Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

siku ya kwanza mpaka ya saba unawapa OTC 20%, SIKU YA 14 NEW CASTLE,SIKU YA 21 GUMBORO,SIKU YA 35 NDUI,UTARATIBU HUU UTAKUWA UNAURUDIA KILA BAADA YA MIEZI 3 KASORO CHANJO YA NDUI TU.
Hao ni kuku wa nyama, wa mayai au wa kienyeji?
 
Wakuu kwema
Mimi bado najikita kwenye swala la soko la uhakika je nyie mnafanya je maana kuwa uzia hawa madalali faida inakuwa finyu sana

Kwa mfano kama nataka kuuza kuku 100 kwa mkupuo na nataka kila kuku niuze 15,000/= naweza pata wapi soko la uhakika mkoa gani Naomba kama una mtandao wa soko la kuku wa kienyeji unijuze . Mimi nipo singida
 
Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..

*_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
* _Popote ulip0 dar unaletewa..*_

CALL-0752-109265
 
Wadau, wafugaji wenzetu wa "Brolier" Dar wanalalamika soko la kuku liko "saturated", kwamba kuku ni wengi mpaka bei imeshuka sana, ni kweli? Kwamba tunauza kuku kwa 5,000/- mpaka 5,500/-...
 
Kwa maandishi ni rahisi sana kila kwa vitendo
Nilikuwa na vifaranga 30 nikwapa chanjo full kila kitu lakn Leo wana miez 2 wamebaki 3.nimeamua niwaachie huru
 
Ugonjwa no 1
Tafuta mafuta ya ng,ombe mabichi

Uwe unawapaka Na kuwalisha hao vifaranga
Duh.mkuu hii point yako nimeikataa.kuna daktari wa mifugo aliniambia kuku hawafai kupewa vyakula vyenye mafut yoyote.hata viporo vya vyakula vilivopikwa,ni hatari kwa uhai wa kuku.
 
Unaweza kufanikiwa iwapo vikishatotolewa vikusanye vyote, lets say hao 100 wametoto wote vifaranga 7 (minimun number) utakuwa na vifaranga 700.

Watunze kwenye chumba chenye joto la wastani ili wasipate baridi, wanunulie chakula (Chic starter ) 50kgs, unaweza ongeza soya iliyosagwa 5kgs hivi changanya fresh.

Nunua OTC plus na any multivitamins (dawa za packet) hizi ni za unga, zichanganye pamoja kisha uwe unawapa vifaranga hvi kwenye maji ya kunywa.

Wiki ya kwanza - chanja Gombolo
Wiki ya Pili chanja Newcastle.
Wiki ya tatu rudia Gombolo
Wiki ya nne rudia Newcastle
Wiki ya sita chanja Ndui (Pox) (Muhimu sana )

Wakifika wiki ya 9, watoe bandani waanze kutafuta msosi wao wenyewe, unaweza kuwa unawaongezea bumba ili wakue vizuri zaidi.

Muda huo mama zao watakuwa wameshatotoa tena, kwa hiyo unaweza kuwa na kuku zaidi ya 6,000 at the end of 2018.

Kama utauza kuku kwa bei ya kutupwa ya 15,000 basi ndugu utakuwa na 15,000 times 6,000 = 90m.

Kazi njema, ila siyo kazi ndogo kufikia hapo, unahitaji kufanya kazi kubwa mno hasa kwenye utunzaji na ulishaji.
 
Njoo pm nikupeleke jukwaa la ufugji kuku huko kuna wbobezi wa haya mambo
 
Sawa mkuu
 
MIFUPA
Tunauza mifupa inayotokana na wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi nk
MATUMIZI
1. Inatumika kutengeneza chakula cha mifugo, kama vile kuku, kanga, bats ,nk
2. Kutungenezea sahani za mifupa
TUNASAMBAZA
1. Kilo moja hadi tan ya kilo za mifupa
YEYOTE ANAYETAKA KWA SHUGHULI YOYOTE
Mawasiliano
0627908738
0685876284
 
Kuhusu ndui kuja mtu anajiita Tamutamusana alijitangaza kuwa na dawa ya ndui. Mm nilinunua nikawapaka vifaranga wagonjwa wote walipona. Ugonjwa wa ndui ndio kikwazo kikubwa sana kwa ufugaji wa kuku
Kweli kabisa mkuu
 
Pata kuku wataamu kabisa
X-mass hii kujiramba mwanzo mwisho
( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa
jogoo 20, 000tsh @1..
tetea 17,000tsh @ 1..
*_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
* _Popote ulip0 dar unaletewa..*_

contact
0714-111058
0752-109265
 
HABARI,
"Abel edward otieno,
Kweli kuroiler wako vizuri sana na unaweza kuwatumia kwa nyama au kwa mayai wanakua haraka ndani ya miezi mitatu na nusu unaweza kuwauza kwa nyama na minne wanaanza kutaga mayai.Wanaweza kujitaftia chakula wenyewe kama kuku wa kienyeji ila ni vema kwa mijini ukawalisha chakula wana wastani wa kutaga mpaka mayai 150 kwa mwaka kila kuku ikiwa na maana ndani ya siku mbili anataga yai moja,kwa hiyo ukiwanao kuku 1000 tegemea kuwa na tray 12-15 kila siku na garama zao za ulishaji sio kubwa kama wale kuku wa mayai pure nikiwa na maana hawaitaji chakula maalaumu ila wanakula sana.
Na kama unataka kununu hao hakikisha unakwenda kwenye watotoleshaji maalumu la sivyo unaweza ukauziwa chotora wa kuroiler ambao kwa mayai hawataweza kutaga sana .Pia unaweza kuwa na kuku wa kienyeji kama 30 ukawaweke mayai yenye mbegu ya kuroiler ukapata vifaranga wake mayai yapo kwa watotoleshaji pia.Ila kama unataka pia kuwa na mayai ya kuroiler kuyaandaa mwenyewe tafuta kuku kuroiler kama 10 na majogoo yake 3 ukiwaweka pamoja peke yao hapo utakuwa na mayai bora yenye mbegu ya kuroiler na unaweza kuwawekea kuku wa kienyeji wakalalia au ukapeleka kwa watotoleshaji mayai wakakutotoleshea kwa bei nzuri.Ila mayai ya kuroiler ya mbegu hayatakiwi kukaa sana hasa zaidi ya siku kumi lazima yaanze kulaliwa au kuwekwa wenye mashine ya kutotoleshea sana yakae wiki moja tu.

LUMUMBA
Nitapate Hawa kuku yaani naomba contact pls
 
Back
Top Bottom