Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Mtaalamu itakuwaje kuku nikiwanynyoa mabawa ili wasiruke fensi? Maana wanaruka na mmoja kapotea

Mimi nilikuwa nikitumia mkasi mkali kuyanyoa yale manyoya marefu kwenye bawa. Ukiyakata nusu ya urefu wa yale manyoya, bawa moja tu ndege haruki maana unakuwa umemharibia balansi! Ukimnyonyoa utakuwa umetatua tatizo kwa muda mfupi tu maana yataota tena mengine, ukimnyonyoa pia unamhatarisha kuku anaweza akapata magonjwa kupitia vidonda yaliyoachwa na manyoya uliyonyonyoa na unapomnyonyoa kuku unamtia stress kubwa sana jamani ni sawa na wewe unyonyolewe ndevu kwa kupunyua ndevu moja moja, yaani huwa hatujuagi tu tunavyowaumiza kuku kwa kuwanyonyoa, kwanza hata wao huwa wanalia sana kuonyesha maumivu makali na damu huwa inawatoka! Kama ni kuku mtagaji anaweza kususia, kama ni mwatamiaji anaweza kususia kama ni Jogoo ......! Hebu chukua mkasi na kata nusu ya urefu wa manyoya yale marefu kwenye bawamoja tu wanafanya hivyo hadi Ulaya, kuku haruki!
 
Jamani kuku (wadogo) wangu wana ugonjwa wa macho kutoa usaha, nategemea kwenda kucheck dawa duka za mifugo but kama kuna mzoefu naomba ushauri wa dawa/tiba

Subiri wakati wa kulijadili umewadia, stay tuned ukizingatia wataalamu wa tiba mbadala Mama Timmy na Mama Joe wapo standby hakuna kitakachoharibika!
 
Hakika toka mwanzo nilikuwa napata elimu hapa nilianza kufuga kuku wa kienyeji mwishoni mwaka jana na ukweli walikufa kuku kumi na kubaki na wiwili jogoo na tetea moja. Tetea lilitaga mayai nikaona niache mayai kumi tu yakaanguliwa yote. Ila ulikuja ugonjwa ambao nimeona hapo wengi wameonesha kuwa ni hatari wakiwa na mwezi mmoja walikufa japo niliwapa chanjo ya jicho. Sasa kilibaki kifaranga kimoja tu. Sasa nimenunua mitetea ambayo karibu inataka kuanza kutaga idadi kumi hivyo jana mmoja kapotea kwani naacha wajitafutie chakula na kuwaongezea chakula cha ziada. Kwa utaalamu ninaoupata hapa najua wazi kuwa nitafanikiwa japo banda la kuku sasa hivi linakuwa na mbu wengi sana je hawawezi kuwathiri kuku wangu? Na mara nyingi naona kuku wanajikuna nini tatizo?

Zipuwawa hapa umenipa hasira ni eneo moja wapo huwa tunapitiwa sana kushughurika nalo tunapowaona kuku wanajikuna tunafikiri walizaliwa kujikuna, yaani ni kawaida yao, stay tuned nakuja na stori nzima nzima ya hao maadui. Usichoke wala usichukie, subiri story kamili!
 
mkuu kubota naomba unijuze zaidi kuhusu aina ya kuku ambayo ni nzuri. kwa maana ya mbegu

