Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kubota;

Upo? Hebu amka endelea kwani wengine tuna hamu sana na thread hii!
Samahani kwa usumbufu wowote ule!

Kha ha ha ha ha ha haaaaa! Kubota bwana!
 
Last edited by a moderator:
Masimulizi yangu jana niliwagusia kuwa nilikuwa nina banda kubwa lenye chumba na sebule, pia nilikuwa nina JELA ambapo mwanzoni nilitumia matenga au mabox! Baada ya kuanza kutotolesha vifaranga, ilibidi nijenge kibanda cha kukuzia vifaranga (Nursery)! Kilikuwa kibanda kidogo kidogo tu mfano wa kigorofa hivi nitaelezea siku nyingine nilivyokitengeneza na mchoro wake mtauona. Picha ya Kuku niliewaonyesha huko nyuma yumo ndani ya moja ya vyumba sita ambapo vyumba vitatu viko chini na vitatu viko ghorofani. Vyumba hivyo vilikuwa vya kukuzia vifaranga.

Mara baada ya kutotolewa kwenye banda kubwa vifaranga na mama zao niliwahamishia kwenye hii nursery. Kila chumba niliweka chakula na maji ya kutosha siku nzima kila siku asubuhi. Kuku walikuzwa humo kwa muda wa mwezi mmoja ambapo baada ya vifaranga kuota manyoya mwili mzima ndipo mama zao niliwatoa. Kisha hawa vifaranga wakubwa ambao nitakuwa nawaita VINYOYA niliwasambaza wote kwenye vyumba vingine vitano na nilibakisha chumba kimoja tu ambacho ndiyo hicho nilikitumia kama JELA! Nilishawaelezea tayari juu ya matumizi ya hii Jela.

Hao VINYOYA baada ya kuwatengenisha na mama zao niliwaacha wiki moja kisha nao nikawa nawafungulia waanze kuokoteza chakula na kuchunga. Wakati huu kwenye banda kubwa kulikuwa na kuku wanaoatamia ambao niliwawekea mayai siku 10 baada ya kutotolewa hawa VINYOYA! Kwa hiyo kwa kujua kuwa kuna vifaranga ambao wangetumia hii nursery hapo baadae, ilibidi nijenge banda lingine kwa ajili ya kuwakuzia hawa Vinyoya. Baada ya kuwahamishia hawa vinyoya kwenye banda lao nilikuwa ninawaaacha hadi miezi miwili au zaidi kabla ya kuwahamishia kwenye banda kubwa.

Hadi kufikia hapo mzunguko wangu wa mabanda ya kuku ukawa umekamilika! Yaani nilikuwa na banda kubwa sebuleni kwa ajili ya kulala na kutaga kuku wakubwa, chumbani kwa ajili ya kuatamia na kutotoleshea, banda la kukuzia vifaranga (nursery) na banda la kukuzia vinyoya. Vipimo na michoro na vifaa nilivyotumia kujenga miundombinu hii itakuja peke yake na siku yake itawadia.


Wana JF kuna mtoto hapa nilipo kaja kuniambia kwamba huko kijiweni kwangu (porini) kimenuka, tanuru langu la mkaa limeachia mwee, ngojeni nikimbie nikalizibe nitarudi baadae mwenye maswali atupie, nikirudi nitakuja yajibu au mwenye mchango tushirikishane! ITAENDELEA……!
Mbona haujarudi tena?unatuweka roho juu kila wakati kuchungulia hapa Kama umerudi,tupe shule bwana
 
Wapendwa Blaki Womani, Liverpool, Mama Tinny na wadau wengine mnaofuatilia huu uzi, chonde chonde msichoke wala kukata tamaa muwe na uvumilivu ule wa kijasilia mali niko nanyinyi hadi msikie mwisho wa hadithi yangu. Nachelewa kuwadumbukizia humu shauri ya pilika zangu za huko porini kwenye mkaa, jana nilikuwa nakurupushana na bwana miti aliona moshi wa tanuru langu la mkaa akafuata ulaji, sasa nabadili staili nitakuwa nayaanzisha kuyawasha matanuru yangu usiku, hadi ifike asubuhi tanuru halitoi moshi! Nitarudi jamani hapa naandaa masimulizi ya chakula cha kuku! Stay tuned no matter how long it gonna take, I will be back mweee eenh Jamani!
 
