Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wadau kwa ujumla na wakuu Malamsha Shao, LiverpoolFC, Sabayi tuko pamoja! Mama Joe shukrani kwa kutujuza kuhusu magonjwa, Mama Timmy mchuzi ukiganda tutauchemsha tu hadi kieleweke! Mkuu LiverpoolFc ulikuwa umeulizia kuhusu chakula cha kuwapa vifaranga wako, iwapo kama hujafanikisha kwa kutumia chick marsh sidhani kama kutakuwa na jibu lingine tena! Tunapokabiriana na vifo vya vifaranga visababishi huwa ni vingi sana ikiwano na chakula duni, chick marsh kama hakijachakachuliwa, ndiyo excellent feed kwa vifaranga.

Na hadi kufikia sasa wakati nikisubiria ujanja mwingine nitaendelea kununua Chick marsh! Kuna ukimya hapa jukwaani iwapo kama kuna mdau aliefanikiwa kukuza vifaranga hadi umri wa wiki sita kwa chakula alichojitengenezea mwenyewe! Ukimya huu ni dhahiri kuwa hii ni changamoto kubwa sana! Sisemi kuwa hili haliwezekani wala sisemi hakuna anaeweza, wapo wanaoweza, ndiyo maana tuko hapa jukwaani kupeana uzoefu na kuelezana wapi tunakwama! Mimi nilishindwa kujitengenezea kama nilivyowasimulia huko nyuma, nikaamua kwa kuwakuza kuku kwa ule mwezi wa kwanza ninanunua chick marsh! Tutashukuru kupata wazo namna ya kupata ufumbuzi wa jambo hili, tumeambiwa mfuko wa chick marsh unafika hadi Shs alfu 40! Kwa hiyo kuweza kumudu kujitengenezea chakula hasa cha kuinulia vifaranga ni ukombozi mkubwa, mimi nilishashindwa kwa hili nilishaliweka wazi , na mkuu DAFO nae pia alikiri kuwa hii ni changamoto kubwa!

Nimesharudi nakuja kama ifuatavyo:
Magonjwa: Kabla sijaendelea kusimulia yaliyonikuta naomba niongee nadharia kwanza kuhusu mtazamo wangu nikilinganisha ufugaji wa kuku wa kienyeji na ule ufugaji wa kuku wa kisasa..............
 
kuna thread nying tu zinatoa ama kuelekeza namna ya kufanya so umechelewa:A S 114::A S 114::A S 114:
 
Naaaam! Kubota; hakika ulikuwa busy sana na hata hivyo pole na mahangaiko ya kibinadamu Ndg yangu!
Hivi katika hali kutaka kuboresha kitu chochote ni lazima mlengwa uwe karibu sana na tukio!
Hebu niambie Ndg yangu Kubota; ni vyombo gani itafaa kwa hawa vifaranga?
 
Last edited by a moderator:
Naaaam! Kubota; hakika ulikuwa busy sana na hata hivyo pole na mahangaiko ya kibinadamu Ndg yangu!
Hivi katika hali kutaka kuboresha kitu chochote ni lazima mlengwa uwe karibu sana na tukio!
Hebu niambie Ndg yangu Kubota; ni vyombo gani itafaa kwa hawa vifaranga?

Kama nimekuelewa vizuri vyombo kwa ajili ya vifaranga
(1) vyombo vya maji visivyomwaga mwaga, kama hali inaruhusu nunua vile spesho vya ujazo wa lita 2 hadi 3 kisha
ukivijaza maji dumbukiza vikokoto visafi mle kwenye maji ili vifaranga wasidumbukize miguu.
(2) Kwa siku za mwanzo weka chakula kwenye kibeseni, naomba rejea kuna picha ya nyuma niliweka picha ya kuku
mwenye vifaranga utaona mfano wa chombo, katikati ya kibeseni hicho weka kitu kizito kama jiwe hivi ili kuzuia mama yao asimwage chakula kwa kupekua na reki zake au akikanyaga kingo za chombo! Upotevu wa chakula kwa kumwagwa mwagwa na kuku ni moja ya hasara za kukwepa ili kupata faida. Mimi hupendelea vyombo ambavyo nikijaza asubuhi ndiyo hadi kesho tena siyo kurudi rudi kila mara kuongezea maji na chakula.
 