Mheshimiwa Rais wa walalahoi, rais wangu, uzuri wa aina unategemea unavutiwa na nini! Uzuri kwa kibiashara, au kupendezesha macho au uzazi, au utamu wa nyama yake n.k Kuna wajuzi nimewahi kukuta thread humu JF wamewataja kuku aina mbali mbali na sifa zake! Mimi nimewahi kujaribu aina tatu tu, hao andunje wa mororogoro, kuku wa malawi na Kuchi! Kuku wa Malawi sitaki tena kwa vile siyo kuku wa kienyeji, Kuchi pamoja na sifa zao nyingi lakini wanakua pole pole sana sanaaaaa! Kuchi anatafuna chakula ukisafiri mwezi ukirudi yuko vile vile! Aka siwataki! Labda ukiwafanya Chotara! Ila kuna kuku wa kienyeji nimewahi kuwaona wazuri wakubwa na wanaukuaji mzuri tu, pia nimewahi kuona jirani yangu mmoja aliwahi kufuga chotara wa broiler kwa kweli nilivutiwa sana. Mwelekeo wangu hivi sasa ni kutambua aina nzuri ili nianze ufugaji mkubwa wa kuku wa kienyeji, eka moja nawamwaga kuku 250 nawaacha wanahangaika wenyewe kuchunga, nitahitaji eka 4 kufuga kuku 1000 ! Ardhi ya kufugia kuku Tanzania mbona ipo, ninaweza nisipate ardhi bora ya kusitawisha nyanya chungu lakini siwezi kukosa ardhi ya kuku wangu kuokotea panzi na mchwa lol! Tuombeane uzima tutapeana updates hapa hapa!
 
Habari zenu wana JF,
Hongera sana Kubota kwa kuanzisha huu uzi pia na wachangiaji wote.

Umegusia Kuwa unafikiria kuanza ufugaji kwa kuanza na kuku 250 Ndan ya ekari moja na baadaye ekari nne. Swali langu ni namna gani utapambana na maadui mf: paka, panya, Mbwa, n.k yaan Wale wote wanaoweza kuwadhuru kuku.

Asante!
 
Swali lako zuri sana na linafanana sana na Zipuwawa, utanifanya nipakue bado mbichi! Hahahaaa! Ninakuja mkubwa wangu umeulizia kitu moja ya vitu lazima niseme nisije kufa nayo nilikuta mama mmoja JASILI sitamsahau ndipo nilinunua kuku mbegu 30, japo alininyonyoa kikwelikweli kwa kuniuzia bei moja ya kuku awe kuku mkubwa au mdogo maana alisema hakuwa amepanga kuuza kwa wakati huo akisubiria wakue apate timiza malengo yake. Nilisema sawa tu maana nilikuwa natafuta mbegu. Huyu Mama alishaondokana na kuhofia hao maadui, nilijifunza mkakati wake kupambana na maadui yaani nilisisimka, ninakuja subiri! Kaka uandishi ni mgumu msione ninachelewa kupost niko na nyinyi, sipendi nilete kitu mbichi nitawakwaza great thinkers hapa JF! Ninaweza kuwa nasimulia kitu halisia lakini kama nisipo edit vizuri inaweza kuja kueleweka vibaya ikaonekana ni uzushi tu. Just a moment mkuu wangu ndege itatua tu!
 
Zipuwawa hapa umenipa hasira ni eneo moja wapo huwa tunapitiwa sana kushughurika nalo tunapowaona kuku wanajikuna tunafikiri walizaliwa kujikuna, yaani ni kawaida yao, stay tuned nakuja na stori nzima nzima ya hao maadui. Usichoke wala usichukie, subiri story kamili!
asante sana naongoja......na kama ningekuwa najua kuweka picha ningeweka aina ya kuku ninao wafuga
 
Kubota; Upo? Usisite kupitia anga hii Kamanda wetu!
Tu pamoja na hata ningependa kumwona member RETI; katika moja ya maoni yake.

Pamoja sana!
 
Last edited by a moderator:
Yaani Mama Joe mpendwa yaani hapa hadi najiona ujinga! Kwa hilo kwa kweli sijawahi kufuatilia! Yaani mwenyewe nilichukulia tu mazoea kwamba wanachukua miezi sita hadi kutaga! Ni hao kuku maarufu wa Morogoro, vifupi vinamiili midogo midogo lakini kwa kutaga mayai wee acha tu kuku hawa wanajituma, Mkuu Malila anawajua jina la hawa kuku, nimelisahau. Next time nitachukua record ya muda wa kufikia kutaga. Kwenye mkaa Bwanamiti karibia mwisho wa mwezi kaishiwa pesa anasumbua sana, wanasumbua kama matrafik barabarani, nimepumzika wapokee mshahara kwanza lol.

