Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Malila niambie breed ya jogoo nzuri naazisha shamba lingine la kuku
 
Last edited by a moderator:
Kwemisaa Jaribu kuwapa majani ya alovera yatwange yachanganye na maji. Asubuhi na jioni
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru Kamuzu kwa kuonyesha uwepo wako nilifikiri niko mwenyewe tu peke yangu hapa jukwaani maana wakubwa wamekasirika wameondoka kwa kuwa nimechelewa kuwasilisha, jamani tuvumiliane!

Nilivyoendelea kufuga baada ya kuona kuwa kuku wanaoatamia wanapata usumbufu sana kutoka kwa kuku wanaoendelea kutaga, Banda langu la kuku nililigawa kukawa chumba na sebule! Nitaeleza wakati ukifika nilivyojenga mabanda yangu. Kwa hiyo chumbani niliweka viota na ndiko ambako nilikuwa nawaweka kuku wanaoatamia ili wasibughudhiwe kabisa na kuku wenzao, mlango wa kuingia chumbani nilitengeneza geti la mianzi iliyopigiliwa karibu karibu kuzuia kuku kupenya. Hapo sebuleni ndiko kuku wote watagao na wasiotaga walikuwa wanalala, kwa hiyo kulikuwa na viota vingi ambavyo juu yake nilikuwa naviwekea kizuizi kwa kutumia Mabanzi ya mbao ili usiku kuku wengine wanaposimama juu yake wasichafue kwa kinyesi chao kwenye viota. Viota hivi nilikuwa navitengeneza kwa kuweka partitions (yaani vijivyumba) kwa kutumia tofari za tope, zenye saizi kama ya matofali ya kuchoma. Kwa hiyo kwa kuambaa ukuta nilikuwa nalaza tofari nne chini kwenda juu, nilifanya hivyo kila baada ya upana wa futi moja, juu ya hizo tofali ndiyo niliweka Banzi! Ndani ya hivyo vijivyumba nilitifua umbo kama kijibeseni na kuweka Majani laini ili mayai yatulie yasisambae. Huko chumbani wakati wote kulikuwa na chombo chenye chakula na chenye maji! Hakuna kuku kutoka na hakuna kuku wa kuwaingilia! Ilikuwa ni incubator TOSHA! Nilikuwa nawaona kuku kama wananishukuru kwa kuwatengenezea mazingira safi maana walikuwa hawabughudhiwi na walikuwa wanashiba chakula vizuri tu! Nitaeleza siku nyingine juu ya harakati zangu za kutengeneza chakula na changamoto nilizokutana nazo! Huko chumbani nilikuwa nimetandaza carpet la nyasi; kando kando ya kuta zote kulikuwa na viota ambavyo nilivizamisha ndani ya hilo kapeti la nyasi nadhani mtanielewa! Ninaposema carpet la nyasi, ni nyasi tu nilizisambaza kwa unene wa kama sm 15 au nchi sita! Kwa hiyo kipindi hawa kuku wanapokuwa wanaatamia nilikuwa nazuia wengine wasiatamie hadi hawa watakapototoa! Kwa hiyo mayai yanayopatikana wakati hawa wengine wanaatamia nilikuwa ninakula na mengine kuuza maana mpango wangu ilikuwa kutotolesha mara moja tu kuku mia kwa mwezi! Hii ndiyo Incubator yangu ambayo nilikuwa ninatotolesha vifaranga 100 kwa siku moja!! Kwa kuwa nilikuwa ninajukumu pia la kulea kuku utotoleshaji nilikuwa ninaudhibiti uendane na miundombinu yangu ya kulea kuku na vifaranga.

ITAENDELEA ............

Hongera sana kwa mafanikio ya kufuga kuku

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
ahsante mkuu kubota
jamani wanajamvi kuku wangu anatoka uvimbe jichoni kama majipu ni ugonjwa gani naomba msaada kwa anayefahamu nitumie dawa gani
 
Pia kati ya hawa wa mayai na kienyeji bora wa kienyeji kwasababu hizi..
1.Wastahimilivu wa magonjwa
2.Hawachagui sana chakula
3.Hawana masharti sana ya ufugaji
4.Pia muda wao wa kutaga ni sawa na hao wa mayai
5.mayai bei nzuri na yana market sana

Nakushukuru sana kwa Mchango wako, Baada ya kusoma maelezo yako nafikiri Nitajishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji, ufugaji wangu utakuwa wa ndani ya banda

SWALI
wale kuku Machotara wanauwezo wa kuhatamia na kutotoa mayai?
 