LiverpoolFC hongera kwa kutarajia vifaranga, kama anavyosema Kubota bado chakula ni starter tu labda uweze kuchanganya starter yako mwenyewe kitu tulichosema tusubiri tuone itakuwaje, pamoja na suala la chakula lakini vifo vingi magonjwa nakushauri yale yanayoweza kuepukwa
1. Osha banda kwa V-rid na vyombo ulivyotumia kwa kuku wakubwa
2. wakiwa na siku tatu wape chanjo ya mdondo rudia wiki ya 3 na kila miezi 3
3. Ukiweza wape vitamini walau wiki 2 za mwanzo
4. wiki ya pili wape chano ya gumboro
5. unaweza kuwapa coccidiostat au ukaacha ila be on standby wakionyesha dalili za coccidiosis
6. kikubwa jitahidi usafi wa banda na vyombo epuka watu kuingia ingia na kushare vyombo na kuku wakubwa
7. ukiweza tumia waterguard walau wiki 2 za mwanzo kwenye maji, kizibo kwa lita 20 yanatumika hata siku 2
ngoja wengine wachangie hapa, mie wangu wanaendelea vizuri tu
 
Wadau kama nilivyodokeza kabla sijasimulia ile stori, ninaomba japo kwa ufupi niseme mtazamo wangu binafsi jinsi ninavyochukulia ufugaji wa kuku wa kienyeji ninapoulinganisha na ufugaji wa kuku wa kigeni (kisasa). Kwa uzoefu wangu nilichowahi kubaini ni kuwa ufugaji wa kuku wa kienyeji ambao nimewahi kuushuhudia ukiwa katika ustawi mkubwa na usiokuwa na changamoto ni ule wa kufugia kwenye maeneo ya wazi makubwa. Kwa mfano sehemu kwenye maeneo ya wafugaji wa ngombe wanaoishi pembezoni mwa miji au vijiji kwenye jamii za wafugaji kokote utakakokwenda nchini huko huwepo makundi makubwa ya kuku! Maeneo hayo ni mara chache sana kusikia yanakumbwa na mashambulizi ya magonjwa kama mdonde, kuhara damu au typhoid! Hii hutokana na ukweli kuwa maeneo hayo yamejitenga dhidi ya maambukizo. Changamoto kwao mara nyingi huwa ni wanyama kama nyoka, vicheche paka pori n.k.

Tunashuhudia vifo vingi sana vya vifananga na kuku wakubwa kwa sababu mazingira tunayowafugia kuku si toshelevu kwa ustawi wa kuku. Tunawafugia kuku kwenye mazingira ambayo kuna uhaba wa chakula unaochangiwa na kuwepo msongamano mkubwa wa kuku kwa eneo dogo. Kuku anaeshinda porini kwenye eneo kubwa anajipatia aina nyigi za chakula kwa hiyo suala la lishe si kikwazo kwa afya yake.

Kuku wanaofugwa sehemu za huko mashambani na maporini kwa wafugaji hustawi kwa kuwa kuna mazingira asili ambapo hawana tatizo la chakula na pia usafi ni wa hali ya juu kwani kila siku kuku hupita kwenye eneo ambalo ni kama jipya halijachafuliwa na kuku wengine na pia kinyesi chao hakilundikani sehemu ndogo bali kinasambaa eneo kubwa kiasi cha kutokuleta madhara ya maambukizi. Kwa hiyo tunapofuga kuku wa kienyeji eneo dogo au kama tunavyofanya kwa kuwafungia ndani ni changamoto kubwa sana.