Nahisi unazungumzia vishingo ni wadogo na ni wazuri sana kwa utagaji
 
Yaani Mama Joe mpendwa yaani hapa hadi najiona ujinga! Kwa hilo kwa kweli sijawahi kufuatilia! Yaani mwenyewe nilichukulia tu mazoea kwamba wanachukua miezi sita hadi kutaga! Ni hao kuku maarufu wa Morogoro, vifupi vinamiili midogo midogo lakini kwa kutaga mayai wee acha tu kuku hawa wanajituma, Mkuu Malila anawajua jina la hawa kuku, nimelisahau. Next time nitachukua record ya muda wa kufikia kutaga. Kwenye mkaa Bwanamiti karibia mwisho wa mwezi kaishiwa pesa anasumbua sana, wanasumbua kama matrafik barabarani, nimepumzika wapokee mshahara kwanza lol.

Asante ila umenichekesha kumbe kuna traffic msituni yaani kila mahali sijui twende wapi, humu kuna mabwana misitu pia watakuibukia idadi ya malipo kwa mwezi itaongezeka
mimi kienyeji pure ninachowahofia hayo maumbo yao madogomadogo yaani hapo unabembeleza mteja hadi basi ila mayai najua wenye maumbo madogo wanataga sana yale mayao madogomadogo, ngoja tusubiri wengine wenye michango zaidi
 
Naona kuna mkanganyiko wamagonjwa kupitia wadau mbalimbali, kutokana na uzoefu wangu kuku wanawezakuumwa ugonjwa tofauti lakini wakawa na dalili mojawapo inafanana:
naomba kuongelea magonjwa mawili matatu yenye kusababisha vifo vingi na dalilizake

1. Newcastle/ mdondo/kideri (Virus)

Dalili
• Vifo vya ghafla vyaidadi kubwa ya kuku katika shamba/banda
• Kuku wanatetemeka nakushindwa kutembea
• Kuku hupooza miguu, mabawa na kupinda shingo; na hujizungusha mahalialipo
• Kuku huharisha kinyesicha kijani na wakati mwingine chenye mchanganyiko wa rangi ya njano
vifaranga vifo hadi 100% wakubwa 20%

Tiba: hakuna ila chanjokwenye maji ya kunywa, kuna antibiotic wanapewa

2. Fowl typhoid (Bacteria)
Dalili
Kuku wakubwa
• Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano
• Vifo vya ghafla
• Kupauka kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu
•
Manyoya hutimka, hushushambawa, hufumba macho na kuzubaa (kuvaa koti)
Vifaranga

• Vifaranga wanatotolewawakiwa wamekufa au dhaifu
• Hujikusanya pamoja nakukosa hamu ya kula
• Kinyesi cha rangi yanjano na huganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
• Hupumua kwa haraka nakwa shida
• Vifo vingi huweza kutokea kuku wasipotibiwa
Tiba
• Yapo madawa mengi aina ya antibiotiki ambayoyanaweza kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa.
Lakini madawa haya hayawezi kumaliza kabisa ugonjwakutoka shambani.
• Pata ushauri wadaktari

3. Coccidiosis (Protozoa)

Dalili
· Kuhara damu au kinyesi cha kahawia
• Mbawa kushuka
• Kuzubaa na kuachakutaga
• Kukosa hamu ya kula
• Kupunguza kasi yaukuaji na uzito
• Kwa kawaida vifo ni vingi

Tiba
• Amprolium hydrochloride
• Sulfa
• Pataushauri wa daktari

Source: vitabu lakini mimi mwenyewe na kuku wangu pia

Asante Sabayi kwenye chotara wa RETI nimepata vishingo wawili tuombe tu wafikie ukubwani nipate mbegu yao pia

Umecross breed Chotara na Vishingo? Nilishawahi kuwafuga hawa vishingo nikiwa mwanafunzi walikuwa wanataga hadi kero.ni wazuri sana najipanga nianze kuwafuga kibiashara sasa unaweza ukawa na Vishingo wengi kwa ajili ya kuuza mayai tu (bei ya mayai ya kienyeji ni nzuri sana na demand ipo juu) na ukafuga chotara kwa ajili ya kuwauza wao wenyewe
 
