Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona haujarudi tena?unatuweka roho juu kila wakati kuchungulia hapa Kama umerudi,tupe shule bwanaMasimulizi yangu jana niliwagusia kuwa nilikuwa nina banda kubwa lenye chumba na sebule, pia nilikuwa nina JELA ambapo mwanzoni nilitumia matenga au mabox! Baada ya kuanza kutotolesha vifaranga, ilibidi nijenge kibanda cha kukuzia vifaranga (Nursery)! Kilikuwa kibanda kidogo kidogo tu mfano wa kigorofa hivi nitaelezea siku nyingine nilivyokitengeneza na mchoro wake mtauona. Picha ya Kuku niliewaonyesha huko nyuma yumo ndani ya moja ya vyumba sita ambapo vyumba vitatu viko chini na vitatu viko ghorofani. Vyumba hivyo vilikuwa vya kukuzia vifaranga.
Mara baada ya kutotolewa kwenye banda kubwa vifaranga na mama zao niliwahamishia kwenye hii nursery. Kila chumba niliweka chakula na maji ya kutosha siku nzima kila siku asubuhi. Kuku walikuzwa humo kwa muda wa mwezi mmoja ambapo baada ya vifaranga kuota manyoya mwili mzima ndipo mama zao niliwatoa. Kisha hawa vifaranga wakubwa ambao nitakuwa nawaita VINYOYA niliwasambaza wote kwenye vyumba vingine vitano na nilibakisha chumba kimoja tu ambacho ndiyo hicho nilikitumia kama JELA! Nilishawaelezea tayari juu ya matumizi ya hii Jela.
Hao VINYOYA baada ya kuwatengenisha na mama zao niliwaacha wiki moja kisha nao nikawa nawafungulia waanze kuokoteza chakula na kuchunga. Wakati huu kwenye banda kubwa kulikuwa na kuku wanaoatamia ambao niliwawekea mayai siku 10 baada ya kutotolewa hawa VINYOYA! Kwa hiyo kwa kujua kuwa kuna vifaranga ambao wangetumia hii nursery hapo baadae, ilibidi nijenge banda lingine kwa ajili ya kuwakuzia hawa Vinyoya. Baada ya kuwahamishia hawa vinyoya kwenye banda lao nilikuwa ninawaaacha hadi miezi miwili au zaidi kabla ya kuwahamishia kwenye banda kubwa.
Hadi kufikia hapo mzunguko wangu wa mabanda ya kuku ukawa umekamilika! Yaani nilikuwa na banda kubwa sebuleni kwa ajili ya kulala na kutaga kuku wakubwa, chumbani kwa ajili ya kuatamia na kutotoleshea, banda la kukuzia vifaranga (nursery) na banda la kukuzia vinyoya. Vipimo na michoro na vifaa nilivyotumia kujenga miundombinu hii itakuja peke yake na siku yake itawadia.
Wana JF kuna mtoto hapa nilipo kaja kuniambia kwamba huko kijiweni kwangu (porini) kimenuka, tanuru langu la mkaa limeachia mwee, ngojeni nikimbie nikalizibe nitarudi baadae mwenye maswali atupie, nikirudi nitakuja yajibu au mwenye mchango tushirikishane! ITAENDELEA……!
Nasubiri kusikia kutoka kwako.hayo Maduka yanauza mahindi yaliyoparazwa Kwaajili ya kuku wakubwa.ukijaribu kuchanganya mchanganyiko wako kwa ajili ya vifaranga hawataweza kula kwani mahindi yanakuwa makubwamakubwa sana.mchanganyiko ambao unaweza kuchanganya na kuku wasipate tabu ni kuku wakubwa.Ni kweli naelewa unatakiwa uchanganye kwa mashine, unaweza nunua kila kitu na vikorokoro vingine ukaongezewa kwenye mashine zinazosaga wakakusagia ukapaki mifuko yako, saizi ya punje itakuwa ngumu kama unatumia kinu na sio mashine. Namsoma amesema alinunua kinu.... alternatively kuna maduka ya vyakula huwa yanauza mahindi yaliyoparazwa na vikorokoro vingine vingi, vifaranga wanahitaji vitu vyote muhimu kwani wanakua haraka. Kuna formula zinataja damu, mabaki ya samaki, majani yaliokaushwa, premix, kwa v iwango tofauti sasa kama vikizidi au kupungua.... mimi nina vifaranga chotara hapa wiki 2 nawalisha starter bado ila watakaototolewa na hawa najiandaa kuchanganya mwenyewe nitaleta feedback hapa
Kuna mashine ya kuchanganyia chakula cha kuku na niliiona 8-8.nahisi ndo inatakiwa kutumika wakati wa kuchanganya chakula hicho
mkuu hii shule ni kubwa sana ambayo kitendo cha kuwa na uzoefu wa kutoka field kabisa sio wa kusimuliwa kwa nadharia.naomba nikiri mi mwenyewe nimekuwa muhanga wa vifo vya vifaranga na nilikuwa nawapa chakula nilichochanganya kwa mkono.Hongera mkuu
Naomba hayo mawasiliano.Ya zipo hizi masjine na kuna jamaa yuko arusha anaziunda, kuna ya tani Moja hadi Tano, mkitaka contact zake nitawapatia
Mama Joe kwenye chakula na hicho kipindi cha mwezi mmoja wa kwanza kweli kuna changamoto.na nahisi tatizo sio kuweka kila kitu na kwa ratio inatakiwa.Inawezekana matatizo yakawa mawili makubwa.mosi, ni size ya punje za mahindi, dagaa na pumba.katika hali ya uchanganyaji wa mikono ni ngumu hivi vitu kusagika na kuwa katika punje ndogondogo kwa kifaranga wa siku moja hadi wiki tatu kuweza kula.mara nyingi inatokea punje za mahindi ni kubwa hata kama zimeparazwa.Tatizo la pili nahisi ni uchanganyaji wenyewe mana kwa kuchanganya na mikono ili vichanganyio vyote vichanganyike vizuri nayo sio rahisi sana hata kwa kuchanganya kilo 50 tu.Kwa mtazamo wangu nahisi hivyo ndo vinavyochangia.Asante.
Naomba hayo mawasiliano.
Nashukuru kwa kujali:smile:Ngoja niyatafute then nita Ku PM