Kwa hiyo ufugaji kuku wa mbugani kwa jamii za wafugaji ambako wanunuzi wa kuku wa kienyeji hueda kule kuzoa kuku kwa wingi umefanikiwa kwa vile kule kuku wanapata mazingira mazuri. Tunapoanza kuwafuga kuku hawa kwenye maeneo madogo kwa idadi kubwa changamoto ya magonjwa hutokea na husababishwa na matatizo ya lishe na mazingira machafu pia ukosefu wa hewa safi kwenye mazingira tunayowafugia. Vifo vingi vya kuku hasa vifaranga husababishwa na lishe duni hasa tunapojaribu kuwatengenezea chakula wenyewe ambacho mara nyingi huwa hakifikii viwango au tunapowaacha wajitafutie chakula wao wenyewe bila kuzingatia iwapo eneo husika linatosheleza kuwafanya kuku washibe.

Kwa hiyo tunapojitengenezea chakula na tukashindwa kufikia viwango husika kuku hasa vifaranga hupatwa na udhaifu mkubwa na upungufu wa kinga ya mwili kiasi cha kuanza kushambuliwa na magonjwa mbali mbali yakiwemo magonjwa ya macho na magonjwa mengine kadhaa. Tunapoona vifaranga wanakufa kwa wingi lazima tukumbuke kuwa lishe duni inaweza kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kuwafanya wapate maambukizi kirahisi! Hatua muhimu kupambana na magonjwa ya kuku wa kienyeji ni kuhakikisha wanapata lishe ya kutosha. BADO INAENDELEA .................
 
Ukiamua kufuga kwa kuachia kuku wachunge wenyewe hakikisha una eneo linalolingana na idadi yao vinginevyo hawatashiba matokeo yake ni kuku kuwa wepesi, utagaji kushuka na vifaranga kufa kwa wingi. Kuku wakubwa wanaweza wasife lakini vifaranga wanakufa kwa wingi. Pia kuku wakubwa unaweza kuwatengenezea chakula hata kisipofikia viwango hawaathiriki sana lakini vifaranga mara nyingi ikitokea chakula cha kujitafutia hakitoshi hapo ni kasheshe maana si kila mmoja anaweza kujitengenezea chakula chenye virutubisho vyote muhimu kama wanavyopata wanapookoteza wenyewe!

Tunapofuga kuku kibiashara huwatunalenga tuwe na kuku wengi na mara nyingi huwa tunawaacha wachunge eneo dogo ambalo halilingani na idadi yao. Au huwa tunawafungia ndani ili tuwahudumie kama inavyofanywa kwa kuku wa kisasa. Kuku wa kienyeji tunapowafungia kama kuku wa kisasa kwa kuwaweka ndani muda wote huwa tumewaweka kwenye mazingira magumu sana kwa afya zao. Kwanza hewa mara nyingi huwa imeharibika, mlundikano wa kinyesi huwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa.Kwenye ufugaji wa kisasa Wataalamu wameweza kutatua changamoto nyingi kwa kuboresha Aina za kuku kuweza kumudu mazingira ya msongamamo, kutengeneza chakula bora ambacho kuku anastawi vema hata bila kutoka nje, kuboresha mazingira anamoishi kuku na tiba za mara kwa mara. Ukifanya haya kwa kuku wa kienyeji si rahisi kupata faida maana wanakua taratibu sana na wanataga mayai kidogo sana.
Pamoja na bei ya kuku wa kienyeji kuwa kubwa bado hailipi kabisa iwapo mfugaji utaamua kuwafuga kuku hao kwa kutumia vifaa, mazingira na lishe kama ile ya kuku wa kisasa.

Ufugaji wenye faida kwa makundi makubwa ya kuku wa kienyeji ni kufuga eneo wazi kwa kuzingatia kutovuka idadi rasmi ya kuku kwa eneo. Kwa mfano eka moja inaweza kuhimili kuanzia kuku 250 hadi 400. Kwa hiyo kama unaeneo dogo jaribu kupiga mahesabu kwa kufuata uwiano huo.

