pichuwanyi
Member
- Jan 13, 2011
- 21
- 7
Sasa kila mtu akifanya biashara ya maduka nani atafuga kuku? Ndio maana bei ya mayai inapanda kila kukicha kwasababu watu wameikimbia hii biashara. Kama mtu anaushauri mzuri wa kufuga kuku plse atujuze wengine tuna interest
Kuku ni biashara nzuri sana lakini inabidi uwe mjanja, kwanza jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe, usiwe unanunua. Pili usiwe mbahili. Hakikisha wanakula vizuri na madawa ya kupulizia kwenye mabanda unatumia. Anza na kuku 2000,
good luck.
Nimeanza majaribio ya ufugaji kuku wa kienyeji na vijogoo, lakini tatizo kubwa ninalolipata ni huu ugonjwa wa kushusha mabawa (kuvaa koti)Coccidiosis! Ninaweza kupata ushauri wa nini kinga na matibabu yake. Nawasilisha wakuu..
Heshema wana JF, nataka kufuga kuku wa kisasa lakini sehemu nayotaka kwenda kufugia umeme haujafika bado naombeni njia nyengine ya kusolve tatizo la umeme.
Nilinunua kigari na kufilisika kwa biashara hii hii
YES, kama ulifuga bila kufuata masharti na uangalizi wako ulikuwa duni nakubali hata nyumba ungeuza bora umeshituka mapema marytina. Sisi tunapeta tu na biashara hii hii.Nilinunua kigari na kufilisika kwa biashara hii hii
Kuku ni biashara kichaa, nimekulia kwenye ufugaji nawajua mwanzo mwisho. Kama wataka biashara mbadala ya kuku nakushauri uanze totoresha vifaranga vya kuku. Nenda sido (karibu na airport) wapo jamaa wanatengeneza incubators. au ng'ombe wa maziwa.
Tray moja ya kuku wa kisasa ni sh elfu 6,na ya wakienyeji ni elfu 7 na mia tano.hiyo ni bei ya jumla.wa dsm ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!
Tray moja ya mayai wa kuku wa kisasa ni sh elfu 6,na ya wakienyeji ni elfu 7 na mia tano.hiyo ni bei ya jumla.wa dsm ebu nambien tray moja ya mayai kuku wa kisasa ni sh ngap? na kienyeji ni sh ngapi, nitaingia apo muda si mrefu!