Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 533
- 1,101
Mtaalamu itakuwaje kuku nikiwanynyoa mabawa ili wasiruke fensi? Maana wanaruka na mmoja kapotea
Mimi nilikuwa nikitumia mkasi mkali kuyanyoa yale manyoya marefu kwenye bawa. Ukiyakata nusu ya urefu wa yale manyoya, bawa moja tu ndege haruki maana unakuwa umemharibia balansi! Ukimnyonyoa utakuwa umetatua tatizo kwa muda mfupi tu maana yataota tena mengine, ukimnyonyoa pia unamhatarisha kuku anaweza akapata magonjwa kupitia vidonda yaliyoachwa na manyoya uliyonyonyoa na unapomnyonyoa kuku unamtia stress kubwa sana jamani ni sawa na wewe unyonyolewe ndevu kwa kupunyua ndevu moja moja, yaani huwa hatujuagi tu tunavyowaumiza kuku kwa kuwanyonyoa, kwanza hata wao huwa wanalia sana kuonyesha maumivu makali na damu huwa inawatoka! Kama ni kuku mtagaji anaweza kususia, kama ni mwatamiaji anaweza kususia kama ni Jogoo ......! Hebu chukua mkasi na kata nusu ya urefu wa manyoya yale marefu kwenye bawamoja tu wanafanya hivyo hadi Ulaya, kuku haruki!