Pia ufugaji wa makundi makubwa ya kuku wa kienyeji iwapo unaeneo dogo unaweza kumudu kwa kuwatenganisha vifaranga kama nilivyokuwa ninafanya na kuwapatia vifaranga mazingira na chakula bora kabisa pia kwa kutengeneza chakula cha ziada kwa kuku wakubwa kama nilivyofanikiwa kufanya. Ili wanapokwenda kuchunga wasiposhiba wanarudi kula chakula kilichopo tayari. Ikumbukwe kuwa ni mara chache sana kuku wa kienyeji kudhurika wanapokuwa wakubwa ukilinganisha na vifaranga. Hivyo nguvu kubwa lazima ielekezwe kwa vifaranga maana hawa ndiyo chanzo cha kukua kwa kundi.

Baada ya nadharia hiyo ugonjwa wa mdonde (NCD)………..ITAENDELEA
 
Wana Jf,

Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

Stay tuned and keep on visiting this thread!!


===============
UPDATE
===============

TANESCO BWANA!, wanaweza kuwa wamesababisha kukatika kwa hii nyuzi. wakirudisha umeme nafikiri mkuu ataunganisha alipokomea.

waiting.....................................
 
Ugonjwa wa Mdonde: Kutokana na uwepo wa chanjo ya ugonjwa wa mdonde ugonjwa huu kwangu hakua tishio kabisa! Ilikuwa ni kawaida kuwapatia chanjo vifaranga mara tu wanapototolewa, nilikuwa natumia chanjo ya kuweka kwenye maji, niliipenda njia hii kwa vile ni njia rahisi zaidi kuliko ile ya kuweka jichoni kuku mmoja mmoja. Kuna wakati nimewahi pia kuweka chanjo hiyo ya kuweka machoni. Chanjo hii ni madhubuti kwa vile haihitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu na hivyo inafaa kutumia vijijini na inawezekana ikawa si rahisi kuharibika.

Ukweli ni kuwa ikiwa mfugaji unawachanja vizuri kuku wako lakini bado unakutana na matatizo ya mdonde hii mara nyingi hutokana na chanjo uliyotumia kuwa ilikuwa imeshaharibika. Si rahisi kujua iwapo chanjo uliyotumia ni nzima au imeshaharibika! Ili kuepukana na hatari hii mimi nilikuwa ninawawekea chanjo kuku wangu kila wanapototolewa vifaranga na kwa vile chanjo hii ni ya maji na huwa ni dose ya kuku 1000 basi nilikuwa ninawapa kuku wangu wote. Kwa kufanya hivyo uwezekano wa kukutana na chanjo nzima ambayo haijaharibika ulikuwa mkubwa. Pia nilikuwa sinunui chanjo toka chanzo kimoja, nilikuwa nikinunua toka kwa wauzaji tofauti. Mara zote nilinunua kwa wauzaji waaminifu tu.

Kuna wakati pia kama alivyodokeza mchangiaji huko nyuma nilifanya kama tabia yangu ninapowawekea chakula kuku wangu nilikuwa nikichangaya na mashudu ya mwarobaini. Kulikuwa na kiwanda cha kukamua mafuta ya mwarobaini kutoka kwenye matunda yake. Kwa kufanya hivi nadhani nilitibu kuku dhidi ya magonjwa nyemelezi yanayoendana na mdonde. Kama uko eneo ambalo kuna miti ya miarobaini kipindi cha matunda yake yanapokomaa au kuiva yavune yaanike na uyasage kwa kutumia kinu au njia yoyote upate unga. Kikombe kimoja hadi viwili saizi ya kikombe cha chai kinatosha kuchanganya kwenye debe moja la chakula.

