CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Uko sahihi sana mheshimiwa neggirl,ndio maana tunashauri ni muhimu sana mfugaji akawa anatengeneza chakula mwenyewe kwani atazingatia mahitaji halisi ya formula bila kuzidisha wala kuacha ingriedient yoyote. Kwa upande wa madawa ni muhimu ukawa wasiliana na wataalam wa mifugo kusudi upate dawa bora. Na vifaranga pia ni vyema ukaagiza kutoka kwenye makampuni yanayojulikana na yenye sifa ,vinginevyo utakuwa mwenye kupata hasara siku zote. Uchakachuzi ni mkubwa sana.
Mtaalamu nimerudi tena, niliweka kwa majaribio hawa kuku wa kienyeji chotara aina mbili
1. Wa Malawi, weusi
2. Cornish brown / kuchi
sasa nikiangalia wa malawi wanaanza kutaga mapema pia wanataga ata least kila leo, hawa cornish naona wana endelea kukua tu bado hawajaanza kutaga ila wana maumbo makubwa, nimecheck mtandaoni naona wanasema hawa cornish ni wazuri kwa nyama kwani wanakua na maumbo makubwa lakini sio wazuri kwa mayai yaani hawatagi sana na hawa weusi au black australorp wazuri kwa mayai.
Jamani kama kuna mwenye uzoefu na hawa naomba kujuzwa ili ninaponunua vifaranga nijue nitafute soko la nini mayai au nyama.
Asante
Kwa kawaida kuku wowote wenye maumbo makubwa si watagaji sana hata ukiagiza kuku wazazi wa kuku wa nyama nao wako hivyo hivyo.Hao kuku wa malawi weusi sio pure wa kienyeji ni machotara,hivyo wamechukua tabia ya utagaji kutoka kwa kuku wa kisasa na pia wamechukua ustahimilivu dhidi ya magonjwa kutoka kwa kuku wa kienyeji.
Cornish brown sina hakika sana kama ndio wanaitwa Kuchi,kwani ninachofahamu mimi ni kuwa Kuchi ni kosaafu ya kuku wa kienyeji ambayo inapatikana mikoa ya kati na maghari ya Tanzania.Ni kosaafu bora sana miongoni mwa kosaafu za kuku wa kienyeji zinazopatikana hapa nchini.Huwa wana warefu na wenye maumbo makubwa.
Kitu ambacho naweza kukushauri kwa hao cornish brown wako ili watege ,wapunguzuie chakula wanachopewa kwa siku ili wapunguze mafuta.
Mkuu sijakuelewa hapo Kuchi ni pure breed ya Kienyeji au ni cross breed ya kienyeji na kisasa?
Kuchi ni pure breed ya kienyeji,inapatikana hapahapa nchini kwetu.Ni kosaafu bora sana kati ya kasaafu za kuku wa kienyeji zinazopatikana hapa nchini.
Mkuu hao kuku nitapata Vipi Vifaranga wao? kuna mtu anamjua anaye zalisha vifaranga origino wa Kuchi?
Kuchi ni pure breed ya kienyeji,inapatikana hapahapa nchini kwetu.Ni kosaafu bora sana kati ya kasaafu za kuku wa kienyeji zinazopatikana hapa nchini.
Kosaafu maana yake ni koo au breedHapo kwenye hilo neno Kosaafu ndo unaponiachaga,okay thanks kwa jibu nimekuelewa walau
Sorry sikuiweka vizuri hawa cornish ni breed ya nje na imekrosiwa na kuchi, na hawa weusi pia ni australorp imekrosiwa na kienyeji ingawa sijui breed gani, wote ni chotara kama usemavyo nimeamua kuwapunguzia ratio ya chakula toka jana nione inakuwaje, nimeisha oda batch ya hawa cornish kwa hivyo ninawaangalia ili nijue wanakuwaje. Nashukuru sana kwa maelezo.Kwa kawaida kuku wowote wenye maumbo makubwa si watagaji sana hata ukiagiza kuku wazazi wa kuku wa nyama nao wako hivyo hivyo.Hao kuku wa malawi weusi sio pure wa kienyeji ni machotara, hivyo wamechukua tabia ya utagaji kutoka kwa kuku wa kisasa na pia wamechukua ustahimilivu dhidi ya magonjwa kutoka kwa kuku wa kienyeji.
Cornish brown sina hakika sana kama ndio wanaitwa Kuchi,kwani ninachofahamu mimi ni kuwa Kuchi ni kosaafu ya kuku wa kienyeji ambayo inapatikana mikoa ya kati na maghari ya Tanzania. Ni kosaafu bora sana miongoni mwa kosaafu za kuku wa kienyeji zinazopatikana hapa nchini.Huwa wana warefu na wenye maumbo makubwa.
Kitu ambacho naweza kukushauri kwa hao cornish brown wako ili watege, wapunguzuie chakula wanachopewa kwa siku ili wapunguze mafuta.
Kuhusu gharama za kufuga kuku 100 wa nyama jaribu kupitia post za nyuma.Kwa gharama za incubator tuwasiliane.Nashukuru kwa mawazo mazuri, naomba kujua mtaji wa kuanzisha ufugaji wa kuku wa nyama 100 na pia hizo mashine za kutotolesha zinauzwaje.
Ni sawa inawezekana ila ni muhimu kuzingata kuwa paa liwe juu ili kuzuia joto kwani turubai hutoa joto kali sana.Mkuu nataka kujenga Mabanda kwa tofali, Ila juu nafunika vizuri na turubai kwamuda lakini baadae nikpata pesa naweka Bati, Vipi ni sawa mkuu?
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.