Kwa hali ya kawaida unapokuwa na kuku wachache wasiozidi 20 mazingira ya majumbani kwa kiasi fulani hutosheleza mahitaji ya kuku! Kuku na vifaranga huzurula huku na kule wakiokoteza wadudu, mabaki ya chakula na majani hata matunda pia! Vifaranga hukua vizuri tu na kama kuna vifo vya vifaranga vifo hivyo husababishwa na mambo mengine na siyo lishe!

Lakini unapoamua kufuga kiujasilia mali kuwa na kundi kubwa ndiyo lengo, kuku wakiwa wengi zaidi utahitaji eneo kubwa zaidi ambako kuku husambaa mbali zaidi wakiokoteza! Kwahiyo wale wanaoishi sehemu zisizokuwa na mbanano wa makazi ya watu wanafursa kubwa sana ya kuzalisha kuku wa kienyeji kwa gharama ndogo. Kuku wakiwa wengi sana hufikia wakati wanakuwa wameshaokota mabaki yote na wadudu wote! Kundi la kuku linapokuwa kubwa kama huwezi kupata eneo kubwa zaidi unalazimika kuwapa chakula cha ziada ni lazima kuwatafutia chakula.


Mimi nilikuwa nikifugia eneo ambalo majirani zangu kulia na kushoto walikuwa umbali wa nusu ya urefu wa kiwanja cha mpira, huku mbele ya makazi yangu na nyuma ilikuwa ni mashamba. Hofu kwangu ilikuwa ni vicheche na wanyama wabaya ambao baadae niliwadhibiti kama nitakavyosimulia huko mbeleni.


Niliamua kujidhatiti kutengeneza chakula. Kipaumbele kikubwa ilikuwa kutengeneza chakula cha vifaranga, kwa sababu sikutaka wazurule! Kuwaacha kuku wenye vifaranga wazurure vifaranga wengi huliwa na maadui, matokeo yake kuku hawaongezeki. Nilinunua kinu kwa ajili ya kutwangia mashudu ya alizeti na dagaa, nilinunua unga wa mifupa, madini ya chokaa, vitamin, nilinunua mahindi na kuyapalaza. Wakati mwingine nilinunua vumbi la dagaa na pia kunamashine zilikuwa zinauza mashudu ya alizeti yaliyosagwa tayari. Nilichanganya mchanganyiko huo kwa kufuata formula ambazo zipo. Kuna aina nyingi tu za formula za kuchanganya vyakula vya kuku hata humu JF ukifuatilia wadau walishazishusha kwa wingi tu! Hiki chakula kwa ajili ya vifaranga ndiyo hiki hiki pia nilikuwa ninawawekea kuku wanaoatamia kwa kuwa hiki chakula kimekamilika kwa lishe na hao kuku waatamiao hawatoki nje kwa hiyo ilikuwa lazima walishwe chakula bora.


Naomba nitumie fursa hii kuwa muwazi na nikiri kabisa kwamba pamoja na umakini wangu wa kutengeneza na kuchanganya chakula kwa ajili ya vifaranga na pamoja na kutumia formula nilizokuwa nazipata kwenye maonyesho ya 8-8 NILICHEMSHA !!


Vifaranga walikuwa wanapukutika baada ya siku 10 au wiki 2. Sikuelewa kwa nini na nilikuwa naona kizunguzungu! Nilifanya kila nilichotakiwa, niliwapa chanjo, niliwapa madini niliwapa antibiotics lakini vifaranga walikuwa wanapukutika! Vifaranga walikuwa wanatotolewa sana na kwakweli ilifikia hatua wala nilikuwa sifurahii huo utotoaji mkubwa maana nilijua hatimae watakufa! Nihadithi ndefu sana kusimulia nilivyohangaika kujua chanzo cha tatizo hilo! Nilikutana na mtaalamu akanieleza kuwa huwezi kuchanganya ingredients za chakula cha kuku kwa mikono ukapata mchanganyiko mzuri! Aliniambia uchanganyaji ni changamoto kubwa! Aliniambia fumba macho nunua chakula cha vifaranga! Chick Marsh!