Minyoo:
Nikiwa katika ufugaji wangu kuna wakati nilikuwa ninawasahau kuku wangu. Nilikuwa ninazidiwa na majukumu mengine kiasi cha kutofuata kanuni za matunzo ya kuku. Kipindi hicho niliwahi kushuhudia kuku wanapotoa kinyesi kilikuwa kina minyoo kibao hali ambayo ilinitisha sana. Hakika inapaswa kuwa karibu sana na hawa viumbe! Kuku wa kienyeji kweli ni kuku wastahimilivu sana. Huwa tunawatazama na kudhani wako salama lakini yanayoendelea miilini mwao ajuae ni Mola tu. Laiti kama tunaweza kuwa karibu nao zaidi kwa kuwakagua kagua mara kwa mara tunaweza kuwafanya wakastawi zaidi kwa maana sitarajii mfugaji yoyote mjasilia mali kweli kama akiona minyooo kwenye choo cha kuku hatachukua hatua yoyote kutibu kuku. Kuku wanapokuwa kundi kubwa, ukiona mmoja yamemfika ujue wapo wengi hujawagundua. Niliwahi chinja kuku mmoja na kumpasua utumbo mdogo nilikuta vitu vya kutisha, alikuwa amesheheni minyoo! Ilifikia baadhi ya minyooo walikuwa wameutoboa utumbo, utumbo ulikuwa una madonda, tulimchinja kuku huyu baada ya kumwona hajachangamka kama wengine! Wataalamu wanashauri kuwapatia kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu! Nililijua hilo lakini nilikuwa nazembea hadi niliposhuhudia kuku akijisaidia minyoo. Baada ya kukuta minyoo ndani ya tumbo la kuku wakiwa wamefikia kiwango cha kuwa wanatoboa utumbo nilijifunza sana ni kitu ambacho hakitakuja kuwatokea kuku wangu tena!! Kila wanachoelekeza wataaalamu tukifanye wanasababu muhimu twapaswa kuzingatia maelekezo ya wataalamu daima.

Chawa na utitiri na viroboto
Watu wengi wanafahamu kasheshe za viroboto na utitiri linapokuja suala la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Tuliokulia vijijini tukilala na kuku ndani ya nyumba adha ya utitiri na viroboto tunaifahamu vema! Wengine pia hasa tuliopitia JKT tunaifahamu adha ya chawa! Hawa wadudu pamoja na kwamba wananyonya damu ya kuku na kumdunga vimelea vya magonjwa pia huwa ni kero sana kwa viumbe hawa! Hii kero ambayo tunaijua kwa namna ile ile ambayo binadamu unakerwa kuku nao hukerwa hivyo hivyo. Na hii hupunguza uzalishaji na ukuuji wa kuku. Viroboto ni adui mkubwa kabisa wa vifaranga! Viroboro vinaweza kumaliza vifaranga wote ndani ya siku mbili tu baada ya kutotolewa! Nilishajua viroboto ni hatari kubwa kwa vifaranga. Iwapo kuku anaatamia naye anaviroboto nilielewa hilo ni bomu litakalolipukia kwa kuua vifaranga.

Jambo ambalo sikuwa nalifahamu kiurahisi ni kuwa kuku wengi huwa wamesheheni chawa mwilini. Kuku wa Malawi ndiyo waliniamsha kugundua kitu hiki. Kuku wa Malawi nahisi damu yao ilikuwa TAMU iliyopendwa sana na chawa na hata viroboto! Kuku wa Malawi walikuwa wakishambuliwa saaaaaaaana na viroboro na chawa kiasi nilikuwa nashangaa sana! Toka hapo nilijenga tabia ya kukagua kuku mara kwa mara kwa kuwafunua manyoya hasa ya kuanzia kifuani na tumboni, na mara nyingi kuku akiwa na chawa huwezi kuwakosa eneo la kuzunguka mkiani na hasa kuzunguka sehemu ya kutokea haja kubwa eneo ambalo huwa na joto kubwa zaidi. Nilikuja kubaini kuwa kuku karibia wote tunavyowaona huwa wamesheheni chawa mwilini! Ndiyo kisa kuku huwa wanaoga kwenye vumbi kupunguza udhia wa chawa. Funua manyoya! Kuku wanapokuwa wanajipekua pekua jua wanachawa mwilini.