Asante Sabayi, RETI ndio kaniapatia vifaranga chotara na wawili nimeshangaa ni vishingo ila kwa vile ni cross breeding sishangai na nimefurahi kuwa breed tofauti tofauti nijifunze ipi nzuri zaidi kuiendeleza baadae. Naendelea kujifunza kwenu hapa
 
Mama Joe;

Hakika uko vizuri Best yangu! Nategemea leo mpaka kesho kupata vifaranga isiyopungua 50 kutokana kuku 4 wanaolalia!
Hebu niambie niambie niwanunulie chakula gani tofauti na starter niliokuwa nawapaga?

Naona kuna mkanganyiko wamagonjwa kupitia wadau mbalimbali, kutokana na uzoefu wangu kuku wanawezakuumwa ugonjwa tofauti lakini wakawa na dalili mojawapo inafanana:
naomba kuongelea magonjwa mawili matatu yenye kusababisha vifo vingi na dalilizake

1. Newcastle/ mdondo/kideri (Virus)

Dalili
 Vifo vya ghafla vyaidadi kubwa ya kuku katika shamba/banda
 Kuku wanatetemeka nakushindwa kutembea
 Kuku hupooza miguu, mabawa na kupinda shingo; na hujizungusha mahalialipo
 Kuku huharisha kinyesicha kijani na wakati mwingine chenye mchanganyiko wa rangi ya njano
vifaranga vifo hadi 100% wakubwa 20%

Tiba: hakuna ila chanjokwenye maji ya kunywa, kuna antibiotic wanapewa

2. Fowl typhoid (Bacteria)
Dalili
Kuku wakubwa
 Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano
 Vifo vya ghafla
 Kupauka kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu

Manyoya hutimka, hushushambawa, hufumba macho na kuzubaa (kuvaa koti)
Vifaranga

 Vifaranga wanatotolewawakiwa wamekufa au dhaifu
 Hujikusanya pamoja nakukosa hamu ya kula
 Kinyesi cha rangi yanjano na huganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
 Hupumua kwa haraka nakwa shida
 Vifo vingi huweza kutokea kuku wasipotibiwa
Tiba
 Yapo madawa mengi aina ya antibiotiki ambayoyanaweza kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa.
Lakini madawa haya hayawezi kumaliza kabisa ugonjwakutoka shambani.
 Pata ushauri wadaktari

3. Coccidiosis (Protozoa)

Dalili
· Kuhara damu au kinyesi cha kahawia
 Mbawa kushuka
 Kuzubaa na kuachakutaga
 Kukosa hamu ya kula
 Kupunguza kasi yaukuaji na uzito
 Kwa kawaida vifo ni vingi

Tiba
 Amprolium hydrochloride
 Sulfa
 Pataushauri wa daktari

Source: vitabu lakini mimi mwenyewe na kuku wangu pia

Last edited by a moderator:
Mimi nimevutiwa sana na hii thred, nilikuwa na mpango wa kufuga kuku wa kienyeji muda kidogo na nikanunua eka 2.5 kigamboni ndio naweka sehemu ya kukaa nihamie nianze ufugaji wangu. Ila muanzishaji mada na wachangiaji kwa kweli ni kitu kizuri sana mmefanya. Nazani itatusaidia sana tunaotaka kuanza ufugaji huu. Na pia kuwatia moyo vijana kufikilia upande huo kwa ajira binafsi.
 
Mi naona Kubota; atakuwa amezidiwa na maliasili kuhusu uchomaji wa mkaa! Kha ha ha ha ha haaaaaaa!

Kubota; hebu zunguka kipande hii kwani Mama timmy; ana kitu cha kukuuliza!

Kwi kwi kwiiii kama ungeniona ungenionea huruma. Mkuu nilianzisha ka hobby kengine huko msituni kwenye mikaa yetu nikajikuta nimekuwa mteja wa Bwana Nyama, mkuu hawa jamaa wanachojua wao ni kupigisha kwata tu! Lakini nashangaa mbona tembo wanaisha tu. Hapa bado nakandwa maji hali mbaya!
 
Back
Top Bottom