moja?
unaweza kuwachanganya wakiwa wadogo kwani wanapenda sana kufuatilia majogoo wanapokuwa wadogo. Tatizo la kanga linakuja wakisha kuwa wakubwa ni wachokozi sana kwa viumbe tofauti na wao na hata wao kwa wao hasa majogoo wakati wa kutaga, halafu wana ushirikiano kwelikweli , wakicharuka kama haupo unaweza kukuta kuku wote wameuawa. Tatizo jingine la kanga ni kelele. Wanatabia ya kupiga kelele usiku na mchana, kwa hiyo kama umezoea utulivu kanga si wa kufunga ingawaje kanga ni rahisi sana kufuga kuliko kuku kwa sababu hawana magonjwa mengi kama kuku. Kanga hupenda kutanga kipindi cha mvua na pia hupendelea kutaga polini, kwa hiyo wakati wa kutaka wafungie bandani tangu asubuhi mpaka saa kumi jioni ndipo uwafungulie ili wafukuzane na na kupandana , usipowafungulia jioni utaathiri utagaji kesho yake. Hapa nilipo kanga wanataga kuanzia mwezi wa kumi. mfululizo mpaka may mwaka unaofuata.
N.B - usiwaruhusu kanga kuhatamia mayai yao badala yake wape kuku wahatamie au weka kwenye mashine ya kutotoresha. Kanga si watunzaji wazuri wa vigaranga wao na pia kutaathiri utagaji wao.
 
Hahahahaha "anafanana na njiwa". Huyo ni KIPANGA hana macheko na kuku. Kama mwanafunzi na kitabu.
 
mimi nilikuwa na changamoto ya kuibiwa kuku mama watoto akaenda kwa mtaalam mwizi alipatikana kesho yake baada ya kuiba jogoo kubwa nakulila na mkewe. Jamaa alijileta mwenyewe akiwa anaumwa tumbo balaa na mke wake huku jogoo akiwika mfululizo tumboni alitaja mwenyewe kila alichoiba kwangu na kwa majirani. Alitozwa faini ya ng'ombe sita kama fidia kwangu na majirani ng'ombe moja wakachinja nyama. Tangu siku hiyo mambo swali kabisa , mwaka huu hata shamba la mahindi sikuweka mlinzi. Kumbe duniani kuna ulinzi asilia sikuwa naamini.
Ha ha ha wee kiboko! Hadithi hii inatufundisha nini? Kwamba tujifunze kutafuta mbadala wa changamoto zetu[emoji1] au tuwe na kamati za ufundi kwa kila jambo?
 
mimi nilikuwa na changamoto ya kuibiwa kuku mama watoto akaenda kwa mtaalam mwizi alipatikana kesho yake baada ya kuiba jogoo kubwa nakulila na mkewe. Jamaa alijileta mwenyewe akiwa anaumwa tumbo balaa na mke wake huku jogoo akiwika mfululizo tumboni alitaja mwenyewe kila alichoiba kwangu na kwa majirani. Alitozwa faini ya ng'ombe sita kama fidia kwangu na majirani ng'ombe moja wakachinja nyama. Tangu siku hiyo mambo swali kabisa , mwaka huu hata shamba la mahindi sikuweka mlinzi. Kumbe duniani kuna ulinzi asilia sikuwa naamini.
Mkuu wewe utakuwa msukuma
 
Mshirikina wewe,pumbavu.
Usimtukane unakosea, Tanzania is a cellular nation mtu unaruhusiwa kuwa mkristo, muislam, mpagani au kuabudu chochote as long usivunje sheria za nchi! Mi nakuona wewe ndio mpumbavu hapa! Mbona povu zito au wewe ndio uliolipishwa ng'ombe una uchungu? Nae alichoka kufugia manyani akatafuta solution anayoiamini na end of the day tatizo likawa solved!
 
Nashukuru mkuu umempa makavu live , hawa ndio wanajifanya kumjua Mungu kumbe ni WACHAWI wakubwa ingawaje bado anatunzwa, ngoja ajitegemee aone. Shida hufundisha maarifa.
 
dawa ya vifaranga kushusha mabawa na. macho kuvumba na mwishoe vifaranga kufa nimejaribu chanjo lakini wapi sijatotoleza muda sasa.
Tafuta OTC 50% uwapatie kwa muda wa siku tano utaona matokeo

Pia karibu ujipatie vifaranga bora vya kuku wa kieneyeji kwa bei nzuri kabisa
Tunapatikana Mwanza - Kisesa

kwa number 0713 646577 au 0752 093038
Tunasafirsha popote pale Tanzania
 
Attachments

  • 18010589_128811530995512_7929575659043006717_n.jpg
    18010589_128811530995512_7929575659043006717_n.jpg
    27.9 KB · Views: 154
  • 18033303_128968150979850_698485185572255482_n.jpg
    18033303_128968150979850_698485185572255482_n.jpg
    97.4 KB · Views: 123
Huyo ndege mdogo anaitwa mwewe. Wafungie ndani hao vifaranga wadogo mpaka wakue ndio uwaachie mtaani! La sivyo faida utaigawana na mwewe...
 
Wakuu, nimeanza tena ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mara hii natumia mfumo
wa NUSU HURIA nimeanza na kuku 15 mwaka Jana mpaka sasa wako 369
Nimeuza kuku 271 kwa bei za kati ya Tsh 17,000 mpaka 23,000 namshukuru
Mungu nimeweza kupunguza ukata.

Mwakahuu kuna ttizo kubwa limejitokeza nashindwa jinsi ya kulikabili, Kuna ndege
Mdogo kwa umbo anafanana sana na njiwa, anakamata vifaranga balaa. Tena
anakamata wale vifaranga wakubwa ambao wanajitegemea. Ndani ya wiki mbili
hizi amekamata vifaranga 18.

Sijajua jinsi ya kumdhibiti yaani huyu mshenzi ananipa hasira si mchezo.
Unaweza kuzungushia wavu kwa juu eneo wanalokula mchana ili ndege asawafikie lakini waendelee kupata jua.Nikumbushe nikupe picha ya mfano kwenye 0713-039875
 
hakikisha kila ck unabadilisha maji ya dawa,ni vidonge 5 ktk lita 1 ya maji.
 
Back
Top Bottom