Kuku hupunguza matatizo ya chawa kwa kuoga kwenye vumbi! Hili ni eneo ambalo pia nilikuwa ninaliwekea dawa ili wakija kuoga vumbi wajipake dawa kisawasawa. Nilikuwa nikinunua SEVIN (wakati haijachakachuliwa), nilikuwa nikiwadondoshea ndani ya manyoya kila miezi mitatu. Kabla sijamweka kuku kuatamia mayai nilikuwa lazima nimyunyinzie dawa ndani ya manyoya yake na kisha kwenye kiota ili awe na utulivu wakati wa kuatamia.

Utitiri nilikuwa ninauangamiza kwa kupuliza dawa za kuua wadudu za kawaida zitumikazo bustanini kama Thionex, Karate, Selectron kwa kutumia sprayer kubwa ya kubeba mgongoni. Kabla sijapuliza dawa kwenye chumba cha kuangulia vifaranga, Kuku wanaoatamia niliwaondoa kwa muda. Kabla sijapulizia dawa bandani nilikuwa ninawafukuza kuku wote bandani wakati wa mchana na nilikuwa ninapulizia kila kona ya banda la kuku chini, kutani na hata paani. Ulipofika usiku kuku wote niliwanyunyizia SEVIN ndani ya manyoya yao..

Viroboto nilikuwa ninawapaka mafuta ya taa kuku wote walioathirika. Kazi hii ilifanyika usiku! Mafuta ya taa yalikuwa yakiokoa sana vifaranga. Baadae nilielezwa kuwa hata mafuta ya kula yakipakwa yanaweza kuuua viroboto walioganda vichwa vya kuku. Sikuwahi kujaribu.

Tuendelee kujadiliana na maswali yanakaribishwa, ITAENDELEA…………………
 
Baba JJ;

Huyu kamanda wetu Kubota bila shaka ile Bedford anayotumia katika kubebea mkaa wake itakuwa imekwama kutokana na mvua inayoendelea sehemu mbalimbali!

Kubota; hebu zunguka huku tafadhali! Nakukumbusha tena ya kwmb wale vifaranga nilimwuliza Mama Joe utaratibu wake hakika wameanguliwa karibia wote, je? Kuna dawa yoyote niwapatie wakati wanaendelea kusubiria ile chanjo ya kideri ya matone?


TANESCO BWANA!, wanaweza kuwa wamesababisha kukatika kwa hii nyuzi. wakirudisha umeme nafikiri mkuu ataunganisha alipokomea.

waiting.....................................
 
Last edited by a moderator:
Baba JJ;

Huyu kamanda wetu Kubota bila shaka ile Bedford anayotumia katika kubebea mkaa wake itakuwa imekwama kutokana na mvua inayoendelea sehemu mbalimbali!

Kubota; hebu zunguka huku tafadhali! Nakukumbusha tena ya kwmb wale vifaranga nilimwuliza Mama Joe utaratibu wake hakika wameanguliwa karibia wote, je? Kuna dawa yoyote niwapatie wakati wanaendelea kusubiria ile chanjo ya kideri ya matone?

Wakuu Baba JJ na LiverpoolFC kama umeme unazingua labda kwenu mimi huku kwangu fresh mbona ninapost threads kama kawa, leo niko kikazi nilishapost several times tu. Kuhusu swali lako,..... Yes wapatie antibiotics kuzuia magonjwa wanayotoka nayo kwenye mayai! Hizi dawa za kutibu magonjwa za antibiotics huwa kuna dose kwa ajili ya kukinga kuku! Si lazima kutibu hadi uone ugonjwa bali vifaranga hunaweza kuwa wametotolewa wakiwa wanavimelea vya maradhi! Nenda duka la madawa ya mifugo ongea nao juu ya hii kitu watakupa dawa ambayo iko sokoni kwa sasa!
 