Hapana machotara hawatamii lakini mayai yao yanambegu so ukiweka kwa incubator yanatoa vifaranga
 
Mimi nimechanganya chotara na pure...but naona pure hawaugui sana kama chotara ikiwa chanjo walipata..na hata kama hawakupata ni wastahimilivu sana..now my focus will entirely rely on pure... Nawafata mkoani mwenyewe then ntawapa intensive care ili waweze kuzaliana na kustahimili Magonjwa...
 
Wakuu mimi pia napenda kufuga kienyeji pure. Ninao kama 20 kutoka 4 nilioanza nao na watatu wamelalia. Hadi sasa nawafuga huria ila nawapa chakula starter, finisher kutegemea umri zaidi wanaokota nje. Ninataka kuwafuga kitaalamu, naweza kuwafuga ndani? Labda na space ndogo ya kucheza nje. Nilijaribu muuliza mtunzaji alinijibu watapigana hadi wafe! Jinsi gani niwafuge wengi mfano hata 100 wa umri mmoja kwenye banda moja kama tunavyofanya kwa chotara?
 
Kuku wa mayai wana faida sana
Me ninao wa mayai na kwa wiki naingiza zaid ya M 1 na nusu.
 
Hongera naelewa, ila wanataka capital kubwa uwalishe chakula maalum miezi 5 ndio waanze kutaga. Kwa kuku 1000 uwe na wastani 5ml. Ila ni investment nzuri sana.
Kuku wa mayai wana faida sana
Me ninao wa mayai na kwa wiki naingiza zaid ya M 1 na nusu.
 
Mama Joe nadhani itavuka m 5...kwa wataalam wanaestimate 9m kwa miezi hiyo kwa kuku 1000.Pia kuna sehem nimepata kuku wa kienyeji kwa bei nzuri ya elf 6500 ni pale chamwino barabarani mnaweza chek pale
 
Mama Joe nadhani itavuka m 5...kwa wataalam wanaestimate 9m kwa miezi hiyo kwa kuku 1000.Pia kuna sehem nimepata kuku wa kienyeji kwa bei nzuri ya elf 6500 ni pale chamwino barabarani mnaweza chek pale

Chamwino ya wapi unayo izungumzia hapa.... mimi najua chamwino ya Dodoma na ile ya Morogoro.
 
Asante kwa taarifa, labda tuulizie wa malori maana pande hizo sina mtu.
Mama Joe nadhani itavuka m 5...kwa wataalam wanaestimate 9m kwa miezi hiyo kwa kuku 1000.Pia kuna sehem nimepata kuku wa kienyeji kwa bei nzuri ya elf 6500 ni pale chamwino barabarani mnaweza chek pale
 
Malila niambie breed ya jogoo nzuri naazisha shamba lingine la kuku

Unataka chotara au pure kienyeji? Unawafahamu kuku chotara ya kuchi na kienyeji wanaoitwa bokea? Hawa ni majogoo wakubwa kwa umbo na uzito mkubwa. Je nikuunganishe na mdau wa hawa jogoo? Yupo Mbezi, njia ya Kisiju.
 
Nimerudi wakuu,
Sikuwa na access ya mtandao,
baada ya kurudi bongo ninaishi mbugani mtandao hakuna,
nikienda mjini sikupata nafasi kuingia internet Cafe!!
Lakini ivi sasa problem is solved !!!
Mama Joel, ninafuga Vyotara, sirudi nyuma kwenye pure kienyeji, wanakua kwa spidi sana,
Mama Timmy, Asigwa, Liverpool FC, wachangiaji wote na wasomaji wetu,
nimefurahi kukuta Thread haijapelekwa Archive !!
Nyote nawapenda sana, tuendelee kujuzana!
 
Pia kati ya hawa wa mayai na kienyeji bora wa kienyeji kwasababu hizi..
1.Wastahimilivu wa magonjwa
2.Hawachagui sana chakula
3.Hawana masharti sana ya ufugaji
4.Pia muda wao wa kutaga ni sawa na hao wa mayai
5.mayai bei nzuri na yana market sana

Kuna mtu yeyeto katika nyie mnaofuga amefanya interbreeding?
 
Back
Top Bottom