Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Msimu Wa mdondo umeanza mtaani kuku wanapukutika tu

HV dawa yake nn?!
 
Ni vyema pia kujua kuwa kuku chotara ana apetite kubwa sana ya kula. Jiandae kwa hilo.
 
Wanapouza Chakula cha kuku na ushauri pale Ilala boma wapo FARMBASE wapo vizur
 
Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.
Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.

HABARI,
"newmzalendo,
Hongera,Kuhusu soko kwa kuku wa kienyeji na hasa kwa Dar usiwe na wasiwasi mkuu soko lipo kubwa sana,

LUMUMBA
 
Msimu Wa mdondo umeanza mtaani kuku wanapukutika tu

HV dawa yake nn?!
Unapofuga kuku zingatia chanjo Katika hatua zote hata kama haujaona dalili za ugonjwa wowote. Shirikiana na mabwana mifugo mkuu kwa ushauri !
 
Vipi kuhusu kuroiler wako vipi kwa kutotolesha kwa kutumia incubator make nasikia hawana uwezo wa kulalia lakini nasikia wanakua na uzito mkubwa na mayai wanataga mengi naomba kujua ukweli juu ya hwa kuroiler plse
 
Vipi kuhusu kuroiler wako vipi kwa kutotolesha kwa kutumia incubator make nasikia hawana uwezo wa kulalia lakini nasikia wanakua na uzito mkubwa na mayai wanataga mengi naomba kujua ukweli juu ya hwa kuroiler plse

HABARI,
"Abel edward otieno,
Kweli kuroiler wako vizuri sana na unaweza kuwatumia kwa nyama au kwa mayai wanakua haraka ndani ya miezi mitatu na nusu unaweza kuwauza kwa nyama na minne wanaanza kutaga mayai.Wanaweza kujitaftia chakula wenyewe kama kuku wa kienyeji ila ni vema kwa mijini ukawalisha chakula wana wastani wa kutaga mpaka mayai 150 kwa mwaka kila kuku ikiwa na maana ndani ya siku mbili anataga yai moja,kwa hiyo ukiwanao kuku 1000 tegemea kuwa na tray 12-15 kila siku na garama zao za ulishaji sio kubwa kama wale kuku wa mayai pure nikiwa na maana hawaitaji chakula maalaumu ila wanakula sana.
Na kama unataka kununu hao hakikisha unakwenda kwenye watotoleshaji maalumu la sivyo unaweza ukauziwa chotora wa kuroiler ambao kwa mayai hawataweza kutaga sana .Pia unaweza kuwa na kuku wa kienyeji kama 30 ukawaweke mayai yenye mbegu ya kuroiler ukapata vifaranga wake mayai yapo kwa watotoleshaji pia.Ila kama unataka pia kuwa na mayai ya kuroiler kuyaandaa mwenyewe tafuta kuku kuroiler kama 10 na majogoo yake 3 ukiwaweka pamoja peke yao hapo utakuwa na mayai bora yenye mbegu ya kuroiler na unaweza kuwawekea kuku wa kienyeji wakalalia au ukapeleka kwa watotoleshaji mayai wakakutotoleshea kwa bei nzuri.Ila mayai ya kuroiler ya mbegu hayatakiwi kukaa sana hasa zaidi ya siku kumi lazima yaanze kulaliwa au kuwekwa wenye mashine ya kutotoleshea sana yakae wiki moja tu.


LUMUMBA
 
Back
Top Bottom