TIP
Wakati nikiendelea na maandalizi ya post nyingine naomba niweke kwa kumbukumbu tu kuwa uzoefu wangu kuhusu utagaji wa kuku wangu wa kienyeji wakiwa katika ustawi mzuri, idadi ya mayai kila siku ilikuwa sawa na theluthi moja ya idadi ya kuku majike yote. Kwa kuku wangu majike 30 nilikuwa naokota mayai wastani wa 10 kila siku ambapo kuku 10 walikuwa wakitaga , 6 wametoka jela wanasubiri waanze mzunguko mwingine wa kutaga na 8 wanaatamia mayai na 4 wanalea vifaranga! Ukifuata utaratibu wa kuwapa kuku wachache waatamie na kuwapa kuku wachache wakuze vifaranga unaweza kukuta kila siku kuku kuna kuku wanaotaga mayai. Usipofuata utaratibu huu kuna wakati kuku wengi huwa kweny kipindi cha kutaga mayai na kuna kipindi kuku wengi huwa hawatagi.
 
Wakuu Baba JJ na LiverpoolFC kama umeme unazingua labda kwenu mimi huku kwangu fresh mbona ninapost threads kama kawa, leo niko kikazi nilishapost several times tu. Kuhusu swali lako,..... Yes wapatie antibiotics kuzuia magonjwa wanayotoka nayo kwenye mayai! Hizi dawa za kutibu magonjwa za antibiotics huwa kuna dose kwa ajili ya kukinga kuku! Si lazima kutibu hadi uone ugonjwa bali vifaranga hunaweza kuwa wametotolewa wakiwa wanavimelea vya maradhi! Nenda duka la madawa ya mifugo ongea nao juu ya hii kitu watakupa dawa ambayo iko sokoni kwa sasa!



Kubota nashukuru na ngoja nielekea hapo kwa akina Malila na bila shaka wataninusuru! Ila kuna siku wameniudhi sana kwani nimechukua dawa ya minyoo pale dukani kwao Alpha Vetenary ikawa imekwisha muda wake na nikawa pigia simu kwa mbona mambo iko hivi wakaniambia niwarudie ila kwa kweli niporudi pale wakanigeuka kwani wameniambia kale choo cha kuku kama bado wana minyoo!
Hiyo kauli yao ilinichefua mpaka nikahama phamacy ile ingali niliwakubaligi kwa dawa zao ya kwamba hawachakachui!

Ngoja niwajaribu tena!
 
Last edited by a moderator:
Kubota nashukuru na ngoja nielekea hapo kwa akina Malila na bila shaka wataninusuru! Ila kuna siku wameniudhi sana kwani nimechukua dawa ya minyoo pale dukani kwao Alpha Vetenary ikawa imekwisha muda wake na nikawa pigia simu kwa mbona mambo iko hivi wakaniambia niwarudie ila kwa kweli niporudi pale wakanigeuka kwani wameniambia kale choo cha kuku kama bado wana minyoo!
Hiyo kauli yao ilinichefua mpaka nikahama phamacy ile ingali niliwakubaligi kwa dawa zao ya kwamba hawachakachui!
Ngoja niwajaribu tena!
Kila la kheri mkuu nilisahau, vitamini kuanzia siku ya kwanza ni nzuri kama iko na antibiotics mie walinipa OTC plus for 2 weeks
 
Kubota asante sana barikiwa nimejifunza mengi kuhusu kuku wa kienyeji mpaka sasa, endelea kutujuza mengine pia hasa security, ila uache nyara za serikali ukikamatwa mbaya sana
 