Kwa kuwa vifaranga ni chimbuko la ukuaji wa kundi la kuku, nilinunua mfuko mmoja wa chakula cha vifaranga Chick marsh kwa ajili ya kuwavusha vifaranga mwezi mmoja tu, kisha baada ya hapo niliendelea kuwalisha chakula changu cha SIDO (cha kutengeneza mwenyewe)!! Kuanzia hapo nilisahau rasmi kushuhudia vifo na kutupa vifaranga. Ndege ya mafanikio ya ufugaji wa kuku wa kienyeji hapo ilianza kupaaa! Kusema kweli kwa kuwa nilishahangaika sana wadau JF kama kuna aliyefanikiwa kutengeneza chakula cha kulisha vifaranga na anafanikiwa kuwakuza vifaranga ninampongeza sana na tusaidiane utaalamu huo maana mimi hapo nilishanyoosha mikono.


Mwezi wa kwanza wa uhai wa kuku ni mwezi wa muhimu sana. Ni huo mwezi wa kwanza hufanya wafugaji wengine kusonga mbele na wengine kukata tamaa! Kuwavusha vifaranga mwezi ule wa kwanza ni hatua kubwa sana! Kuku wakishafikia hatua ya kuota manyoya unakuwa umepita kipindi kimoja kigumu sana! Ni ushindi! Hadi sasa nilishaamua kwa ule mwezi wa kwanza huwalisha vifaranga wa kuku wa kienyeji chakula bora kisichokuwa na mashaka kwa kununua Chick Marsh.

Kwa ndugu zangu mlioko maeneo ambako chakula hiki cha kununua hakipatikani, nawashauri acheni kuku wenye vifaranga wachunge wenyewe huko wanapata balanced diet kulikoni kuwafungia! Labda kama tutapata msaada wa ujanja wa kutengeneza chakula cha vifaranga hapa JF


Masimulizi ya Chakula cha kuku YATAENDELEA…..
 
Mkuu shule nzuri sana, nadhani inabidi uwe commited sana kama kweli unataka kuendelea vizuri kwenye ufugaji kama wako wenye gharama nafuu
 
mkuu hii shule ni kubwa sana ambayo kitendo cha kuwa na uzoefu wa kutoka field kabisa sio wa kusimuliwa kwa nadharia.naomba nikiri mi mwenyewe nimekuwa muhanga wa vifo vya vifaranga na nilikuwa nawapa chakula nilichochanganya kwa mkono.Hongera mkuu
 
hii habari ya chakula inabidi kuifanyia kazi hii hebu Kubota atwambie kama aliweka kila kitu kinachohitajika na kwa uwiano halisi? mimi naona tukikwamuka hapa kwenye chakula itakuwa mteremko sana maana mfuko wa chakula unafika hadi 45000 kipindi sasa vifaranga vikiwa vingi itakuwaje?
 
Mama Joe kwenye chakula na hicho kipindi cha mwezi mmoja wa kwanza kweli kuna changamoto na nahisi tatizo sio kuweka kila kitu na kwa ratio inatakiwa. Inawezekana matatizo yakawa mawili makubwa.

Mosi, ni size ya punje za mahindi, dagaa na pumba.katika hali ya uchanganyaji wa mikono ni ngumu hivi vitu kusagika na kuwa katika punje ndogondogo kwa kifaranga wa siku moja hadi wiki tatu kuweza kula. Mara nyingi inatokea punje za mahindi ni kubwa hata kama zimeparazwa.

Tatizo la pili nahisi ni uchanganyaji wenyewe mana kwa kuchanganya na mikono ili vichanganyio vyote vichanganyike vizuri nayo sio rahisi sana hata kwa kuchanganya kilo 50 tu.

Kwa mtazamo wangu nahisi hivyo ndo vinavyochangia.

Asante.
 
Ni kweli naelewa unatakiwa uchanganye kwa mashine, unaweza nunua kila kitu na vikorokoro vingine ukaongezewa kwenye mashine zinazosaga wakakusagia ukapaki mifuko yako, saizi ya punje itakuwa ngumu kama unatumia kinu na sio mashine. Namsoma amesema alinunua kinu.... alternatively kuna maduka ya vyakula huwa yanauza mahindi yaliyoparazwa na vikorokoro vingine vingi, vifaranga wanahitaji vitu vyote muhimu kwani wanakua haraka. Kuna formula zinataja damu, mabaki ya samaki, majani yaliokaushwa, premix, kwa v iwango tofauti sasa kama vikizidi au kupungua.... mimi nina vifaranga chotara hapa wiki 2 nawalisha starter bado ila watakaototolewa na hawa najiandaa kuchanganya mwenyewe nitaleta feedback hapa
 
