mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,682
- 10,801
Mama Joe kusema kweli umenitia moyo sana kwa kuweka wazi uzoefu wako khs hawa kuku chotara, nimesoma comments zako zote nimefarijika sana, hata nashindwa niseme nini tu kuelezea furaha yangu!Namshukuru Mungu na ushauri wenu ni kweli tukikazana tutaweza tu, changamoto kubwa ni magonjwa ya ghafla kutokea ila nashukuru yaani kila likija hili unakuta mwingine hapa kesha leta na ufumbuzi umejadiliiwa yaani imenisaidia sana sikuwa na Dr yoyote wa mifugo zaidi ya kupata ushauri hapa, kwa RETI na kwenye phamarcy. Sikutaka kuchukua mkopo nilitaka niende taratibu kwa kujibana tu na kupunguza matumizi yasiyo lazima. Naomba nikutie moyo mama Timmy kuku chotara hawana tofauti na hawa kienyeji kwa kulisha na dawa, mimi nimefuga wale wa kisasa ndio nimehamia kwa hawa, ukuaji wa hawa chotara ni wa haraka wakati hawahitaji gharama kubwa kihivyo maana hawali chakula kingi kama wakisasa wala hawahitaji vitamin isipokuwa wiki chache 2 za mwanzo. Kwavile wanakua haraka tayari wakifika kiezi 5 tu unauza kwa 10000 lakini ukiwaacha hadi miezi 8 jogoo ni wakubwa sana na wanauzwa 15000 -20000. Unakuwa huna pressure ya kukubali bei ndogo maana hawali chakula kingi. Faida ya pili wanataga mapema kuliko wa kienyeji hivyo wanaanza kujilisha wenyewe wakiwa na miezi 6 kuendelea na vilevile waweza kuwatumia mayai yao kutotoa vifaranga aidha kwa kuwatumia tetea wa kienyeji pure au incubator na hivyo kutokuwa na haja ya kununua tena vifaranga wengine. Nitajaribu kuweka mchanganuo wa gharama na faida ingawa nikiangalia sio tofauti na iliyowekwa na RETI hapahapa. Lengo langu ni kuongeza aina nyingine ya kuku chotara ili kuwa na aina tofautitofauti, kuanza kutengeneza chakula changu mwenyewe kupitia formula nilipewa na ex SUA lecture na Dr mifugo sasaivi yuko wizarani yeye na mkewe wameitumia na waliniambia inafaa sana ingawa itabidi nipate ushauri wa mwenye mashine kiwango cha usagaji na uchanganyaji wa chakula nitaleta feedback hapa. Nawashukuru wote kwa michango yenu Mungu azidi kuwafanikisha zaidi ktk malengo yenu.
Naomba kujua namna ya kuwapata na bei zake, manake nataka nianze kuwafuga mwezi ujao kuanzia tar 20 hivi, uzuri banda ninalo so ni kiasi cha kulifanyia usafi tu na kuandaa pesa kwaajili ya kuwanunua. Nalenga kuwafuga kwa ajili ya mayai so nitahitaji majike.
Last edited by a moderator: