Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Je unawapatiaje joto? Inabidi uweke taa za umeme ama vipi?

Mdau No admission, soma kwa makini masimulizi yangu kuhusu ukuzaji wa vifaranga, nimesimulia joto la vifaranga lilipatikana kutoka kwa mama zao na wao vifaranga wenyewe kwa wingi wao huzalisha joto la kubwa la kutosha. Nakuomba usome taratibu na kwa umakini simulizi hii kuanzia mwanzo, lazima kuna kitu utaokota tu kitakachokuongezea pale ulipofikia.
 
Kubota pole na mikaa, hawa kienyeji wako pure wanachukua muda gani hadi kuuzwa au kutaga. Hawa hybrid miezi sita kutaga ila majogoo wanaendelea kukua. Na wanakoma kutaga umri gani?

Yaani Mama Joe mpendwa yaani hapa hadi najiona ujinga! Kwa hilo kwa kweli sijawahi kufuatilia! Yaani mwenyewe nilichukulia tu mazoea kwamba wanachukua miezi sita hadi kutaga! Ni hao kuku maarufu wa Morogoro, vifupi vinamiili midogo midogo lakini kwa kutaga mayai wee acha tu kuku hawa wanajituma, Mkuu Malila anawajua jina la hawa kuku, nimelisahau. Next time nitachukua record ya muda wa kufikia kutaga. Kwenye mkaa Bwanamiti karibia mwisho wa mwezi kaishiwa pesa anasumbua sana, wanasumbua kama matrafik barabarani, nimepumzika wapokee mshahara kwanza lol.
 
Ndugu zangu mimi ninapata tabu sana ninapotaka kuwatengenezea kuku wangu funza au mchwa kwani bado sijaelewa vizuri namna ya kuwatengeneza hawa wadudu.naomba mwenye ujuzi huo anipige msasa kidogo.

Mama Timmy umeuliza kitu muhimu sana, protein ni kitu muhimu sana kwa hii mifugo! Wengine huwa wanatumia damu, jamani mnaojua hii kitu msaada!
 
Mama Timmy umeuliza kitu muhimu sana, protein ni kitu muhimu sana kwa hii mifugo! Wengine huwa wanatumia damu, jamani mnaojua hii kitu msaada!
Mchwa nilielekezwa nichanganye samadi ya ng'ombe na majani makavu halafu ni nyunyuzie maji kidogo.mchanganyiko huo niufunikize chini ila aliyenipa somo Hilo hakumalizia nikae muda gani mchwa watakuwa tayari.nawaogopa hawa wadudu kwani wanaweza geukia Banda langu likaisha lote.funza ndo bado kabisa.naomba nielekezwe vzr ili niifanyie kazi Hiyo shule
 
Ndugu zangu mimi ninapata tabu sana ninapotaka kuwatengenezea kuku wangu funza au mchwa kwani bado sijaelewa vizuri namna ya kuwatengeneza hawa wadudu.naomba mwenye ujuzi huo anipige msasa kidogo.

Mama timmy, pole na kupata tabu ya kutengeneza funza.mimi nilikuwa natumia mbolea ile ile ya kuku na pumba za mahindi.kuna dumu la lita 20 nimelikata juu kote uwa naanza kuweka bolea kama nusu na juu na weka pumba nusu ya kiwango cha mbolea nilichoweka.Baada ya hapo namwangia maji hadi kunalowana kabisa, nafanya zoezi la kumwagia maji kwa siku 2 halafu siku ya 3 simwagii then siku ya 4 unakuta funza wameshapatikana wa kutosha naewapa kuku.Njia nyingine ambayo ina gharama kidogo ni ya kutumia pumba na utumbo au nyama zile ambazo hazifai kuliwa.unachanganya hizo nyama au utumbo na pumba halafu unamwagia maji kiasi hadi vilowane kwa siku 3 hadi 5.Karibu.
 
Wao!nashukuru sana ndugu yangu Dafo.nilikuwa natamani sana kujua kuwatengeneza hawa funza!nitaleta mrejesho wake hapa hapa jamvini!
 
ImageUploadedByJamiiForums1361462821.254335.jpg

Mkuu Tunashukuru sana kwa Semina Yako tumejadiliana na Mama Yoyoo tukaona ni bora tuboreshe Banda letu la Kuku tumefanya la Kisasa kama unavyoliona
 
View attachment 84075

Mkuu Tunashukuru sana kwa Semina Yako tumejadiliana na Mama Yoyoo tukaona ni bora tuboreshe Banda letu la Kuku tumefanya la Kisasa kama unavyoliona

wewe kweli mjasiriamali kama bwana kubota na mama timmy kila mfugo na zao wanapenda hawa ndio wajasiriamali sasa hawana utani katika maswala ya msingi big up and keep it up kubota na mama timmy
 
View attachment 84075

Mkuu Tunashukuru sana kwa Semina Yako tumejadiliana na Mama Yoyoo tukaona ni bora tuboreshe Banda letu la Kuku tumefanya la Kisasa kama unavyoliona

Kaaaaah! Umenitamanisha walaahi ningekuwa nalo banda kama hilo ningelifanya iwe nursery ya vifaranga iwe rahisi kwenda nalo kwenye matanuru yangu ya mkaa, asante kwa kuboresha maarifa!
 
Hakika toka mwanzo nilikuwa napata elimu hapa nilianza kufuga kuku wa kienyeji mwishoni mwaka jana na ukweli walikufa kuku kumi na kubaki na wiwili jogoo na tetea moja. Tetea lilitaga mayai nikaona niache mayai kumi tu yakaanguliwa yote. Ila ulikuja ugonjwa ambao nimeona hapo wengi wameonesha kuwa ni hatari wakiwa na mwezi mmoja walikufa japo niliwapa chanjo ya jicho. Sasa kilibaki kifaranga kimoja tu. Sasa nimenunua mitetea ambayo karibu inataka kuanza kutaga idadi kumi hivyo jana mmoja kapotea kwani naacha wajitafutie chakula na kuwaongezea chakula cha ziada. Kwa utaalamu ninaoupata hapa najua wazi kuwa nitafanikiwa japo banda la kuku sasa hivi linakuwa na mbu wengi sana je hawawezi kuwathiri kuku wangu? Na mara nyingi naona kuku wanajikuna nini tatizo?
 
Jamani kuku (wadogo) wangu wana ugonjwa wa macho kutoa usaha, nategemea kwenda kucheck dawa duka za mifugo but kama kuna mzoefu naomba ushauri wa dawa/tiba
 
Mtaalamu itakuwaje kuku nikiwanynyoa mabawa ili wasiruke fensi? Maana wanaruka na mmoja kapotea
 
nasubiri muendelezo mkuu Kubota, hii wikiend ulisema utarudi kuendelea pale ulipoishia
 
nasubiri muendelezo mkuu Kubota, hii wikiend ulisema utarudi kuendelea pale ulipoishia

Ni kweli mkubwa Singo, nitatimiza ahadi! Nakushukuru kwa kufuatilia, unanitia hamasa mkuu!
 
Back
Top Bottom