Elimu nzuri..Ila kama mtu anakosa jiko la mkaa n.k,unaweza kutumia dumu: chemsha maji halafu chukua dumu la lita 20 na yaweke humo halafu funga kabisa liweke juu ya tofari ili vifaranga wasiungue,kwa kawaida dumu litatoa joto ambalo linawafaa sana vifaranga
Wakisogea karibu sana na dumu ujue joto halitoshi kwa hiyo maji hayakuchemshwa vizuri na wakikaa mbali sana na dumu ujue joto ni kali,ongeza tofali likae juu kidogo.
La msingi kuhusu banda ni vizuri kama una eneo la kutosha fuga nusu huria: jenga banda ambalo kuku watalala usiku halafu mchana wanakaa ndani ya uzio na hiyo itapunguza gharama za usafi na pia kuku watapata mazoezi.Zingatia pia kwamba hawa ni kuku wa kienyeji kwa hiyo unaweza kuwaachia wakatoka nje kabisa ya uzio ili wapate chakula kama wadudu wanaoruka na wanaotambaa.
Nitarudi baadae.........