Kubota ahsante sana kwa som lako. ninakufuatilia kwa karibu sana.Bodonachanganyikiwa kwenye eneo la chanjo, ngoja nitulie nisome hatua kwa hatua.Hii chanjo ya mdondo ya kuweka kwenye maji inaitwaje?
Mama Joe ahsante nimekupata kama ifuatavyo;
1. Osha banda kwa V-rid na vyombo ulivyotumia kwa kuku wakubwa
2. wakiwa na siku tatu wape chanjo ya mdondo rudia wiki ya 3 na kila miezi 3
3. Ukiweza wape vitamini walau wiki 2 za mwanzo
4. wiki ya pili wape chano ya gumboro
5. unaweza kuwapa coccidiostat au ukaacha ila be on standby wakionyesha dalili za coccidiosis
6. kikubwa jitahidi usafi wa banda na vyombo epuka watu kuingia ingia na kushare vyombo na kuku wakubwa
7. ukiweza tumia waterguard walau wiki 2 za mwanzo kwenye maji, kizibo kwa lita 20 yanatumika hata siku 2

Kila la kheri mkuu nilisahau, vitamini kuanzia siku ya kwanza ni nzuri kama iko na antibiotics mie walinipa OTC plus for 2 weeks​



Stay blessed.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mama Joe; ila ningependa kujua hii chanjo ya kideri ni muhimu kuwapa kwa muda gani vifaranga kama hawa?


Kila la kheri mkuu nilisahau, vitamini kuanzia siku ya kwanza ni nzuri kama iko na antibiotics mie walinipa OTC plus for 2 weeks

Nimefika hapa Interchick na wamenipa dawa hii CHICKMYCIN na ngoja nitarudisha majibu hapa hapa baada kuanza matumizi kwa vifaranga!
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mama Joe; ila ningependa kujua hii chanjo ya kideri ni muhimu kuwapa kwa muda gani vifaranga kama hawa?




Nimefika hapa Interchick na wamenipa dawa hii CHICKMYCIN na ngoja nitarudisha majibu hapa hapa baada kuanza matumizi kwa vifaranga!

newcastle au mdondo wanapewa siku za mwanzo ila wengi tunaanza na vitamin kuvipa nguvu si unajua vinakuwa dhaifu. Pia ukiweka maji jitaidi iwe ulitoa vyombo mfano asubuhi sana ukawaacha wale wakipata kiu unaweka chanjo kama saa tatu ili wote wanakuwa na kiu unayaacha masaa 2 unatoa unaweka ya kawaida na vitamin. Jitaidi kuwasogeza wote wanywe dawa. Baada ya wk tatu unarudia tena.
 
Last edited by a moderator:
newcastle au mdondo wanapewa siku za mwanzo ila wengi tunaanza na vitamin kuvipa nguvu si unajua vinakuwa dhaifu. Pia ukiweka maji jitaidi iwe ulitoa vyombo mfano asubuhi sana ukawaacha wale wakipata kiu unaweka chanjo kama saa tatu ili wote wanakuwa na kiu unayaacha masaa 2 unatoa unaweka ya kawaida na vitamin. Jitaidi kuwasogeza wote wanywe dawa. Baada ya wk tatu unarudia tena.



Nashukuru sana Mama Joe na bila shaka tu pamoja mwanzo mwisho!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mimi nina dada yangu anatarajia kuanza ufugaji wa kuku wa mayai. Kwa jinsi nilivyo ongea naye hana utaalamu mkubwa. Kama sijachelewa naomba na mimi unitumie mchakato mzima kwenye PM. Pili mimi nimgeni kwenye hii site na nimefurahi sana wana JF kwani hii site imenifumbua macho sana. Hapo nyuma niliona post yako kuhusu kilimo kwanza (Mahindi) kwangu mimi hii ilikuwa mpya kabisa kwangu na nilifurahi sana kuona kuwa nyumbani kuna mambo mengi ya kufanya. Nilikuwa naomba uni update kuhusu kilimo. Mambo yalikuwaje? Thank u.
 
Back
Top Bottom