Ni kweli naelewa unatakiwa uchanganye kwa mashine, unaweza nunua kila kitu na vikorokoro vingine ukaongezewa kwenye mashine zinazosaga wakakusagia ukapaki mifuko yako, saizi ya punje itakuwa ngumu kama unatumia kinu na sio mashine. Namsoma amesema alinunua kinu.... alternatively kuna maduka ya vyakula huwa yanauza mahindi yaliyoparazwa na vikorokoro vingine vingi, vifaranga wanahitaji vitu vyote muhimu kwani wanakua haraka. Kuna formula zinataja damu, mabaki ya samaki, majani yaliokaushwa, premix, kwa v iwango tofauti sasa kama vikizidi au kupungua.... mimi nina vifaranga chotara hapa wiki 2 nawalisha starter bado ila watakaototolewa na hawa najiandaa kuchanganya mwenyewe nitaleta feedback hapa
Nasubiri kusikia kutoka kwako.hayo Maduka yanauza mahindi yaliyoparazwa Kwaajili ya kuku wakubwa.ukijaribu kuchanganya mchanganyiko wako kwa ajili ya vifaranga hawataweza kula kwani mahindi yanakuwa makubwamakubwa sana.mchanganyiko ambao unaweza kuchanganya na kuku wasipate tabu ni kuku wakubwa.
 
Kuna mashine ya kuchanganyia chakula cha kuku na niliiona 8-8.nahisi ndo inatakiwa kutumika wakati wa kuchanganya chakula hicho

Ya zipo hizi masjine na kuna jamaa yuko arusha anaziunda, kuna ya tani Moja hadi Tano, mkitaka contact zake nitawapatia
 
mkuu hii shule ni kubwa sana ambayo kitendo cha kuwa na uzoefu wa kutoka field kabisa sio wa kusimuliwa kwa nadharia.naomba nikiri mi mwenyewe nimekuwa muhanga wa vifo vya vifaranga na nilikuwa nawapa chakula nilichochanganya kwa mkono.Hongera mkuu

Mkuu kuna Ile Manula ya RLDC kama sijakosea speling, wana manual nzuri sana ya jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku, niliipenda sana Manual yao, na kuna moja wa Kenya nao walikuwa na ya maelezo ya kila chakula na altenative yake, ukisoa Damu utumie nini, ukikosa hiki utumie nini,
 
Mama Joe kwenye chakula na hicho kipindi cha mwezi mmoja wa kwanza kweli kuna changamoto.na nahisi tatizo sio kuweka kila kitu na kwa ratio inatakiwa.Inawezekana matatizo yakawa mawili makubwa.mosi, ni size ya punje za mahindi, dagaa na pumba.katika hali ya uchanganyaji wa mikono ni ngumu hivi vitu kusagika na kuwa katika punje ndogondogo kwa kifaranga wa siku moja hadi wiki tatu kuweza kula.mara nyingi inatokea punje za mahindi ni kubwa hata kama zimeparazwa.Tatizo la pili nahisi ni uchanganyaji wenyewe mana kwa kuchanganya na mikono ili vichanganyio vyote vichanganyike vizuri nayo sio rahisi sana hata kwa kuchanganya kilo 50 tu.Kwa mtazamo wangu nahisi hivyo ndo vinavyochangia.Asante.

Katika Utengenezaji wa Chakula cha Kuku, Kwenye vifaranga wa One day old, huwa inashauriwa kutumia Unga wa Dona ambao tiyali umesgwa ndo utumike badala ya Pumba,au mahindi, so kwenye kuchanganya unashauriwa kutumia unga wa Dona, Ila hakikisha mahindi hayana Dawa make unaweza ua vifaranga,

Ukiachiulia mabali formula ya ratio ya kila kimoja, kwenye ku changanya napo kuna Formula ya Kuchanganya si kuchanganya tu ilimuradi unachanganya, Kuna makundi unatakiwa kugawa vyakula katika makundi kama mawili hivi na kila kundi lina changanywa kivyake na mwisho unacompail pamoja hayo makundi mawili

 
Back
Top Bottom